clinton gidioni
Senior Member
- Oct 24, 2016
- 145
- 165
Kiukweli, unatupambania sana vijana na hakika unatutakia mema. Kijana yeyote anayejitahidi kupambana lazima ataona juhudi zako.
Mheshimiwa, nimejitahidi kadri ya uwezo wangu, lakini nimeshindwa kufanikisha mambo kupitia fani na taaluma nilizonazo. Kwa sasa, nimeamua kuanza upya maisha yangu na kuingia kwenye kilimo chenye tija. Uamuzi huu nimeufanya binafsi, bila kushauriwa na mtu yeyote.
Hata hivyo, sina chochote kama kianzio – sina ardhi wala mbegu. Mtaji pekee nilionao ni afya, akili, na nguvu za kufanya kazi. Hitaji langu kubwa ni kupata ardhi ya kulima, na endapo nitapata kupitia BBT (Building a Better Tomorrow), itakuwa vyema zaidi.
Nimepita kwenye baadhi ya mashamba ya BBT na kuona juhudi zako, Mheshimiwa. Nipo tayari kuanza kazi hata leo. Sitaki kupoteza muda zaidi. Naomba msaada wako, Mheshimiwa Hussein Bashe.