Siku chache zilizopita, Waziri wa Utumishi na Utawala Bora akiwa mkoani Kigoma, alijinasibu kuwa kuanzia tarehe 20/12/2021 yaani siku ya Jumatatu iliyopita wataanza kulipa malimbikizo ya watumishi. Cha kushangaza wamelipwa baadhi na wengine hatujalipwa.
Hivi kweli tokea Mei, 2019 mpaka sasa takribani miaka mitatu kinachoshindikana hasa nini kulipa stahiki zetu?
Wengine wanacheka, wengine tuna huzuni kuu.
Tafadhali sana Mh Rais na Mh Waziri wa Utumishi tunaomba kuwepo na usawa katika hili la kulipa stahiki za watumishi. Maana hakuna asiye na uhitaji.
Ni kama mnatugawa pasipo sababu za msingi. Ninawaomba mrekebishe hilo, sote tuneemeke na jasho letu tulilolitoa katika utumishi wetu.