The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Nilimsikia waziri wa fedha akisema, kwa ajili ya kukuza kilimo cha umwagiliaji vikundi vya skimu za umwagiliaji, vitatozwa ada ya kuendeleza miradi ya umwagiliaji.
Hivi ni kweli kwamba serikali imeshindwa kubuni mbinu za kuwatafutia ruzuku wakulima wetu hata kwa kukopa toka mabenki mbalimbali?
Ni nani kwenye nchi hii asiyejua madhira wanayopata wakulima wetu ikiwemo kukosa uhakika wa masoko ya mazao yao, achilia mbali uzalishaji wenye tija ndogo.
Kwa maoni yangu nilidhani kilimo ni sekta inayohitaji kulelewa na serikali ili izidi kutoa ajira kwa wananchi kuliko kuwaongezea kongwa la ada za kuendeleza skimu za umwagiliaji.