Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Kwako Dada yangu na rafiki yangu humu JF especialy jukwaa letu pendwa la MMU.
Nimeamua kukuandikia huu ujumbe jukwaani badala ya kukutumia PM..
Rafiki yangu nilichokigundua ni kwamba unataka kupendwa, ndiyo maana moyo wako ni rahisi kupenda. Watu wengi huwa wanalipenda tu wazo la kupenda na hawafikirii nini kiendelee zaidi wakishapenda, ndiyo maana muda ukipita hilo wazo wanalichoka kukuhusu wewe waliyedhani walikupenda. Wewe unataka kutulia, ila watu unaowapata wanafikiri unataka kucheza, kwa sababu huwaonyeshi mapema kwamba unategemea watulie nawe, kwa hiyo baadaye ukija kuwaonyesha unataka kutulia nao... wao wanakuwa wanazingua. Hilo si tatizo lako kwa sababu ni wenyewe ndiyo wanakuwa wanashindwa kuona jinsi mambo yalivyo kihalisi. Kwa kifupi ni kuwa wao wanataka mambo yaende kwa haraka na wewe huwa unapenda mambo yaende taratibu huku moyo wako ukitaka ujiridhishe na uweze kupenda kabisa.
Pole sana Dada yangu na rafiki yangu, nina mengi ya kuandika lakini muda sio rafiki na mambo mengine yananizonga. Ukiusoma huu ujumbe naomba uni PM