Kwako Rais Magufuli sasa pasipo na kupepesa maneno: Kwa unavyoshughulika na Corona sasa - NO!

Failed president for five years...... Destroyed our nation values and our economy and our unit..........
Too partisan and tribalism...
 
Binafsi nashangaa sana kuwa mpaka Leo yupo madarakani wakati ofisi kaikimbia. Halafu tunadanganyana eti ofisi ya Rais ni popote!

Hata katika hali ya kawaida sikupata kusikia Nyerere akikaa Butiama wiki mbili mfululizo ije kwenye majanga kama haya? Yaani wakati wakati wa vita vya Amin angejificha Butiama siku 27 tungemuelewa? JK au Mkapa hawakuwa na kwao? Aibu sana.
Atuachie tuu ofisi yetu yeye aendelee kukaa zake huko apendavyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madaraka ni kama pumzi.
Na pumzi hua hairudishwi kwa hiari mpaka unyang'anywe!
 
Tunamuonea bure Rais wetu!
Alishawaambia wale akina IWE, kuwa wasimlilie yeye kwani sio yeye aliyewaletea TETEMEKO!
Tena kwa kejeli kubwa, akawauliza, wakati wa kuomba kura, aliwaambia kuwa akichaguliwa kuwa Rais wa Tanzania, atawaletea tetemeko?
Sina shaka, hata janga hili, msimamo wake ni kuwa, SIO YEYE ALIYEILETA CORONA!
 
Watanzania wanataka kufahamu tuna vipimio(equipment) vingapi (idadi) vya Corona na viko wapi, Dar es Salaam pekee au na mikoa gani? Na kama kuna mipango gani ya karibuni ya kupata vipimio na kwa idadi gani.

Ni vizuri Watanzania kujua watu wangapi wanapimwa kila siku(saa 24) kama nchi nyingine zifanyavyo. Hii ni kwa sababu huwa inachukua siku nyingi mpaka Watanzania kupata takwimu nyingine za wagonjwa tofauti na nchi nyingine, mfano Kenya au Uganda. Ni vizuri kusema idadi ya waliopimwa hata kama matokeo yatakuwa ni sifuri. Mfano, wamepimwa 500, hakuna mgonjwa aliyepatikana.

Ni vizuri Watanzania kuona wageni wanaoingia nchi wanapimwa Corona na si joto. Tumeshuhudia wenzetu Uganda wamewagundua madereva wa Kitanzania zaidi ya 6 kuwa na ugonjwa wa Covid-19 baada ya kuwapima mpakani. Ni dhahiri hao madereva walitoka Dar es Salaam, Je watakuwa wamewaambukiza watu wangapi mpaka kufika Mutukura? ukizingatia fujo za madereva katika vituo mbalimbali wawapo safarini?

Ni vizuri pia Watanzania kuona vifo vyote kwa sasa vinachunguzwa vyanzo vyake ili kuondoa maambukizi wakati wa kushughulika na marehemu mpaka maziko. Tunafahamu kuwa Serikali hushughulika kuwazika marehemu waliofariki kwa Corona na kudhibiti idadi ya washiriki wakati wa maziko. Je ni kwa vipi inahakikisha kuwa watu wanaofariki wakiwa majumbani wanafanyiwa vipimo ili kuondoa maambukizi zaidi wakati wa maziko?
 
Wenye akili tulishagundua musee yuko karantini kijijini... maana awali amekutana na wageni wengi toka nchi zilizoathirika, alafu anapresha tokana na mauoga yake yakawaida na inasemekana wasee wenyepresha wakipigwa korona kupona nishida naona museeiya akaona acharu mpaka kijijini kujikarantini.

Tungetangaziwa mitandao ingechafuka na wapinzani wangeitumia hata kwenye kampeni ndomana akaona anyuti tuu kistaili. Sahivi ata-church haendi.
 
Ninaposoma bandiko kama hili najisikia vibaya sana. Jirani yangu nyumba inayofuata kutoka kwangu wote wapo Carantini wakati Baba yao ambae ni Daktari wa Hospitali ya Rufaa hapa Moro anapumua kwa msaada wa Oxygen. Hali ishakuwa tete, Jamani tuchue tahadhali juu ya hili janga la Dunia.
 
Utazifungia Dar na Zanzibar kwa muda gani?.

Nani anajua ni lini hii corona itakuwa imeweza kudhibitiwa?

Marekani wamekufa zaidi ya watu 55000 lakini baadhi ya majimbo yanafunguliwa.

Lockdown inakuwa na maana ukishafahamu ni lini huu ugonjwa utakuwa umeshaweza kudhibitiwa.
 
Huyo kijana mpuuzi sana. Alileta Uzi humu akiomba ugonjwa ufike Tanzania.
Kwa hiyo unaamini kabisa maombi yake ndio yameleta Corona Tanzania!
Hii ni unscientific! Hakuna mahusiano yoyote kisayansi ya mtu kuomba au kuanzisha thread humu na kuingia kwa pandemic ndani ya nchi.
 
Mkuu Chakaza, ina maana Chato sio Tanzania ni Burundi?.

Kwa hiyo rais ili aingoze nchi ni lazima awe Dar?..JK alikuwa safarini muda mwingi lakini hakuna aliyehoji nani anaongoza nchi.

Mkapa aliugua akakaa nje miezi kadhaa na hakuna aliyehoji nchi kama ina rais au haina.

Tuachane na hizi nongwa zisizo na msingi.
 
Mkuu hapangiwi

Ulisema kweli. Kakomaa kama luba. Hadi kifo.

Hata sasa waliopo wangeanza na hili kwanza labda hata kabla ya kuapishwa. Kama dharura sana:

Barakoa na social distancing.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…