kwan udom kuna tatizo gani?{waliosoma huko tafadhali mnijuze}

kwan udom kuna tatizo gani?{waliosoma huko tafadhali mnijuze}

ntita

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2013
Posts
513
Reaction score
285
mi ni kijana wa kidato cha 6, nmekuwa na hamu sana ya kujiunga na chuo kikuu cha dodoma, lakini kila nnaemwambia hilo hunibeza na kusema eti udom si chuo cha kwenda.

Ninachotaka kufahamu ni ubovu na ubora wa chuo hicho hasa kutoka kwa wale mliosoma hapo ili niweze kufanya uamuzi sahihi muda utakapofika.

Natanguliza shukurani.
 
Aliyesoma UDOM hawezi kukupa ukweli maana ukweli wake utakuwa unaonyesha jinsi alivyovurugwa na kupata digrii isiyo digrii. Swali lako ni vema ulielekeze kwa waajiri walio waajiri wanafunzi waliomaliza chuo hicho fake.

Kuna simu au television za SAMSUNG na kuna simu au television za SAMSANG. Ni ushauri tu, kabla hujanunua soma vizuri majina hayo. Kujenga jina na jina liuze bidhaa yako ni kazi! SAMSANG (UDOM) huwezi kulinganisha na SAMSUNG (UDSM, SUA, MZUMBE UNV. nk). Tafakari!
 
tufahamishane ndugu.

nnachojua mimi hakuna taasisi isiyokuwa na mapungufu.
nmesoma hapo na nmeajiriwa,wengi wanaoiponda udom hawaijui. nliwah kutembelewa na rafik zangu toka mzumbe walikaa udom zaid ya miez 3 walikuwa field,waliponda sana kwamba udom ni majengo lkn kadri muda ulivyozid kwenda walianza kutoa udhaifu wa huko walikotoka.
endelea kuchunguza zaidi ili ufanye maamuz sahihi.
kila la kheri
 
Hili nalo neno.
 
Ondoa Mzumbe hapo huwezi ukailingalisha na Ud na Sua. Mzumbe wanafunzi hawadiscontinue.
 
Mti hujulikana kwa matunda (kuni, mbao, kivuli, matunda, nk) yake. Taasisi za elimu, pamoja na mapungufu ambayo taasisi husika inaweza kuwa nayo; muhimu tunaangalia ubora wa wahitimu. Nina mfano hai, mwalimu mmoja aliajiriwa UDOM afundishe Botany toka SUA. Mwalimu huyo alitumia notes za botany za SUA kufundishia wanafunzi wa UDOM, wanafunzi waligoma wakidai wanafundishwa mambo ya Masters/PhD! Na watawala wa UDOM walimsihi mwalimu huyo aandae notes zingine kama wanafunzi wanavyotaka. Na ndivyo ilivyokuwa. Unategemea nini hapo? Ndio maana mimi naamini kuwa waajiri wanaweza kutoa jibu kwa mtoa mada na si wanafunzi waliosoma UDOM.
 
udom wala hakuna tatizo kijana wewe kama unapenda kusoma pale nenda mimi nimesoma udom ninaajira na kila kitu kiko sawa, pia mapungufu CIO udom tu hata huko sua, mzumbe yapo omba udom upate elimu kijana.
 
Ondoa Mzumbe hapo huwezi ukailingalisha na Ud na Sua. Mzumbe wanafunzi hawadiscontinue.

Naam! Nakubaliana kabisa nawe. Ndio maana nilianza kuandika UD nikaja SUA na kisha Mzumbe. Hapa nilikuwa namaanisha huwezi kuilinganisha UDOM na Mzumbe. Mzumbe katika soko imeanza kujenga jina na UDOM bado sana.
 
udom wala hakuna tatizo kijana wewe kama unapenda kusoma pale nenda mimi nimesoma udom ninaajira na kila kitu kiko sawa, pia mapungufu CIO udom tu hata huko sua, mzumbe yapo omba udom upate elimu kijana.

Wakati UKIMWI unaingia nchini, tulishuhudia walioupata wakiwaambukiza wengine, kisa? Waathirika wasife peke yao bali wafe wengi! Siwezi kutofautisha maneno yako na waathirika wa UKIMWI wa wakati huo. Hata hivyo nawashukuru sana waathirika wa wakati huo maana walisaidia nchi kutafuta mikakati ya kuokoa watu na ninadhani hata mpango wa kutoa ARVs kwa waathirika ni zao lake! Nawe kazana tu kushawishi kuwa UDOM ni nzuri ili kuzalishwe watu wa aina yako wengi hata ifike wakati wa serikali kuona makosa yake. Nafikiri itachukua hatua sitahiki kuokoa taifa.
 
Ondoa Mzumbe hapo huwezi ukailingalisha na Ud na Sua. Mzumbe wanafunzi hawadiscontinue.

Kwanini unaudanganya umma?? Hata news zinazozizima taifa (mf. Mwanafunzi wa Mzumbe ajiua baada ya kudisco, mzumbe unadisco kwa semester 1 tu n.k) huzijui.😕😕😕
Pole sana kilaza
 
Kaka kasome udom achana na mbwembwe za watu ni chuo kizuri sana. Tatizo ni maji ya chunvi kama huja yazoea. Labda kama nawewe upo kwenye kundi la wanao kibeza indirect
 
Wanaofundisha UDOM wengi ni Wahindi kati ya hao wengi wao ni maProf na wachache wana PHD na hichi ndo chuo chenye wageni wengi,Wanafunzi wa nchi za nje wanatoka Rwanda,Mozambique,burundi,kenya,Congo,nk ila kwa upande wa wahadhiri wa kitanzania wengi wamepata degree zao SUA,MZUMBE,UDSM, kwa upande wa course kuna baadhi ya course zipo UDOM tu Mf BA korea,Japanise,IR illa kwa upande wa Elimu sio ngumu kwa kua Mfumo wa kukamiana kati ya wahadhiri na wanafunzi kama chuo vingine haujapewa kipaumbele kwa kuwa wengi wa wahadhiri wanafundisha kwa mikataba hasa Wahindi ila nihitimishe kwa kusema hivi kwa research niliofanya kwa vyuo Vikuu hapa Tz ubora wa Mwanafunzi unatokana na Effort zake mwenyewe kwa kuwa technologia imeweka mambo mengi wazi hasa upatikanaji wa material kwa hio kama ukitaka kuwa competence unaweza ukawa kwa juhuzi zako kama ukitaka kuwa M .s .e.n.g.e. Unaweza kuwa ,according to Laswell Development is Human effort,
 
Wakati UKIMWI unaingia nchini, tulishuhudia walioupata wakiwaambukiza wengine, kisa? Waathirika wasife peke yao bali wafe wengi! Siwezi kutofautisha maneno yako na waathirika wa UKIMWI wa wakati huo. Hata hivyo nawashukuru sana waathirika wa wakati huo maana walisaidia nchi kutafuta mikakati ya kuokoa watu na ninadhani hata mpango wa kutoa ARVs kwa waathirika ni zao lake! Nawe kazana tu kushawishi kuwa UDOM ni nzuri ili kuzalishwe watu wa aina yako wengi hata ifike wakati wa serikali kuona makosa yake. Nafikiri itachukua hatua sitahiki kuokoa taifa.
Tatizo Watanzania wengi wanapoona wenzao wanaendelea hujaa WIVU zisizo na sababu kwa kuanza kuponda maendeleo hayo in NEGATIVITY FORM.ONGEZA JUHUDI
 
mi ni kijana wa kidato cha 6, nmekuwa na hamu sana ya kujiunga na chuo kikuu cha dodoma, lakini kila nnaemwambia hilo hunibeza na kusema eti udom si chuo cha kwenda.

Ninachotaka kufahamu ni ubovu na ubora wa chuo hicho hasa kutoka kwa wale mliosoma hapo ili niweze kufanya uamuzi sahihi muda utakapofika.

Natanguliza shukurani.

Yaani wewe Dogo umeanza kukata mbeleko kabla mtoto hajazaliwa, piga shule kwanza, rekebisha combination kulingana na ambition yako. Ukishafaulu vizuri mambo ya Chuo cha kwenda huja yenyewe, watu hawachagui chuo wakiwa shuleni bali huchagua masomo ya kusoma watakapokuwa chuoni, sasa wewe unafanya kinyume chake !!!!
 
Tatizo Watanzania wengi wanapoona wenzao wanaendelea hujaa WIVU zisizo na sababu kwa kuanza kuponda maendeleo hayo in NEGATIVITY FORM.ONGEZA JUHUDI

Tafsiri ya neno au maneno siku zote huwa na msemaji. Vyuo vya Tanzania ni vya watanzania, humo husoma watu wetu ambao ni mstakabari wa maendeleo ya nchi yetu. Ni vema tukiwa wakweli hata kama ukweli unauma. Mfano ni ujinga kuogopa kusema ukweli huu "watanzania tulio wengi tu masikini na wengi tunaishi chini ya dola moja kwa siku", kisa? Eti tunajidhalilisha? Lakini huo si ndio ukweli? Tusemeje sasa? Watanzania ni matajiri na hatuishi chini ya dola moja kwa siku. Tunamdanganya nani na kwa faida ya nani? Kulinganisha UDOM na UD kitaaluma ni sawa na kulinganisha ccm na act (chama cha akina mwigamba) kwa wingi wa wanachama! Jamani, UDOM badooooooo!
 
Ni mjadala mzuri na unafikirisha, mi nipo Udom na haya yanayosemwa si kihivyo na ubora wa mhitimu ni yeye mwenyewe, Udom ina product kibao tu na wanafanya vyema ktk nyanja tofauti tofauti,tuwape muda na mtakuja kujua ukiritimba mnao uonesha ni mawazo mfu! Hebu jadilini geology ya Udsm na Udom, washikaji wako vyema sana tu.
 
Ni kweli. Huwezi kumlinganisha kingunge na Zitto, Udom bado kwa kuwa hata miaka Kumi hakina ila kwa nini watu wanakuwa na hofu juu ya ujio wa UDOM? Ila kuimalika kwa udom hutegemea sana UDSM kwa kuwa kila kilichopo UDOM ni kopy na pest ya UDSM kama Udom kuna udhaifu basi huo ni udhaifu wa udsm umebebwa na udom hata ivyo Udsm ina heshima kwa kuwa ya Umri ndo maana hata baba akiwa mjinga,mlevi ni baba kwa kuwa ndio alikuleta duniani ila kwa ujumla elimu ya Tz bado sana sana
 
Nakushaur kasome vyuo ambavyo watu hawavisemi vibaya,kwanini uendelee kukomaa na chuo kinacho zungumzwa vibaya na kila mtu!
Udom wataenda wanaotaka kwenda huko...
 
Back
Top Bottom