DOKEZO Kwani Serikali inamuogopa Bayi na wenzake? Hatupati Medali Olimpiki kutokana na makandokando ya Viongozi wa juu wa TOC

DOKEZO Kwani Serikali inamuogopa Bayi na wenzake? Hatupati Medali Olimpiki kutokana na makandokando ya Viongozi wa juu wa TOC

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naanza na kunukuu maneno ya Mwanariadha maarufu Nchini, Alphonce Simbu ambayo nimeona JamiiForums.com ilimnukuu wakati anawasili akitokea Paris, Ufaransa alipoenda na Wanamichezo wenzake kushiriki Michezo ya Olimpiki 2024.

Simbu “Tulitakiwa tuijue njia ambayo tutaenda kukimbia miezi miwili kabla ili tuweze kuifanyia mazoezi kuanzia hapo lakini tuliijua siku za karibuni kabla ya kuelekea Paris kwa kuona ramani yake, hiyo ilikuwa ni changamoto kwetu na ilichangia kutofanya vizuri.”

Mwisho wa kunukuu, kama unahitaji kusoma hilo andiko zaidi bofya hapa ~ Alphonce Simbu: Hatukwenda kuiangalia njia(Olimpiki 2024), tuliiona tu kwenye Mtandao

Kabla sijaendelea tena, nigusie kwa ufupi barua iliyowahi kuandikwa na Faustin Musa Starehe kuelekeza kwa Waziri wa Michezo mnamo Februari 21, 2022.

Kwa ufupi, Faustin alisema “Viongozi wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC) wamekaa madarakani kwa zidi ya Miaka 20 bila hata medali moja ya Olimpiki, wao wametajirika kutokana na fedha za ruzuku kutoka Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Duniani (IOC) ambapo tangu mwaka 2000 fedha hizo zinaweza kufika Tsh. Bilioni 5.”

Faustin akasema, amewahi kuiwakilisha Nchi katika michezo hiyo Mwaka 2012, anajua mengi na anavyo vielelezo zaidi ya 500, lakini sikumbuki kama aliwahi kutiliwa maanani zaidi ya kusema amekuwa akitishiwa maisha baada ya hapo.

Moja la mwisho kabla sijaandika hoja yangu ni kuhusu fedha ambazo TOC imekuwa ikipata kutoka IOC kwa ajili ya maandalizi ya kuelekea kushiriki Olimpiki. Fedha hizo huwa zinatolewa kwa vyama vyote vya Olimpiki Duniani kwa madhumuni ya kusaidia michezo yote, lakini zimekuwa hazifiki kwa walengwa husika.

Nimefuatilia Mitandaoni na kwenye vyanzo mbalimbali kuhusu fedha hizo, mgawanyo wake unasomeka hivi:

1) 2001 - 2004 Athens Olympic Games TOC walilipwa USD 282,594 sawa na TSH: 649,966,300
2) 2005 - 2008 Beijing Olympic Games TOC walilipwa UDS 293,863 sawa na TSH: 675,884,900
3) 2009 - 2012 London Olympic Games TOC walilipwa USD 680,592 sawa na TSH: 1,565,361,600
4) 2013 - 2016 Rio de Janeiro Olympics TOC walipokea USD 523,993 sawa na TSH: 1,205,183,900
5) 2017 - 2020 Tokyo Olympic Games TOC walipokea USD 586,132 sawa na TSH: 1,348,103,600

Kusoma zaidi unaweza kubofya hapa ~Kashfa kubwa kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), waziri pitisha fagio la chuma

TOC NI SHIDA
Sasa nije katika hoja yangu ambayo mwanzo kabisa naanza kwa kukiri TOC ni tatizo na ni tatizo hasa, wanaohusika na tatizo hili ni wale viongozi wa juu wa Kamati hiyo ambao ni Mwenyekiti, Gulam Rashid, Makamu Rais - Henry Tandau na Katibu Mkuu Filbert Bayi.

MIKATABA MINGI HAIKO WAZI
Viongozi hao wa juu wakiongozwa na Bayi ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wamekuwa na kawaida ya kufanya usiri wa mikataba inayohusisha michezo mbalimbali wanayoisimamia.

Mfano imewahi kutokea katika Olimpiki ile ya China, Bayi alishikilia msimamo wa mkataba ambao ulikuwa na fedha ndogo, wakati kulikuwa na mkataba wa fedha nyingi, mara tano ya kiasi ambacho kiliwekwa na ule aliokuwa anautaka Bayi, inadaiwa alikuwa ananufaika binafsi ndio maana akashirikia msimamo na jambo hilo likafanyika.

TOC WATELEKEZA WACHEZAJI AIRPORT WALIPOWASILI KUTOKA UFARANSA

Wachezaji walioenda kishiriki Olimpiki 2024 walirejea kwa mafungu, fungu lililohusisha Wanariadha wakiongozwa na Simbu lilitelekezwa Uwanja wa Ndege wa Dar bila msaada wowote.

Tandau ambaye alikuwa kiongozi wa msafara, aliwasili majira ya saa Kumi alfajiri, baada ya kukamilisha kila kitu akawa anaondoka uwanjani hapo, alipoulizwa na Wadau kuhusu walipo wachezaji akasema watakuja baada ya dakika 20.

Ajabu yeye akakusanya mabegi yake huyoooo akasepa, dakika 20 baadaye wachezaji ambao walienda kuwakilisha Taifa waliowasili, walipofika ikabainika mabegi yao yamebaki Cairo Nchini Misri ambapo ndege yao ilipita.

Wakaanza kuhaha kujaza fomu, wakati huo kiongozi wa msafara hayupo, ikabidi Mdau wa riadha na mwanariadha wa zamani, Suleiman Nyambui aliyekuwa uwanjani hapo, akaomba kuingia ndani kwenda kutoa msaada kwa Wanariadha hao ambao waliwasili Saa Kumi Alfajiri lakini hadi wanakamilisha na kufanikiwa kutoka nje ilikuwa imetimia 12:30 Asubuhi.

Program za Olypaafric zinazofadhiliwa kutoka nje zinafanyika Shuleni kwake, kungeweza kufanyika katika Shule za Jeshi, Serikali, inaamana hzipo hazi difanyie shuleni kwake, n kiongozi ni mwanaye

RUZUKU ZA WACHEZAJI ZINATAFUNWA
Fedha ambazo Wachezaji wanatakiwa kupatiwa kwa ajili ya kujiandaa ambazo ni ruzuku zimekuwa zikipigwa juu kwa juu kwa mika mingi nyuma, inadaiwa huu baada ya baadhi ya Watu kushtuka na kupiga kelel ndipo wakina Simba wakapewa fomu wajaze.

Bayi aliwapa fomu hizo kwa shingo upande kwa kuwa walilazimika kuzijaza zaidi ya mara mbili kutokana na sababu mbalimbali ambazo hazina kichwa wala miguu.

Pia Bayi na wenzake wamekuwa hawaweki wazi kiasi cha fedha ambacho wachezaji wanatakiwa kulipwa, wanafanya kama vile ni fedha za familia.

SHULE YA BAYI NDIO KITUO CHA MATUMIZI YA FEDHA ZA IOC
Najua hili sio jipya sana, ila niliweka hapa kwa faisa ya wengi, nimecopy na kupesha kama lilivyoandikwa huko nilikotoa:

1) Ndg Bayi anaamua ni shughuli gani itafanyika chini ya ufadhili wa IOC
2) Ndg Bayi huandaa hafla hiyo katika Shule yake iliyopo Mkuza Kibaha
3) Ndg Bayi na familia yake hutoa huduma zote zinazohitajika kwa shughuli hiyo (Milo, Ukumbi wa Mikutano na vifaa vingine, usafiri na malazi inapobidi)
4) Wote kwa pamoja; Bw Bayi mwenyewe, Rais wa TOC ndg Gulam Rashid na Makamu Rais wa TOC ndg Henry Tandau ndio wawezeshaji wa shughuli zote; mfano(Semina, kozi fupi, warsha n.k) na inasemekana wanajilipa mara kadhaa ya kiasi kinacholipwa kwa wanachama wengine ikiwa ni pamoja na Wajumbe wa Tume ya Wanariadha (Athletes Commission).


KAMATI YA OLIMPIKI HAINA MHASIBU MKUU
Mhasibu Mkuu wa TOC, Charles Nyange amejiweka pembeni kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu sasa, nilipofuatilia nimebaini kuwa jamaa aliona kuna ubabaishaji mwingi ambapo Mtendaji wa Kamati alikuwa akienda ndivyosivyo.

Kwa kuwa Nyange ni mtu msomi na ambaye ana msimamo na anayejielewa amekataa kuingia kwenye mchezo wa upigaji, hivyo Bayi kuonesha ubabe naye akamchukua msaidizi wa Mhasibu ambaye anaweza kum-control kamuweka hapo asimamie ofisi.

NI NGUMU KUWANG’OA, SERIKALI IPO KIMYA
Nguli hao wa TOC ambao wamekuwa wakishinda katika kila chaguzi, wao ni kama wametengeneza ufalme ndani ya TOC hata viongozi wa Serikali au mamlaka nyingine zimeshindwa kufuatilia na kuondoa michezo michafu inayotumika.

Nguvu ya fedha ni kubwa inayotumika hasa kwa kuwa Wapiga Kura wao ni wachache na ni rahisi kuwa-control.

FEDHA ZA MIRADI ZINAPELEKWA KATIKA SHULE YA BAYI
Shule ya Filbert Bayi imekuwa ikitumika kimkakati katika mambo mengi, kuna mirdi ambayo inakuja kutoka IOC inaishia kupelekwa Shuleni hapo na mtoto wa Bayo ndiye anayepewa jukumu la kusaidia.

Bayi alitakiwa kushirikiana na Serikali kutumi fedha hizo katika Shule za Serikali au Shule za Jeshi kwa kuwa fedha zinapokuja sio ufadhili wa shule yake, lakini anachokifanya ni kuendelea kujineemesha ili utajiri wote uwe wake na Serikali ipo kimya.

Miradi kama ya Olympafrica, fedha zinatafutwa tu na familia ya watu wachache kisha kila siku tunalaumu wanamichezo wetu hawafanikiwi Olimpiki.

Hivi Mamlaka za Serikali zinaogopa kufanya ukaguzi wa matumizi ya fedha hizo au kuna jambo linapita wanaohusika nao wanakuwa kimya?

Wachezaji wanakabidhiwa bendera ya Nchi kisha jambo linachukuliwa poa, kama vipi wasiwe wanakabidhiwa bendera kwa kuwa tunajua maandalizi ni mabofu na wanaenda kuaibisha Nchi tu kila Mwaka.

Pia soma ~ Rais Dkt. Samia: Hashiriki wetu hawafanyi vizuri Olimpiki kwa kuwa watuna maandalizi mazuri
 
Ama kweli kila mbuzi atakula kutokana na urefu wa kamba yake.
Hivi Mama Bayi bado yupo.? Nakumbuka back then 2012 mashindano ya Copa coca cola kitaifa tuliweka kambi hapo shuleni kwa jamaa kibaha. Jamaa kaanza kupiga mahela kitambo sana.
 
Bayi kama kweli anahujumu vipaji vyetu vya riadha anatenda vibaya mno, ila Sina uhakika kama anafanya hii dhuluma ili asiwepo mtu wa kuipiku record yake nasikia tu mtaani.

TAKUKURU tokeni ofsini chunguza hizi tuhuma za Bayi
 
Wakichunguza bila kulambishwa Rushwa niko pale najinyonga
Bayi kama kweli anahujumu vipaji vyetu vya riadha anatenda vibaya mno, ila Sina uhakika kama anafanya hii dhuluma ili asiwepo mtu wa kuipiku record yake nasikia tu mtaani.

TAKUKURU tokeni ofsini chunguza hizi tuhuma za Bay
Bayi kama kweli anahujumu vipaji vyetu vya riadha anatenda vibaya mno, ila Sina uhakika kama anafanya hii dhuluma ili asiwepo mtu wa kuipiku record yake nasikia tu mtaani.

TAKUKURU tokeni ofsini chunguza hizi tuhuma za Bayi
wa nchi gani? Wao wenyewe wanalambishwa kimyaaa
 
Ama kweli kila mbuzi atakula kutokana na urefu wa kamba yake.
Hivi Mama Bayi bado yupo.? Nakumbuka back then 2012 mashindano ya Copa coca cola kitaifa tuliweka kambi hapo shuleni kwa jamaa kibaha. Jamaa kaanza kupiga mahela kitambo sana.
Mama alishafariki muda mrefu.
 
Utamsikia akiingia madarakani disemba 14 mwaka huu....anahonga wajumbe wote pale dodoma hoteli
 
Waziri yupo songea kwenye kampeni za siasa, ameacha michezo hewani wajitegemee.

Kuna haja wachezaji wa zamani wapewe wizara ya michezo hawa wa sasa PUure kabisa
 
Back
Top Bottom