Kwamtogole on Tuwsday

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
Huyu bi shost alitaka kumdhibiti mume basi kama ilivyoada aliwlekezwa kwa sangoma, ni Nyamwicho huyo alimwambia anataka kucha za mikono na za miguu za mumewe ili kazi ifanyike.

Bi shost kila akipiga hesabu za kukusanya kucha ni ngumu , mwisho alitafuta box tupu la kiberiti, alimtaimu mume amelala akaanza kukata kucha. Jamaa amestuka usingizini anamuona mke anamkata kucha, alifanya jicho moja na kujifanya anakoroma mke akakusanya kucha na kuziweka kwenye kiberiti. Akaenda mkono wa pili, na miguu wa kwanza, mume anaangalia.

Alipomaliza akahifadhi kibiriti kwenye draw chumbani na kwenda chooni kujisaidia kabla ya kulala . Mume aliamka akafungua draw na kuhamisha kibiriti kwenye briefcase yake. Dada anashindwa kuuliza mzigo wake uliokuwa kwenye draw umekwendavwapi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…