Nilijaribu kuangalia mechi mbili za kimataifa za kirafiki kati ya timu yetu ya taifa (Taifa stars) .. Dhidi ya Algeria na dhidi ya DRC..Mechi hizi mbili nimezifurahia sana kwa kuwa TFF walijitahidi kutafuta timu ambazo zimetuacha mbali sana katika viwango wa FIFA..
Mechi dhidi ya Algeria..Mwalimu alikwenda na game plan nzuri sana..tulicheza kwa kuzuia Zaidi na kufanya mashambulizi ya kushtukiza..Nakumbuka Himidi Mao na Mudadhir Yahya walicheza kama viungo wawili wakabaji huku mbele yao kakicheza Said Ndemla..Msuva na Samatta walikuwa mbele Zaidi huku Kichuya akicheza winga ya kushoto ambapo alionekana kucheza Zaidi nyuma ambapo aliweza kumsaidi vizuri kukaba Gadiel Michael.. Mwalimu alifikiri riyard mahrez angecheza winga ya kulia..
Wa Algeria walitushambulia kwa speed sana huku wakitumia ma winga wao walio kuwa na speed kali sana..Nakumbuka 1st half Kapombe alipa tabu sana.. Saidi Ndemla hakuoneka sana ..Alikuwa chini ya ulinzi wa Nabil Bentaleb
Katika mechi ile Tanzania ilicheza vizuri sana..Nimpongeze mwalimu kwa kuenda na mbinu nzuri..Japo tulifungwa 4-1 lakini tulionesha mabadiliko..kumbuka mara ya mwisho Tanzania kwenda Algeria tulifungwa magoli 7..
Mechi dhidi ya DRC ..Hii ilikuwa mechi nyingine ambayo Tanzania tulicheza vizuri sana.Mwalimu alifanya mabadiliko machache katika kikosi kilichoanza kule Algeria..mudadhir Yahya na Ndemla hawakuanza..Pia golikipa Manula alirudi baada ya kuukosa mchezo dhidi ya Algeria..
Tofauti ya DRC na Algeria ni aina ya mpira wanaocheza..Algeria wanacheza kwa speed kali sana ..Wanashambulia na kukukaba kwa speed kali..Lakini congo hawana speed kali kama ya Algeria lakini wana watu wenye nguvu sana..Jaribu kuwaangalia Yannick Bolasie na Assambolang..
Kwa kuwa hawakuwa na speed kali hii ilitupa sisi Tanzania mwanya wa kuwa kwa free kuchezea mpira na kuweza kuwashambulia..Pia ilitupa nafasi ya kuweza kujipanga vizuri wakati congo wanapotushambulia..
Kiujumla katika mechi hizi mbili tulijitahidi sana tanzania..Pongezi kwa benchi la ufundi na wachezaji kwa ujumla..Pia wachezaji wetu wa ndani walijitahidi kucheza vizuri sana
Lengo kuu la kuandia post hii ni kuangalia jinsi Pro footballers wetu walivyo tusaidia..
Katika mechi zote mbili wapinzani wetu walijaribu ku deal sana na Samatta..Mabeki wa kati wa Algeria walimsumbua sana Samatta..Kuna wakati Samatta ilimbidi kuhama nafasi..Hata dhiya ya Congo..Lakini unaweza kuona pamoja na kukabwa sana Samatta aliweza kufunga goli dhidi ya Congo
Kwa upande wa Msuva yeye aliweza kupata advantage baada ya wapinzani kudeal sana na Samatta..Msuva amebadilika sana..Mechi dhidi ya Algeria alionekana kuwa na kasi sana na maamuzi ya haraka mno
Pia Abdi Banda siwezi kumsahau..alituonye kuwa hachezi Tanzania..Abdi alikuwa imara mno..Yuko fiti juu pia hata kwenye marking unaweza kuona alivyokuwa imara todfauti na alipokuwa simba
Hapa ndipo ninapo patwa na maswali mengi juu ya watu wenye mamlaka ya kuwapeleka wachezaji wetu wa ndani kwenye trial nchi za wenzetu zilizo tuzidi kisoka..je watu hawa hawaoni Samatta,Msuva na Abdi Banda walivyocheza dhidi ya Algeria na Congo??????
Matunda ya wachezaji hawa kucheza nje yanaonekana kila kukicha..Lakini tuna wachezaji wa chache sana wanaocheza katika ligi kubwa za nje ya nchi..kuweza kuwapata Samatta,Msuva,Banda na Farid Mussa hii inatuonyesha Tanzania tunavipaji vya kutosha..
Mimi bado nalia na watu wenye mamlaka juu ya haya..Jaribu kufikiria wakati Msuva anakwenda Morocco, Shiza Kichuya nae alipata dili la kwenda kucheza huko Afrika Kaskazini..Lakini baadaye tulisikia Kichuya karudi kwa sababu za kimaslahi..Nimezisikia sana hizi sababu za kimaslahi..
Tatizo limekuwa sana kwenye sababu za kimaslahi… Hii ni kwa wote timu,wachezaji na mawakala…Tumekuwa tukihitaji fedha nyingi na za mkupuo ifikapo mchezaji wetu anapo hitajika na timu za nje..Najaribu kukumbuka Haruna Moshi Boban aliamua kurudi bongo kisa maslahi..Hata Kapombe pia aliondoka France kisa maslahi..
Hapa Napata picha kuwa tatizo liko kwetu sisi..Timu zetu,wachezaji na mawakala..Tumekuwa tupo nyuma sana kwenye suala la mikataba..Leo hii skauti akiambwa kuwa kuna kipaji kutoka Tanzania na Nigeria nadhani wakala atakiwahi kipaji cha Nigeria..Kwakuwa tayari Nigeria wanawachezaji wengi maarufu ulaya..Hii inakuwa rahisi sana wao kukubalika..Lakini sisi ulaya tuna Samatta tu ambaye bado hajafikia umaarufu wa Jay Jay Okocha,Taribo West wala Mikel John Obi
Watu wetu lazima wae wajanja kwenye suala la maslahi..Ujanja wenyewe upo kwenye mikataba..Na mikataba ya siku hizi inakua imara kutokana na performance ya mchezaji..Nakumbuka wakati Chelsea inamsajili Oscar kutoka klabu ya internacional ya brazil Oscar alitakiwa kulipwa pesa kiduchu tuu kwa wiki lakini kutokana na kucheza vizuri Oscar mshara ulipnda mpaka pauni 60000
Jaribu kufikiri jambo dogo tuu..Endapo simba kama wangemuuza Samatta kwa pesa kiduchu kwenda TP mazembe then wakaweka vipengele vifuatavyo kwenye mkataba wake..Wangeweka labda endapo TP mazembe wakichukua ubingwa wa Congo then simba ipate kiasi Fulani..Endapo TP Mazembe ichukua kombe la Afrika na Samatta basi simba ipate kiasi Fulani..Au endapo Samatta atauzwa kwenda timu za ulaya simba ipate kiasi Fulani..Je simba leo ingekuwa imemuuza Samatta kwa kiasi gani?????
Msuva anacheza Morocco ambapo ni jirani sana na Hispania..Morocco kuna maskauti wengi sana wa ulaya wanaangalia vipaji vya morocco..Hivyo ni rahisi kwa Msuva kupata timu ulaya..Je Yanga wanaweza kufaidika vipi endapo Msuva atasajiliwa na timu kutoka ulaya?????????
Jaribu kuangalia mkataba wa Isco unavyo ifaidisha Malaga kila Isco anapopata ubingwa na Madrid
Jaribu pia kuangalia jinsi ambavyo Neymar alivyokuwa akinufaika yeye na Santos kwa kila stage ambayo Barca ilifuzu katika champions league na makombe mengine
Ni wakati wa timu,mawakala na wachezaji wetu kuwa wajanja kwenye mikataba..Sidhani kama kuna haja ya kuhitaji donge nono kwa mchezaji kama kichuya,gadieli michael,domayo au mchezaji yeyote anayecheza VPL kwa mkupuo..Donge nono siku hizi linakuja katika mikataba ya kijanja inayo tokana na performance ya mchezaji..
Watanzania tubadilike..tunahitaji Professional footballers wengi Zaidi katika nchi yetu ili tuweze kufikia malengo yetu