Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Failed president for five years...... Destroyed our nation values and our economy and our unit..........
Too partisan and tribalism...
 
Hakuna mtanzania yeyote timamu anayetaka lockdown, Watanzania wanataka uwajibikike kama Rais wao, Watanzania wanataka uwazi wa wagonjwa wangapi wanakufa na wangapi wanaumwa? Watanzania wanataka kujua pesa za misaada ziko wapi? Watanzania wanataka kujua vifaa vilivyonunuliwa viko wapi?

Watanzani labda ungewaambia kwanini umejificha? Watanzania wanataka kujua kwa nini madoctor wanakimbia wagonjwa ? Watanzania wana haki ya kujua yote hayo?

Kama tatizo hakuna tanganza kuanzia leo kazi zote ziendelee kama kawaida.

Fungua shule, Rudi Ikulu uchape kazi au jiuzulu watu wanakufa wanateseka hospitali bila huduma zozote wewe umejificha haileti picha nzuri.

Magufuli unatushangaza sana sisi ndugu zako nakuomba achia Ikulu kama hauwezi kusimama na watanzania kwenye majanga ya Kitaifa.
Binafsi nashangaa sana kuwa mpaka Leo yupo madarakani wakati ofisi kaikimbia. Halafu tunadanganyana eti ofisi ya Rais ni popote!

Hata katika hali ya kawaida sikupata kusikia Nyerere akikaa Butiama wiki mbili mfululizo ije kwenye majanga kama haya? Yaani wakati wakati wa vita vya Amin angejificha Butiama siku 27 tungemuelewa? JK au Mkapa hawakuwa na kwao? Aibu sana.
Atuachie tuu ofisi yetu yeye aendelee kukaa zake huko apendavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madaraka ni kama pumzi.
Na pumzi hua hairudishwi kwa hiari mpaka unyang'anywe!
 
Huyu Rais linapokuja suala la majanga anakuwa wa hovyo kwelikweli. Sijui huo upendo anaohubiri ni upi zaidi ya kupambana na majanga kwa watu wake. Ila sishangai maana kwenye utawala wake yamefanyika mambo mengi sana ya kikatili dhidi ya binadamu.

Rais anapokea fedha za kuyakabili majanga yeye anaenda kuzihifadhi BoT ili zi boost uchumi! Sijawahi kuona aisee!
Tunamuonea bure Rais wetu!
Alishawaambia wale akina IWE, kuwa wasimlilie yeye kwani sio yeye aliyewaletea TETEMEKO!
Tena kwa kejeli kubwa, akawauliza, wakati wa kuomba kura, aliwaambia kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atawaletea tetemeko?
Sina shaka, hata janga hili, msimamo wake ni kuwa, SIO YEYE ALIYEILETA CORONA!
 
Mkuu suala si kuwa wamekufa wangapi. Suala ni uhusiano wa wanaoambukizwa kulinganisha na wanaopona kwa siku au kwa kipindi fulani.

Hapo itakupa hali ya ugonjwa bila kujali wanaokufa ni wengi au kidogo.

USA, Spain, Germany, Italy, China na kote waliko udhibiti maambukizi ni kidogo kuliko wanaopona.

Uganda, Rwanda na Kenya ni hivyo pia.

Mkuu namba ya wanaokufa haina maana yoyote (irrelevant).

Ila kumbuka mgonjwa hadi kufa au kupona ataambukiza wengine kama 90 kwa hali yetu iliyopo hivi sasa.

Ndani ya wiki 2 - 3 mgonjwa atapona au atakufa kutegemeana na huduma za afya zilivyo alipo au katika nchi.

Pia 5% - 10% ya walioambukizwa watakufa kwa ugonjwa huu.

Kasi ya maambukizi itafanya namba ya wafu kuwa kubwa mno katika kipindi kifupi kama maambukizi hayadhibitiwi.
Watanzania wanataka kufahamu tuna vipimio(equipment) vingapi (idadi) vya Corona na viko wapi, Dar es Salaam pekee au na mikoa gani? Na kama kuna mipango gani ya karibuni ya kupata vipimio na kwa idadi gani.

Ni vizuri Watanzania kujua watu wangapi wanapimwa kila siku(saa 24) kama nchi nyingine zifanyavyo. Hii ni kwa sababu huwa inachukua siku nyingi mpaka Watanzania kupata takwimu nyingine za wagonjwa tofauti na nchi nyingine, mfano Kenya au Uganda. Ni vizuri kusema idadi ya waliopimwa hata kama matokeo yatakuwa ni sifuri. Mfano, wamepimwa 500, hakuna mgonjwa aliyepatikana.

Ni vizuri Watanzania kuona wageni wanaoingia nchi wanapimwa Corona na si joto. Tumeshuhudia wenzetu Uganda wamewagundua madereva wa Kitanzania zaidi ya 6 kuwa na ugonjwa wa Covid-19 baada ya kuwapima mpakani. Ni dhahiri hao madereva walitoka Dar es Salaam, Je watakuwa wamewaambukiza watu wangapi mpaka kufika Mutukura? ukizingatia fujo za madereva katika vituo mbalimbali wawapo safarini?

Ni vizuri pia Watanzania kuona vifo vyote kwa sasa vinachunguzwa vyanzo vyake ili kuondoa maambukizi wakati wa kushughulika na marehemu mpaka maziko. Tunafahamu kuwa Serikali hushughulika kuwazika marehemu waliofariki kwa Corona na kudhibiti idadi ya washiriki wakati wa maziko. Je ni kwa vipi inahakikisha kuwa watu wanaofariki wakiwa majumbani wanafanyiwa vipimo ili kuondoa maambukizi zaidi wakati wa maziko?
 
Wenye akili tulishagundua musee yuko karantini kijijini... maana awali amekutana na wageni wengi toka nchi zilizoathirika, alafu anapresha tokana na mauoga yake yakawaida na inasemekana wasee wenyepresha wakipigwa korona kupona nishida naona museeiya akaona acharu mpaka kijijini kujikarantini.

Tungetangaziwa mitandao ingechafuka na wapinzani wangeitumia hata kwenye kampeni ndomana akaona anyuti tuu kistaili. Sahivi ata-church haendi.
 
Ninaposoma bandiko kama hili najisikia vibaya sana. Jirani yangu nyumba inayofuata kutoka kwangu wote wapo Carantini wakati Baba yao ambae ni Daktari wa Hospitali ya Rufaa hapa Moro anapumua kwa msaada wa Oxygen. Hali ishakuwa tete, Jamani tuchue tahadhali juu ya hili janga la Dunia.
 
Utazifungia Dar na Zanzibar kwa muda gani?.

Nani anajua ni lini hii corona itakuwa imeweza kudhibitiwa?

Marekani wamekufa zaidi ya watu 55000 lakini baadhi ya majimbo yanafunguliwa.

Lockdown inakuwa na maana ukishafahamu ni lini huu ugonjwa utakuwa umeshaweza kudhibitiwa.
 
Huyo kijana mpuuzi sana. Alileta Uzi humu akiomba ugonjwa ufike Tanzania.
Kwa hiyo unaamini kabisa maombi yake ndio yameleta Corona Tanzania!
Hii ni unscientific! Hakuna mahusiano yoyote kisayansi ya mtu kuomba au kuanzisha thread humu na kuingia kwa pandemic ndani ya nchi.
 
Binafsi nashangaa sana kuwa mpaka Leo yupo madarakani wakati ofisi kaikimbia. Halafu tunadanganyana eti ofisi ya Rais ni popote!

Hata katika hali ya kawaida sikupata kusikia Nyerere akikaa Butiama wiki mbili mfululizo ije kwenye majanga kama haya? Yaani wakati wakati wa vita vya Amin angejificha Butiama siku 27 tungemuelewa? JK au Mkapa hawakuwa na kwao? Aibu sana.
Atuachie tuu ofisi yetu yeye aendelee kukaa zake huko apendavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu Chakaza, ina maana Chato sio Tanzania ni Burundi?.

Kwa hiyo rais ili aingoze nchi ni lazima awe Dar?..JK alikuwa safarini muda mwingi lakini hakuna aliyehoji nani anaongoza nchi.

Mkapa aliugua akakaa nje miezi kadhaa na hakuna aliyehoji nchi kama ina rais au haina.

Tuachane na hizi nongwa zisizo na msingi.
 
Mkuu hapangiwi

Ulisema kweli. Kakomaa kama luba. Hadi kifo.

Hata sasa waliopo wangeanza na hili kwanza labda hata kabla ya kuapishwa. Kama dharura sana:

Barakoa na social distancing.
 
Back
Top Bottom