Kwako Mkuu wa Mkoa wa Kigoma

Kwako Mkuu wa Mkoa wa Kigoma

johnmashilatu

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2010
Posts
841
Reaction score
909
C&P
Kwako Mkuu wa mkoa wa Kigoma. Salaam.

Sisi ni wahudumu wa Afya ngazi ya jamii ( CHW's) kutoka tarafa za Buhingu na Ilagala wilaya ya Uvinza mkoani kigoma. Idadi yetu ni 80( themanini).

Mwezi Juni mwaka huu, ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma (RMO) kupitia kwa Mganga mkuu wa wilaya(DMO) ya uvinza walitualika kushiriki mafumzo ya wiki moja kuhusu kukabiliana na magonjwa ya mlipuko pamoja na Malezi Bora.

Mafunzo haya yalifanyika Ilagala Centre ambako, washiriki waliahidiwa kulipwa pisho ya shilingi elfu arobaini 40,000 kwa siku pamoja na nauli za kwenda kwenye mafunzo na kuturudisha makwetu.

Hadi siku ya tano ya mafunzo, hatukuwa tumelipwa chochote hali iliyokuwa ikituweka matatani hasa kwa wasichana na wanawake ambao hawakuwa na fedha za kujikimu hasa malazi.

Wengi waliomba hifadhi katika nyumba za wenyeji ambako chumba kimoja waliishi zaidi ya watu watano kwa waliopata bahati na wengine ambao hawakubahatika, itoshe kusema walikuwa na wakati mgumu.

Ilipofika siku ya tano mratibu wa elimu kwa umma wa mkoa alikuja kututisha kuwa ambaye hawezi kuvumilia afunge virago na arudi alikotoka kwani hela haijulikani itatoka lini.

Ndugu mkuu wa mkoa, hii ni lugha mbaya ya kejeli kutolewa na kijana kwenda kwa watu wazima na wenye umri wa zaidi ya baba yake. Hali hii iliamsha hasira ambapo washirki walitaka kuandamana kuja ofisini kwako, lakini mratibu huyo aliahidi kuwalipa washiriki kesho yake lakini itakuwa posho ya siku tatu.

Ndugu mkuu wa mkoa, kesho yake washiriki walilipwa shilingi 120,000 ikiwa ni posho ya siku tatu, wakiahidiwa kulipwa kiasi kilichobaki pamoja na nauli yao siku ya mwisho ya mafunzo.

Washiriki hao, ndugu RC hawajulipwa chochote. Walilazimika kutumia fedha walizopewa kulipia vyumba, chakula cha usiku na nauli! Kifupi kuna watu waliondoka bila kukipa madeni yao. Walikuwa wakipata huduma kwa ahadi ya kulipa baada ya kupata posho aao lakini ilishibdikana. Hivyo wapo walioacha mabegi yao kama dhamana.

Inafahamika kazi A CHW hazina malipo hivyo ni kitendo cha kuwadhulumu wahudumu hawa ni dhambi mbaya. Kuna waliokopa ili kupata nauli ya kuhudhuria mafunzo na pia kuna ambao wametumia hadi shilingi elfu sitini kama nauli ya kufika kwenye mafunzo, hawa na wengine mpaka sasa hawajalipwa hata shilingi.

Tumekuandikia waraka huu, tukitegemea utaingilia kati ili tulipwe stahiki zetu zilizobaki na pia angalia mwnendo wa maofisa wako wanaichonganisha serikali na wananchi kwaninhaiibgii akilini hela za wahudumu eti zimefungiwa hazina kwa kuchelewa kuzitoa ilihali waliopewa tenda ya kuleta chakula wakilipwa fedha zao zote!

Tunaomba kulipwa stahiki zetu ili tuweze kufanya kazi zetu kwani ni miezi karibu minne sasa serikali imezikalia fedha zetu kwa maelezo kuwa hazina imezinfungia!
 
Aibu kwa Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma (RMO) na Mganga mkuu wa wilaya(DMO) ya uvinza!
Hawa binadamu wengine sijui waliumbwa vipi. Juzi boss wao kawaonya tabia ya kuwafanya( waajiri) wao kuwa watumwa wao lakini hawasikii. Wanaamini kwa kushika madaraka hayo wamemaliza kila kitu.

Kwanini mpaka sasa mwezi wa nne huu hakuna taarifa yoyote kuhusu haya malipo?
 
Tena idara ya afya kwenye wilaya ndo inaongoza kuwa na budget na mafungu manono waisani wakutosha na mashirika ya kimataifa kama ICAP, MDH, Health Care, USAID, Plan international lkn zote zinaishia kwa maofisa waandamizi.
Sasa hawa watu kama wanapata fedha hizo zote na zinakuwa kwenye bajeti, vipi wanawadhulumu wahudumu hawa wanaofanya kazi kwa kujitolea? Fedha zenyewe sasa eti 40000 kwa siku kwa kichwa!
 
Back
Top Bottom