Kwangu ukimtoa Joseph Haule (Prof Jay), msanii wangu bora wa Hip Hop ni Nikki Mbishi. Nenda YouTube kaangalie kazi yake mpya inaitwa Romanza

mimi nimependa wimbo wa "Akili kumkichwa na Kopareti" kwenye hii album yake mpya.
 
Sina unyonge sidelay kama Echo,
Konde gang hatetewi Baba Levo...
 
Ana uwezo mzuri wa kurap na flow nzuri Ila ukiachana na nyimbo chache Alizoimba Kama Katiba Mpya na I'm sorry Jk na smatta bado uwezo wake wakuandika upo chini .

Prof jay anachowazidi hawa Marapa ni kucheza na Mada Fulani hadi ikaeleweka anachoimba.

Uwezo aliwahi kuwa nao Johmakin katika nyimbo ya " I see me" alipokuwa ana meditate kuhusu future yake.

So ninachokiona kwa Nikki ajaribu kuimba mambo yanayo make sense zaidi kama alivyowahi kuimba nyimbo iliyomtambulisha Play Boy
 
Mkuu nimekuelewa hoja zako lakini sisi wa bongo ni kama tumekalili kuhusu mtu kuimba vitu vinavyo sense [ vitu vya jamii ]Hiyo kwangu ni BiG No.....

Wasani wa hip hop wote wa ulaya na American wanaimba kama nikki mbishi tu coz wanakuwa na mawanda mapana ya kufikiri
 
Tafuta ngoma moja ya nikki mbishi inaitwa kusingekuwa na mziki moja ya mistari wa wimbo huo unaanza hivi

kusingekuwa na mziki Tusingemjua nikki wala mwana FA asingetuuliza ingekuwa vipi mwasiti asingevua pendo diamond ingemuua dhiki
 
Kwako sawa ila kiuhalisia hata top 5 haingii..
Ijulikane pia mi ni shabiki wa Nikki Mbishi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…