Kwako ni zipi ni mechi bora zaidi za world cup 2026

Kwako ni zipi ni mechi bora zaidi za world cup 2026

Mngoni asiyepiga gambe

Senior Member
Joined
May 4, 2017
Posts
168
Reaction score
334
Ubora wa mechi unachangiwa na vitu vingi mfano; intensity ya mechi,element of suprise,Level ya ushindani na ufundi,vibe la nje ya uwanja, mvuto wa wachezaji husika, n.k
kwa mtazamo wangu Hizi ni mechi bora zaidi world cup 2026

1. Brazil vs Morocco
surpsise kubwa ya kiwango bora cha Morocco ilileta mvuto mkubwa wa mechi na uwiano wa ushindani wa mechi pia ulikuwepo mfano mzuri wa game iliyojaa ufundi

2. Uholanzi vs Morocco
Surprise nyingine toka kwa Atlas Lions goli la dakika ya 90 la Issa Doop kuisawazishia Morocco 🔥 ( what a moment it was) bonge la game lililoenda kuwapalia uholanzi kwenye matuta

3. France vs Spain
Moja ya mechi iliyokuwa na mvuto mkubwa nje na ndani ya uwanja huku Spain walitoa burudani nzuri ya soka wakitukumbusha kizazi cha La Roja ya mwaka 2014 cha kina Xavi,Iniesta dhidi ya France iliyopewa nafasi kubwa kushinda

4. England vs Argentina
Kuna style ya soka la Argentina yaani unapigwa ile unatoa hautoi ,soka la ufundi na ubabe huku England wakionyesha kukosa mbinu za kivita na ukubwa unaohitajika kwenye level kama hizi kiwango bora zaidi cha Messi kwenye kombe la dunia hili.

5. Dr Congo vs England
Kuna mvuto fulani wa kuangalia taifa maarufu la soka duniani likicheza na timu flan ya Africa ya kati na mashariki, kiwango kizuri kwa The Leopards nilipenda sana confidence na spirit yao ni bahati mbaya kwao Harry Kane alikuwa na siku nzuri zaidi.

Overall mashindano hayakuwa na mvuto mkubwa sana huenda sababu ni hatukuona mechi nyingi za kiufundi na kutolewa mapema kwa timu nyingi za Africa , Brazili,Portugal ambazo zilikuwa na mvuto wa kipekee. Kwako ni zipi mechi bora na mambo unayoyakumbuka zaidi jwa World Cup hii ya 2026
 
Screenshot_20260720-104949_Facebook.jpg
 
Cape verde vs argentina.
Cape verde walionyesha uwezo ambao wengi hawakurajia.

Spain vs belgium
Kila upande ulipiga mpira mkubwa sana. Nafikiri ndio game pekee ambayo spain alilala na viatu.

France vs senegal
Ulipigwa mpira mkubwa sana. First half senegal alionekana kuwa timu bora zaidi uwanjani. Over confidence na ubutu kwenye umaliziaji ukawagharimu second half
 
Cape verde vs argentina.
Cape verde walionyesha uwezo ambao wengi hawakurajia.

Spain vs belgium
Kila upande ulipiga mpira mkubwa sana. Nafikiri ndio game pekee ambayo spain alilala na viatu.

France vs senegal
Ulipigwa mpira mkubwa sana. First half senegal alionekana kuwa timu bora zaidi uwanjani. Over confidence na ubutu kwenye umaliziaji ukawagharimu second half
Spain na Belgium 🔥🔥,usingefikiria kuwa Spain angekuwa bingwa jinsi alivyotaabika kwa Belgium ambayo haikuwa tishio kivile
 
Back
Top Bottom