1995 | Teddy Kilenza Magayane-CCM 61% | Daniel Nsanzugwanko NCCR 33% |
2000 | Michael Mussati-CCM | CCM haikurudisha jina la Nsanzugwanko |
2005 | Daniel Nsanzugwanko –CCM 56.1% | Agripina Buyogela-NCCR 38.4% |
2010 | Agripina Buyogela-NCCR (54.58% | Daniel Nsanzugwanko –CCM 38% |
2015 | Daniel Nsanzugwanko –CCM | |
2020 | Prof. Joyce Ndalichako VS Daniel Nsanzugwanko |
Kwa hizo laps lazima mafao yapotelee kwenye harakati. Yani mbunge aliyekaa mfululizo miaka 10 ana afadhali kuliko mbunge ambaye gari linakata kata wese kwenye uchaguzi hata akae miaka 20 bungeni hutoona mafanikio yake.
Ukweli mtupu kule hanang' Mary Nagu ni mbunge toka nipo primary,mpaka leo Nina mjukuu,yupo tuu(in makongoro's voice) na bado juzi kasema atarudi,,,tumewachoka hawa watu,MBUNGE MIAKA 25? USIWE KUPE
1995Teddy Kilenza Magayane-CCM 61% Daniel Nsanzugwanko NCCR 33% 2000Michael Mussati-CCM CCM haikurudisha jina la Nsanzugwanko 2005Daniel Nsanzugwanko –CCM 56.1% Agripina Buyogela-NCCR 38.4% 2010Agripina Buyogela-NCCR (54.58% Daniel Nsanzugwanko –CCM 38% 2015Daniel Nsanzugwanko –CCM 2020Prof. Joyce Ndalichako VS Daniel Nsanzugwanko
Ndugu yetu Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko amekuwa akipambana kupata ubunge tangu 1995, Mwaka 2010 alikosa ubunge maisha yalikuwa magumu sana kiasi kwamba mikopo aliyochukua bank ulimfikisha pabaya kiasi cha kuuza Nyumba yake pale Kasulu. Inaonekana nje ya ubunge maisha hayawezi.
Jimbo la Kasulu Mheshimiwa Prof. Joyce Ndaliachako anaonekana kutia nia hivyo kumnyima usingizi. Juzi alisikika Nsanzogwanko akilalamika eti miradi ya elimu iliyopelekwa jimboni kwake ni mipango ya Serikali na siyo Mtu anaejipitisha eti katika jimbo lake, nani amesema Nsanzugwanko ndiyo mwenye hati milki ya ubunge wa jimbo la Kasulu?
Pia, alisikika Mheshimiwa Obama Mbunge wa Buhigwe-Kasulu akilalamika eti kuna mtu anajitisha katika jimbo lake (akimaanisha Mheshimiwa Waziri wa Fedha Dr. Philip Mpango) alietangaza kutia nia kugombea jimbo hilo. Obama alibweka bungeni akilalamikiwa kuvamiwa jimboni.
Huu ni mfano kwa majimbo mengi hapa nchini baadhi ya wabunge kuona kwamba watanzania wengine hawatakiwi ya kugombea majimbo yao. Kwa mfano Mheshimiwa Daniel Nsanzugwanko amekuwa katika harakati za ubunge kwa miaka 25 sasa huku jimboni kwake hakuna jipya.
Amekuwa akionekana active akichangia wakati kama huu ili aonekane jimboni kwake. Aliwahi kuwapiga makofi/vibao wananchi waliompokea kwa madumu ya maji kama ishara ya kuonyesha kero waliyonayo. Sasa ni wakati wa wabunge kama hawa kuacha demokrasia iamue mbunge anaefaa kuwatumikia wananchi.
Na mzee wa vijisenti je? Aliingia bungeni kama mwanasheria mkuu wa serikali mwka 1993 kabla hajaachana na nafasi hiyo na kuendelea na kugombea ubunge.Ukweli mtupu kule hanang' Mary Nagu ni mbunge toka nipo primary,mpaka leo Nina mjukuu,yupo tuu(in makongoro's voice) na bado juzi kasema atarudi,,,tumewachoka hawa watu,
"Miaka 5 inatosha sana kutusua kwa mbunge ".Tatizo wanachukua mikopo mikubwa sana na wanajiendekeza life ya juu sana
Ananuna gari milioni 100 angeweza vuta used tu za hapo japani na kuzibadilisha kila ikichoka
Kuna Gari zinahimili safari ndefu Kama kluger,Suzuki ,escudeo grand Vitara ,hata Alphard nzuri na za dizaini hio Sasa unakuta jamaa kavuta VX v8 halafu ikifika kipindi Kama hiki kichwa kinauma
Gari inakula mafuta ,kampeni za kuchaguliwa upya zinatka hela za waganga ,kuhonga nakadhalika
Matokeo yake kiinua mgongo chote kinafyekelewa huko .
Ana mikopo ya miradi ya ajabu ajabu haiingizi faida yeyote
Ndio maana hawaachi kugombea Tena na Tena unakuta alichovuna kwa miaka 5 anaenda poteza katika hii miezi 3 ijayo Hasa kwa wale wanaohemea ubunge tu .
Miaka 5 inatosha sana kutusua kwa mbunge
Sent using Jamii Forums mobile app
Pia Kuna kutusua ndani yake we unadhani wanasukumwa na hicho unachowaza wewe [emoji3][emoji3][emoji1787]pole sana"Miaka 5 inatosha sana kutusua kwa mbunge ".
Unachagua mbunge ili akatusue!!??
Unagombea ubunge ili utusue!!!???
Mwakilishi wa wananchi ni nani!!???
Ni ukweli mtupu. Mzee chenge,job ndugai, na wengine tangu mkapa wapo Tu.Pia Kuna kutusua ndani yake we unadhani wanasukumwa na hicho unachowaza wewe [emoji3][emoji3][emoji1787]pole sana
Ubunge una ulaji asikuambje mtu
Hizo slogan za kutetea wananchi na kijikazi uchwara Cha kusiriba ulaji uliopo ndani yake
We hujawahi jiuliza mbunge Ni kasulu huko lakini anaishi dar why kwanini asikae na wananchi wake jimboni
Wananchi mkae na shida zenu yeye anakula upepo mbezi beach akifika bungeni anasisinzia akishtuka anagonga meza na kusema ndiyooooo!! Anasaini posho huyo zake mnadani kula nyama nyie mpambana na madumu ya maji huko kwenye kilimahewa[emoji1787][emoji1787]
Ubunge tunaangalia maslahi sio hayo mawazo yako[emoji1787][emoji1787][emoji123]
Sent using Jamii Forums mobile app