Wananchi kama wananchi wa maeneo hayo hawajawahi kusema kuwa wanashida na mkoa mpya katika maeneo hayo, ni kiherehere cha mtu mmoja tu,aliyekuwa anataka kila kitu akipeleke nyumbani kwake ndiye aliyekuwa na shida na mkoa mpya akauweke nyumbani kwake.
Kwakuwa hata watu wanamna hiyo hawakosagi wafuasi japokuwa hawawezi wakaweka wazi nia zao kuwa wanaunga mkono mkoa kupelekwa Chato nyumbani kwa mwendazake,wanajificha kwenye kivuri cha kuwasogezea wananchi huduma karibu, ndiomaana wengine tunasema kuwa kama nikuwasogezea wananchi huduma, Chato siyo mahali sahihi pakuweka makao makuu ya mkoa kutakuwa ni kuwatesa wananchi zaidi badala ya kuwasaidia niheri wabaki kama hapo mwanzo.
Halafu mkoa kuitwa Chato,kuitwa Bmlo, kuitwa Muleba, kuitwa Ngara, kuitwa Runazi, Buziku siyo tatizo, tatizo ni mahali gani sahihi ambapo makao makuu ya mkoa yawekwe mahali ambapo itakuwa ni kusogeza huduma kwa wananchi na si kwa ajili ya kudumisha fikra za mtu mmoja za kupendelea nyumbani kwake.
Hata hivyo sidhani kama ni wakati mwafaka wa kuwepo mkoa mwingine wakati hata mkoa wenyewe wa Geita bado haujaendelezwa kutokana na uchanga wake.