Kwani madereva wa vibaby walker wana fujo sana?

Mtu huna upcountry trip sana unaanzaje kununua above 3000cc cars!?.. Nunua hata IST ikubebe mjini hapa lower fuel, less service, longer comfortability.

Siwatetei wenye Passo (kagari kabaya kale bora hata probox).
 
Unasave vipi pesa usiyonayo ?
 
Ukishaendesha gari kubwa manake una uwezo wa kulimiliki.ishi kwa kujinyima usave nduguzo wapiganie mirathi hata wanao wasifaudu
 
Mtoa Maada ngoja ni kwambie nitu,ukiwa na nyumba yenye room moja na sebule unahesabika una nyumba na mwenye ghorofa naye tunasema ananyumba,mwenye semi anagari na mwenye Vitz anagari huwezi sema ana baiskeli,kama wewe umebarikiwa kununua Hammer mshukuru Mungu naye mwenye Vitz/ Stalet naye anamshukuru Mungu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna aliesema Vits sio gari?
 
Ni kama walivyo wanaume wafupi...vinafujo, vibishi kila saa vinahisi vinadharauliwa..
Ndivyo ilivyo kwa madereva wa baby walker wanahisi wanadharauliwa na wenye mafuso

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani kakwambia kuwa speed limit ni 80.. ?
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi Kwa nini madereva wa vibebiwoka wana vurugu sana barabarani? Ni ugeni wa gari au sms(short man syndrome)?
Wengi ni new drivers. Wanashangaa kuona kigari kidogo lakini kina mbio. Vile wanaona daladala na gari nyingine kubwa haziendeshwi mbio mara nyingi.

Hii pia naiona kwa wanaonunua gari ndogo za Ulaya. Unaweza hisi hazina speed za chini. Maana wakiingia tu wanataka kuondokea 60 na kuendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…