Kwani Kuna ulazima wa watu kuchangia mchango wa harusi?

Kwani Kuna ulazima wa watu kuchangia mchango wa harusi?

Mtu afanye harusi yake, familia yake inatosha kwa bajeti atakayoiandaa kulisha ndugu zake watakaohudhuria. Haina haja ya kusumbua watu baki wachange kufanikisha sherehe. Mtu apige mahesabu ya kulisha wanaukoo wake watakaohudhuria watakula kiasi gani agharamike mwenyewe. Akiona ni ghali na hana hela basi afunge ndoa tu na arudi kwake akale msosi wa nyumbani kwake kama kawaida na maisha yaendelee.
 
Kufanya harusi bila kuchangisha watu inawezekana. Unaenda kwa msajili wa ndoa kanisani, msikitini, bomani au milani unafungiwa ndoa kirahisi tena kisheria kisha unarudi nyumbani kuanza maisha ya ndoa. Si lazima ndoa ifungwe kwa sherehe za gharama kubwa za kuchangisha watu, jibebe mwenyewe
 
Nimeshuhudia Kuna watu wanakosana na marafiki ndugu kisa alishindwa kutoa hela ya mchango wa harusi

Kwani ni lazima kufanya harusi na hauna bajeti?
Siyo lazima.Harusi siyo tukio la ghafla.Anayetaka kufunga ndoa ana muda mrefu wa kujipanga na kuamua harusi yake iweje.Mchango utolewe kwenye ndoa ya mkeka tu.
 
Ndugu mdau kama ww ulishatumia michango ya watu kuendesha shughuli yako na wewe changa tu usikwepe na pia kama unaona ww unajiweza kiuchumi kwenye mambo yako ya shida na raha basi michango sio lazima (sikuizi michango ni uwekezaji utakaokufaa kwenye shida na raha)
 
Watu wana guts 😀
We Wakomeshe na setting za wasap yako.. ukiset asikuadd yeyote basi zinakuwa zinakuja kama link we ndio unachagua uingie au upotezee..
Tupe shule hii unaingia wp hadi unafika huko
 
Nimeshuhudia Kuna watu wanakosana na marafiki ndugu kisa alishindwa kutoa hela ya mchango wa harusi

Kwani ni lazima kufanya harusi na hauna bajeti?
Sio lazima!
Mungu aniwezeshe harusi za wanangu sitachangisha..... waalikwa watakuwa watu wachache tu na zawadi zao mkononi 😂 😂 Ukifika unakabidhi zawadi mlangoni unaingia ukumbini, ni mwendo wa kula, kunywa na kucheza tu, ndani ya saa 2 hadi 3 tunatawanyika, sio tunawekana ukumbini hadi saa saba usiku
 
😂😂hutaki mambo mengi
 
Haya mambo ya mamichango achana nayo !!!
Hasa sherehe sijui harusi, birthday, sendoff n.k

Changia vitu muhimu tu kama msiba ama ugonjwa tena kwa watu wako wa karibu !!!!

Mtu mmesoma wote o_level ama primary, 10yrs+ huna namba yake na hamuwasiliani...from no where eti unakuwa added kwenye grp anaoa....uote mchango....

Sitoi hela yangu yaan...uzenge
Naunga hoja mkono
 
Back
Top Bottom