Kwani kudai Katiba mpya kuna dhambi gani?

Kwani kudai Katiba mpya kuna dhambi gani?

Kikwete huyu mliyekuwa mnamuita dhaifu? Au kuna mwingine?
Yaani hawa ndugu "wanarukaruka" tu....🤣🤣

Jana Lema anasema AFADHALI UTAWALA WA JPM kuliko wa DIKTETA wa sasa 😲😲🤣🤣

#KaziIendelee
 
Uhusiano inakuja pale hali za maisha inapokua bora hivyo vitu Kama ndio maendeleo hata mkoloni alijenga miaka hiyooooo
Mkuu mkoloni MUINGEREZA hakujenga hivyo vitu.....

Mkoloni MJERUMANI alijenga yafuatayo:

1)Reli (kwa ajili ya kusafirisha biashara yake ya mkonge/katani n.k)

2)Bandari ya Dar (kwa ajili ya kusafirisha na kupokea vitu vyake)

3)Hospitali ya SEWA HAJI ilijengwa kwa huruma ya mhindi mzalendo ambaye aliingiwa imani baada ya kuona hatutibiwi mahospitalini

4)Maboma yao ya wilaya(kwa ajili ya utawala)
*******************

Leo karibia kila MKOA umeunganishwa na LAMI(DRC hawana)

Leo Kuna vyuo vikuu VINGI MNO....
Leo Kuna vyuo vya kati na Veta kibao.......
Leo kuna VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI ,HOSPITALI ya rufaa kila Mkoa.......

Daah MAMBO NI MENGI MNO.....je unataka kusema kipindi Cha mkoloni Hali zetu zilikuwa ni Bora kuliko Sasa?!!!

#KaziIendelee
 
Mkuu mkoloni MUINGEREZA hakujenga hivyo vitu.....

Mkoloni MJERUMANI alijenga yafuatayo:

1)Reli (kwa ajili ya kusafirisha biashara yake ya mkonge/katani n.k)

2)Bandari ya Dar (kwa ajili ya kusafirisha na kupokea vitu vyake)

3)Hospitali ya SEWA HAJI ilijengwa kwa huruma ya mhindi mzalendo ambaye aliingiwa imani baada ya kuona hatutibiwi mahospitalini

4)Maboma yao ya wilaya(kwa ajili ya utawala)
*******************

Leo karibia kila MKOA umeunganishwa na LAMI(DRC hawana)

Leo Kuna vyuo vikuu VINGI MNO....
Leo Kuna vyuo vya kati na Veta kibao.......
Leo kuna VITUO VYA AFYA ,ZAHANATI ,HOSPITALI ya rufaa kila Mkoa.......

Daah MAMBO NI MENGI MNO.....je unataka kusema kipindi Cha mkoloni Hali zetu zilikuwa ni Bora kuliko Sasa?!!!

#KaziIendelee
Ninachotaka kukuambia hicho unachosema hata mkoloni alifanya lakini hali ya maisha ya watu haikua bora na ndicho kinachofanyika Sasa hivi hali ya maisha ya watu sio bora ukiondoa kundi dogo la watawala na wanaowazunguka.jiulize sawa wamejenga hayo yote je kule kijijini huduma zilizopo zinamkomboa mwananchi kifikra,kiafya au kiuchumi,mpaka leo kwa rasilimali tulizonazo je tunauza bidhaa au mali ghafi kwanini ndio utajua hiyo miundo mbinu bado ina malengo yaleyale ya kikoloni
 
Kumbe tulikosea lile kusanyiko lililokaa kujadili Rasimu ya Tume ya Jaji Warioba lilikuwa genge la kutengeneza chokochoko na ugaidi na halikuwa Bunge Maalum la Katiba Mpya.
 
Hebu tuambizane ukweli, kudai katiba mpya kuna dhambi gani katika taifa hili mpaka kufikia hatua ya kufungulia na kesi za ugaidi? Kwani mjadala tu wa kuidai katiba mpya una tatizo gani hadi kufikia kukamata viongozi wote wa chama kimoja kilichotajwa kufanya mjadala huo?

Hivi ni kweli CCM hamchukui mifano kutoka mataifa mengine mkajifunza kua movement ya katiba ni suala gumu na kulizuia hamuwezi? Dunia imejua kua katiba ya Tanzania ina kasoro kubwa na ndiyo chanzo kikubwa cha ukandamizaji wa haki za binadamu.Hili suala limeamshwa kulizima ni ngumu maana si la CHADEMA pekee, mnakoelekea sasa mtakamata wanaharakati watakaoendesha mijadala hii na si wanasiasa pekee.

Mnamfungulia mashtaka ya Ugaidi kiongozi ambaye tangu kuanza kwake siasa akiwa kijana mdogo wa miaka 20 hajawahi hata kutuhumiwa kutishia kumpiga mtu achana na kuua, hiki mnachokifafanya kilianza kupata shinikizo la kimataifa tutakua salama?

Jeshi letu linatoa maelezo ya kujichanganya kua halijamkamata Mbowe kwa sababu ya mjadala wa katiba, sasa hao viongozi wengine wa CHADEMA wamekamatwa na kwenda kupekuliwa kwa sababu gani? Hii dhambi kubwa ya jeshi letu itatuvusha? Wanadhani hili jambo linaweza kuzimwa kwa wepesi kiasi hicho?

Hivi polisi wanaelewa maana na madhara ya kukamata kiongozi mkuu wa chama kikuu cha upinzani katika taifa lolote lile? Mbaya zaidi kumtuhumu kwa kesi ngumu kama ya ugaidi mtu ambaye hana historia ya matukio hayo maisha yake yote. Ngoja tupate mashinikizo ya jumuiya za kimataifa ndio tutajua,sisi tujawe na viburi vyetu lakini tutaelewa mbeleni.
Ni kuhatarisha uhai wa ccm na genge la wahuni wa humo ndani
 
Dawa ya kuuondoa Ujinga ni Kuelimisha sio kuwacheka na kuwakebehi kama unavyo Fanya!
Na ukae ukijua hata mjinga naye Anayo Haki kwenye Nchi Yake, Ambayo kitovu chake kimedondokea!

ISA. 29:24 Hao nao wakosao rohoni mwao watapata kufahamu, na hao wanung’unikao watajifunza elimu.

MIT. 4:10-13 Mwanangu, sikiliza, na kuzipokea kauli zangu; Na miaka ya maisha yako itakuwa mingi. Nimekufundisha katika njia ya hekima; Nimekuongoza katika mapito ya unyofu. Uendapo, hatua zako hazitadhiikika, Wala ukipiga mbio hutajikwaa. Mkamate sana elimu, usimwache aende zake; Mshike, maana yeye ni uzima wako.
Mkuu hii Biblia unayotumia ni aina gani?na naipataje?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Ndio alithubutu.....

SGR....
NDEGE...
BWAWA LA MWALIMU NYERERE....
MAKAO MAKUU YA SERIKALI DODOMA.....
UKUTA WA MBUGUNI MERERANI....

👆👆👆👆👆👆👆👆
Hayakuonekana huko nyuma

#KaziIendelee
he was simply a killer
 
Back
Top Bottom