Wana MMU,
Mimi jembe tangu nitelekeze mchumba nimebaki najiuliza hivi kuoa au kuolewa ni lazima au?
Nisipooa kwani kuna kitu kinapungua? maana mi naona kuishi na mtu mwenye kwao naona nikuzinguana tu. Kwani nisipooa eti wanasema kwenye jamii sitaheshimika, kwani heshima ni mke?
Mbona vitabu vitakatifu vinasema kama utaweza kujizuia basi usioe, sasa inakuaje nisipooa watu wanaanza kuhoji oooh labda mgonjwa, oooh labda ana gundu sasa wewe inakuhusu nini?
Eti home jana wameniuliza naoa lini mimi nimewajibu mpaka nifikishe miaka 65.jaman tusaidiane hiv kuoa ni lazima?