KENZY
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 32,529
- 76,691
Sikuwahi kupenda hivi kama ninavyokupenda wewe. Hisia zangu juu yako hazipimiki Kama usivyoweza kuupima ulimwengu!,umekuwa ukitikisa hisia zangu pindi nisikiapo sauti yako tamu. Hakika nimepata mpenzi nakuahidi kukutunza na kukuimbia utenzi.
Tabasamu lako hunimulika na kuuona uzuri wako!,si tu sura nzuri yenye kuvutia bali hata umbile lako zuri huutakasa moyo wangu hata kabla ya kukushika. Ngozi yako nyororo ni faraja kubwa ktk mboni zangu.
Ee malikia wangu mwenye kutikisa virija vya mishipa yangu sema nikupe nini ujionee fahari ya uhai wako? Nilipokuita uliitika,nilipokushika ulishikika. Najivunia utamu wa penzi lako murua hakika nimepata nilipopatika
Nimependa sana usumaku wako mwanamke wewe,nitakuvika taji la mapenzi ili nikuenzi kwa vitendo na kwa upendo. Kwako taabani ya moyo wangu ulietamu na furaha ya nafsi yangu.