Hicho kinaitwa "kibuti cha kidiplomasia".Hilo la kuitana ndugu hata usihoji maana Tanzania ndio lipo sana.
Kuna demu wa Kitanzania aliwahi nikomesha na hilo la undugu...hehehehe. Nilitia jitihada nyingi sana kumtongoza, tukazoeana na kuwa marafiki wa karibu, sasa nilipoanza kubadilisha gear ili nielekeze uhusiano uwe wa kimapenzi akaibuka na "jameni tumezoeana hadi umekua ndugu yangu, hatuwezi kuwa na uhusiano wa kimapenzi".
Nilibaki hoi nikajiuliza maswali mengi sana, ni nini nilichokifanya hadi mrembo akaniona nimekua kama ndugu yake. Anyway, ilibidi tuendelee kuwa marafiki na zaidi tukawa mandugu hadi leo.
Dunia nzima inasema Obama's half brother lkn ukija kwa Waafrika tunasema Obama's brother, ni kwa nini?
Je ni kwa sababu ya polygamy kwamba sisi jamii yetu inaruhusu polygamy?
Huyo mmoja ni mchotara (Obama) yaani Mama yake ni Mzungu na Baba yake Mwafrika mweusi kama mimi huyo mwingine Baba yake mweusi kama mimi na Mama yake pia mweusi, ndiyo maana huitwa Obama's half brother!