Kwako Mwanamichezo, Gamondi na Nabi yupi zaidi?

Fene

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2021
Posts
2,824
Reaction score
4,447
Habari Wanamichezo

Wote ni mashuhuda kwa sisi Wanamichezo tumemshuhudia Nabi katika kipindi chake namna alivyokuwa anaweza kuusoma mchezo na namna anavyoweza kubadilika uwanjani kwa kufanya super sub
Huku Mayele ikiwa akiwa ndio funguo yake yake kuu katika kusaka matokeo

Tumeona Nabi aliweza ku dominate soka la nyumbani na kimataifa pia hadi kuiwezesha Yanga kufika fainali shirikisho
Sisi wengi wa kizazi hiki ndio mara ya kwanza kushuhudia tukiachana na mambo ya magazeti

Kuondoka kwake na Mayele tuliweza kutoa majibu kwa asilimia 80% Yanga inaenda kuanza tena upya kwani kama katika nyumba mfanoe Baba na mtoto mkubwa wa kiume wamesepa

Ujio wa Gamondi na sajili mpya tukaona mabadiliko makubwa kwani Yanga pia staili yake ikabadilika namna ya uchezaji na pia wingi wa magoli yaliyokuwa yanapatikana huku ukishindwa kuelewa ni yupi hasa mchezaji wa kutegemewa k
wa sasa Yanga,
Lakini pia unaweza sema Gamondi labda alikuwa anabebwa na ubora wa wachezaji lakini
yote kwa yote ubora wa Gamondi ulikuja kuonekana katika kipindi kigumu hiki kuwahi tokea katika msimu huu kwani yule ambae Wa-Afrika wote walioohofia kupangiwa nae aliambiwa utakutana nae
Hiyo haitoshi mbaya zaidi anatakiwa akam face akiwa hana wachezaji wake muhimu

Wote sisi mashahidi tactics zake alizoingia nazo tumemshuhudi Max akicheza kama wing back, tumeshuhudia jana Musonda akicheza kama kiungo na mengine mengi hadi kufikia huyu Mamelody ambae ni giant of Afrika akipita kwa masimango kwamba hakustahili
Na pengine tungekuwa Ulaya huenda Yanga ndie angekuwa club ya kwanza usiku wa jana kwenda Nusu

Let's back on our question

Kwa mtazamo wako Gamondi na Nabi yupi zaidi?
 
Kwangu mimi nadhani Nabi alikua vizuri sana kimkakati kulingana na mechi husika halafu pia uwezo wa kuusoma mchezo na kufanya maamuzi ya haraka ya Sub na kwenda ku impact that was superb. Ila kilichokua kinanitia hofu kwa Nabi ni kile kitendo cha kusubiri kipindi cha pili ndio mnakua na uhakika wa matokeo. Yan anaingia kipindi cha kwanza kama kuusoma mchezo then cha pili anakuja na majibu. Hii ukikutana na wababe wa mbinu umeisha kabisa.

Gamond mimi namsifu kwa mbinu zaidi kuanzia mwanzo wa mchezo mpaka mwisho. Ana uwezo mkubwa kuisimamia mechi na kumtawala mpinzani na hata kumuingiza kwenye mtego wake. Jana Yanga alikaa nyuma sana lakini kuanzia dkk ya 70 naona akaanza kufunguka mdogo mdogo naamini kama Gamond angekua na striker quality ya Mayele ile game tungeimaliza hapahapa Dar.

Kwakusema hivyo kwangu Gamond nampa heko kwa kuweza ku impact wachezaji kuwa na uwezo wa kufunga kila mmoja bila kutegemea striker pekee. Japo naye Gamond anahitaji ku prove walau kufikia achievements za Nabi la professer
 
Kwa mimi ni Gamondi.
Nabi alifanya vizuri akiwa na Yanga katika mashindano ya Shirikisho ila hakubahatika kukutana na kigogo yeyote yule wakuweza kum challenge kimbinu na kiufundi na alipokutana na Al Hilal tu shughuli ikaishia hapo.
Ila Gamondi kakutana na test nyingi tena timu zilizokuwa mabingwa wa nchi na timu zilizokuwa juu sana kwanzia kwenye rank, bajeti hadi ubora.
Belouizdad, Al Ahly, Mamelodi na wale Medeama japo hawana kitu kwenye rank ila ni mabingwa wa Ghana hawakuwa wanyonge.

Gamondi kaweza kupambana na hivi vigogo ipasavyo. Ila anakwamishwa na uwepo wa straika wa maana tu pale mbele. Kungekuwa na straika mzuri, Yanga alikuwa anampiga Mamelodi nje ndani bila shida. Watu wameidharau Mamelodi kwavile ime struggle dhidi ya Yanga lakini ukweli ni kwamba kocha aliwamudu kimbinu ila wale jamaa ni noma aisee wana kasi halafu wanatumia sana rula kupiga pasi.

Ukitaka kupima vizuri mzani wa Gamondi vs Nabi tazama angle hii,

Kikosi kilichocheza dhidi ya Mamelodi ni Guede na Max peke yake ambao ndio wameingia katika usajili mpya ila wengi ni wachezaji wa zamani ambao walikuwa wa daraja la kati. Wachezaji wa hadhi ya juu waliosajiliwa (Yao na Pacome) hawakutumika kabisa na haikuwa shida. Aucho ambaye ndiye injini ya Yanga pia hakucheza kabisa lakini bado Yanga waliweza kuimudu timu bora kabisa. Nabi alimkosa Aucho pekee lakini alipoteza mechi ya Dar dhidi ya USMA.

mbali ya yote jana Yanga walistahili kwenda hatua inayofuata ila ndio hivyo waamuzi hawakuamua kutenda haki kwa kukataa goli halali. Upande wangu namuona Gamondi yupo vizuri ila tu Mzize na Guede hawamtendei haki katika utumiaji wa nafasi.
 
Mkuu umenena vyema
 
Acha kumlinganisha Gamond na vitu vya hovyo

Sent from my TECNO BE6 using JamiiForums mobile app
 
Wote wapo vizuri. Kila mmoja ameweza kuitangaza Yanga vilivyo kimataifa.
 
USIMFANANISHE NABI NA WATOTO WADOGO.

ACHANA NA NABI KABISA MZEE.

Nikipata nafasi nitaelezea hoja 10 Nabi anazomzidi mbali huyo Gamondi.

Nabi is the best Coach
 
USIMFANANISHE NABI NA WATOTO WADOGO.

ACHANA NA NABI KABISA MZEE.

Nikipata nafasi nitaelezea hoja 10 Nabi anazomzidi mbali huyo Gamondi.

Nabi is the best Coach

Ungesubiri upate nafasi ndio uje utoe comment. Halafu si ulisema kufuatilia Simba na Yanga ni kupoteza muda na ukosefu wa akili, Mbona kila nyuzi upo unasoma na ku comment?
 
Enewei, tunamshukuru mama kwa kutupa ndege tukashangilie
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…