okay ni hivi . katika mambo ya grammer kwenye kiingeeza huwezi sema
i bought me a helicopter au
I'm going to buy you a helicopter
- hizi sentensi hapo juu zina grammatical errors ingawa mesegi yake ipo wazi na inaeleweka vzr tu
Sasa basi kwanini mond kasema ili kuwa waiga jamii ya wamarekani weusi ambao hupendelea kusema hivyo.
Historia
Jamii ya watu weusi waishio marekani wanamovement yao ambayo kimsingi wanataka jamii ya watu weusi (america -blacks ) wawe tofauti na jamii ya watu weupe . Na utofauti huo wanataka uanzie
-Uvaaji
-Uongeaji
Hapa kwenye uongeaji ndyo nataka nipazungumzia haswaa. Katika uongeaji jamii hii imeanzisha lugha isiyo rasmi inayoitwa ibonic language ni lugha isiyo lasmi kwasababu inaongelewa sanaa na wamarekani weusi lakini bunge la marekani bado halijaitambua lugha hii . Lugha hii ni lugha ya kiingeeza ambayo wameamua kwa makusudi kabisa kubadilisha mifumo ya lugha ya kiingeeza ili kujitofautisha na jamii ya watu weupe .
Mfano.
1) Imma call you tonight
- Lemme Call you tonight
-He ain't my type
- i don't go no where today .(mfumo unaohusisha matumizi ya double negative ) katika sentisi moja
Katika lugha ya kiingereza hamna kitu kama hichi ni kosa kusema hivi lakini jamii ya watu weusi hutumia imma badala ya i 'm going to ili tu kujitofaitisha na jamii ya watu weupe hivyo hapo ilibidi iwe
-I'm going to call you tonight.
-I don't go no where today badala ya
- I don't go anywhere today
- he aint my type badala ya he is not my type
Mfano 2.
imma buy you a nice car .
- buy you ilibidi iwe i'm going to buy a nice car for you. Lakin jamii ya watu weusi hupendelewa kusema hivyo ili kuepuka hii kauli "you speak white " kutoka kwa wenzao weusi .