Natumai mu wazima wa Afya Huku tukizidi kupiga hatua mbele katika Bwana
Mimi ni Msikilizaji mzuri sana wa Mahubiri TV, Na sio Msabato pia siwezi kuwa Msabato Ila neno la Mungu halina dini, Nitakufa na Kuzikwa KKKT.
Hapa majuzi mchungaji Mmbaga umefundisha somo zuri sana (Maombi ya Yehoshafati) Nikiri wazi nimejifunza sana na sana pia nikaunganisha mafundisho yako ya Obedi-Edom jinsi ambavyo Mungu aliibariki nyumba yake baada ya Sanduku la Bwana kuwa katika nyumba yake baada ya Daudi kulikataa wakati linatoka (Haya mafundisho nimeyaelewa sana)
sasa niliamua kutendea kazi haya mafundisho mawili ila nikijikita sana Mungu aibariki nyumba yangu na kuitazama kama alivyoitazama nyumba ya Obedi-Edom. baada ya siku 4/5 ya maombi hayo mawazo kama sauti yakanijia kichwani "Je nyumba yako ina kipi niibariki kama Obedi-edom" (ila kimawazo hili swali nililielwa sana kwamba je kuna kitu gani kwangu hadi Mungu aniangalie kama alivyofanya kwa Obedi Edom)
Baada ya mawazo haya kama sauti kwakweli nilikua kama nimemwagiwa maji nikaacha kusali nikaenda kulala tu nikiwaza sana kwamba nifanye kipi ambacho Mungu atakiangalia.
Sasa Mchungaji naomba fundisha je tufanye kipi au ni kitu kipi katika dunia ya sasa ambayo ukifanya kama baba wa familia(ni baba wa familia mimi) Mungu atatitazama Nyumba yangu kama Obedi Edomu
ASANTE