Nataka kukueleza Kitu, Kaa utulie. Hivi!, Unajua sisi ni wapuuzi sana.
⁰00000000000000000000000000000⁰
Ngoja nikusimulie...
Kwa jina xoxo nina akaunti Benki ya NMB. Kuna huduma ya nmbsimbanking ambayo inakupatia huduma zote za kibenki Kwa mtandao, yaani kidigitali. Kwa hiyo mteja mwenye simu akiwekewa Hela au kutoa kwenye akaunti yake ya benki ni lazima meseji itumwe kwenye namba ya simu yake kwamba Fulani amekuwekea kiasi kadhaa siku ya Leo muda huu. Pia mtu akitoa hela vivyohivyo unatumiwa meseji kwenye simu yako kwamba kiasi kadhaa kimetolewa katika akaunti yako muda huu. Sharti la kwanza la huduma hii ni kwamba lazima meseji ifike muda huohuo. Ikichelewa meseji ni makosa.
****""$$$$$$$$$$$__&-$$$3333
Ama la uwe umezima simu ama upo nje ya mawimbi ya mtandao. Kwa hiyo ikitokea mtoa huduma Kwa kujisahau ama kwa kutumia ujanja ujanja kwa kutegemea ujinga wa mteja wake kulazimisha kuuza huduma ileile Moja zaidi ya mara moja ni makosa.
Namaanisha nini?
Nitoe sinario ya kwanza.
Nabonyeza menyu ya Benki ambayo ni *150*66# ikumbukwe kwamba Benki na mtandao wa Airtel hawajakubaliana kufanya biashara pamoja hivyo Kila mtu anakata chake mapema.
Najibiwa na kompyuta kwamba Ili kuruhusiwa kutumia menyu hiyo ni lazima Airtel wakate shilingi mia. Sawa Kwa kuwa nimeweka vocha ya jero shilingi mia si kitu acha wakate tu. Basi nimebonyeza ok kuruhusu na kweli menyu inafunguka na meseji inaingia kwenye simu kwamba mtandao wa Airtel wamechukua mia Yao Kwa kukuunganisha na benki yako.
Sasa endelea na huduma Benki.
Basi Kwa mawazo yangu nikajua kuangalia Salio ni Ile mia iliyokatwa na Airtel nikisahau kuwa Sasa nipo ndani ya mtandao wa Benki nikacheki Salio.
Kucheki Salio wanakata 500 Kwa hiyo kama una 5000 inabaki 4500. Pia kumbuka kwenye simu baada ya kuweka vocha walikata mia Kwa hiyo imebaki 400 tupo pamoja mpaka hapo?
Ukishapata Salio kwenye menyu ya NMB hakuna kitufe cha kurudi nyuma.
Network inakata . Inakulazimisha uanze upya ili ulipe shilingi mia nyingine kwenye mtandao wa simu yaani Airtel.
Ok Ina maana hata ukikosea chaguo mfano ubonyeze mbili halafu utake kurudi kwenye menyu kuu ili ubonyeze moja haikuruhusu. Lazima uanze upya Ili ukatwe shilingi mia nyingine. Huo ni wizi.
Sisi tuliosomea mtandao Tena kwa pesa za walipa kodi maskini wenye uelewa wa chini ni lazima tuwe wazalendo. Watu hawa wametutuma twende tukasome Kwa niaba yao, Leo hii kutumia ujuzi wetu kuwaibia waliotuagiza Kwa kisingizio cha kwamba chukua chako mapema SI halali.
Basi nifunge mjadala ni hiviiii, tumepotoka