kwani mfumo wa cash less unasua sua Tanzania

julaibibi

JF-Expert Member
Joined
Jun 16, 2020
Posts
3,081
Reaction score
4,224
Mifumo hii ya cash less kwa maana ya kulipa bila kutoa hela ndio mradi wa dunia ya kisasa ila kwa hapa naona kama watu wanaikwepa chukulia tu lipa kwa namba

Wengi ukienda anakwambia sina namba hasa hasa maeneo yenye huduma za muingiliano mkubwa kama mfano Kariakoo. Wengi wanazo na wengi hawana. Hivi hadi leo kweli dunia ya sasa ulazimike uwe na hard cash all the time? Kwanini isiwe lazima kila anayefanya biashara awe na mfumo wa cashless na hii TRA na hawa providers kama kina Yas, Voda na wengine watoe ofa Bure kabisa kutengenezewa lipa namba.

FAIDA ZA CASH LESS.(KWA TANZAANIA LIPA NAMBA)
● Inaepusha na chuma ulete. hela zako zinakua salama kwako mfanyabiashara
● Kupunguza shida ya chench. lipa ina uwezo wa kulipa mpaka sent 50.
● Inaondoa kaz ya kubeba beba mahela na mifuko ya nguo kutoboka.
● Usalama wa hela.
Wenzetu China sasa hivi una scan macho tu baam umelipa huduma. kwa vile hatujaweza kufika huko. Lipa namba pia inasaidia au zile mashine za POS.
 
Vipi kuhusu "makato ya ziada", mfano nanunua kitu cha elfu 20. Je, kwenye account yangu (bank, mobile, apple pay nk) inatoka elfu 20 tu au +additional charges?

Mi sio mdau wa izo mambo ila kuna siku nilileta uzungu pale Discount Center M'City nikalipa kwa kadi kwenye POS yao. Ilikatwa mara mbili maana transaction ya kwanza ilionekana kama imefeli, ya pili ndio ikakubali. Kumbe zote zimekubali.

Sio case, nikacheki statement baada ya masaa kadhaa nikarudi. Kwao haijafika kwangu imetoka.

So nikaenda NMB nikajaza form flani na maelezo (inakua kama mtu alietoa hela ATM afu pesa haijatoka ila imekatwa) pesa ikaja kurudi baada ya kama siku 3.

Check mlolongo huo.

Pia issue ya usalama, mfano debit card skimmer. Wenye maduka sio wote waaminifu, wapo wanaoweza kuweka skimmers izo ukiweka card yako inachukua information zao kama namba ya card, CVV, date of expiro, jina lako ambavyo anaweza kutumia baadae kufanya manunuzi online. Ingawa hii kidogo imepunguzwa na OTP ila bado ni shida.

Na pia wengi wetu tunaenda kununua vitu katika maduka ambayo hawapokei izo aina za malipo. Kama serikali ingependa hii game, ingeanza kwa kulazimisha vituo vya mafuta vyote kiusalama kupokea malipo kwa kadi tu. Mfano Total na Puma waka kadi zao unajaza hela kama kadi ya mwendokasi unakua unatumia kuweka wese.

Me naona izo ni changamoto kwangu.
 
Tutafika taratibu. Ujerumani wenyewe imewachukua muda raia kuweza kubadilika wawe wanatumia cashless payments lakini hata sasa bado cash payments zina account 51% ya malipo yote ya points of sale. Napo hapo asilimia imeshuka sana.
So tutaenda mdogo mdogo. Pia nadhani inachangiwa na watu wengi hasa vibarua ambao ni wengi kulipwa kwa cash hapa kwetu. Ukinilipa kwa cash na matumizi yatakuwa kwa cash.
 
Tumekosa nia ya dhati katika hilo, lakini hili jambo ni rahisi mno na ni salama.

Mfano China wanafanya malipo cashless kwa kila kitu haijalishi ni biashara gani na ipo level gani.
 
Lipa namba kwa kwetu hapa ni muhimu kuanza na hawa wafanyabiashara.
 
wewe unachanganya madesa,jamaa anazungumzia LIPA NAMBA!!!
 
tuache kujiendekeza LIPA NAMBA nayo mnataka mpaka muone ujerumani wamefanya ndo muige???!!!
 
tuache kujiendekeza LIPA NAMBA nayo mnataka mpaka muone ujerumani wamefanya ndo muige???!!!
My point ni kwamba adaption ya haya mambo na kwa mazoea ya watanzania itachukua muda sana ukizingatia watu wengi wanalipwa cash maana watanzania wengi ni vibarua. Kama nchi iliyoendelea kama germany nayo imechukua muda sana bila shaka na sisi adaption itaenda taratibu.
Hebu imagine mimi nafanya kazi kiwandani nalipwa 7000 kutwa tena cash au weekly 32000 kwa cash. ni ngumu nitakapoanza kuitumia niweke kwenye simu ili nifanye lipa namba. Kwanza lipa namba ina gharama za malipo wakati cash nalipia exact amount.
 
Shida hatuaminiani wabongo watu uogopa mtu anaweza zirejeshe kwenye simu yke baada ya huduma.uelewa pia shida ya mitandao kidogo kidogo tutafika
 
Ila hii mifumo ya cashless imefanya kazi ya ujambazi ikose Dili watu hawatembei na cash kama zamani
 
Kwan hizi kampuni za mafuta hazina prepaid card yaani unanunua mafuta kwenye card gari ikiisha wese unaenda na card yao kwenye kituo chao unajaza tu hadi itakapoisha kama mwendokasi
 
Kwni hizi cashless ni FreeCharge yaani unakatwa unacholipa pekee au kuna transaction cost
 
wewe unachanganya madesa,jamaa anazungumzia LIPA NAMBA!!!
Unapolipa kwenda lipa namba wanakata ada ya muamala. Hiyo haijakaa sawa. Ufanye kibarua cha 20000. Ulipwe kwa simu labda. Ukienda kununua sukari kilo moja kwa lipa namba, lazima watakata 200 ya ada. Ukienda kununua kingine wakati mwingine, watakata tena ada. Hapo ni changamoto
 
kwahiyo wewe kwa akili yako wakiacha kutoza hizo mia mia unahisi watafanya vipi maintainance ya hiyo mifumo.

Unahisi kampuni zitajiendeshaje labda??!!!
 
MCHAWI WA YOTE NI MAKATO BINI TOZO.

Mfano leo nimetuma sh.100,000 toka App ya CRDB kwenda tigo imekatwa sh.7100,halafu ili yule jamaa niliyemtumia atoe hiyo hela kama ilivyo imebidi nimtumie sh.105,000. so jumla nimelipa transaction charge ya sh.12,100 hii ni asilimia 12.1% ya hela niliyotuma. huu sasa si ni wehu.ningeenda kutoa ATM Ningekatwa 1200 tuu nikamlipa keshi.Sasa hapa tunaenda mbele au tunarudi nyuma.
 
na ni easy kumiliki LIPA NAMBA,shida ni MIJITU MYEUSI kila kitu haifanyi mpaka ilazimishwe.
nachkukia hasa uanaenda kariakoo kuna duka moja la cosmetics ukinunua ana bei nzur tu.vitu ving unachagua chagua ukifika kulipa unamuuliza naomba lipa namba anakwambia sina.ila lnina namba ya wakala toa.naweza kuelewa kuwa ni janja yake ya kuingiza pesa nying mana anaku force utoe pale pale ulipe. ndio mana nashangaa why this Lipa isiwe lazima kwa mfanyabiashara.mwanzon nilihis labda wanaogopq kuwa tracked kimahesab may be wanaogopa kodi. laki n kuna mtu akaniambia wala hizo hazihusiani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…