Budget hii ya Waziri Wa Fedha imeweka dhahiri kwamba:
1) Dk Mwigulu haiwezi hio Wizara, na anageuka kuwa mzigo kwenye serikali ya SSH.
2) Waziri Wa Kilimo na Naibu Waziri wake sasa ni maadui wakubwa wa wakulima nchini.
Moja, huwezi kuruhusu upumbavu huu kufanyika kwenye wizara yako ya kilimo wakati wakulima bado hawajajiweza wala hawajaingia kwenye kilimo cha kisasa.
Pili, wakulima hawana mtaji na hawana masoko ya mazao yao wanayolima.
Tatu, swala la kilimo cha umwagiliaji kwanza lingepewa kipaumbele ili wakulima wengi waingie kwenye sekta hio ya kilimo cha umwagiliaji.
Nne, ahadi za CCM za uchaguzi mkuu 2015 zilikua kuongeza idadi za hekta katika kilimo cha umwagiliaji (Jambo ambalo hawakuweza kufanya, hawakuongeza hata ekari 1 ya kilimo cha umwagiliaji, kwasababu walikua bussy kununua ndege na treni).
Tano, nchi haijaweza kujikwamua kwenye kilimo na haijaweza kuzalisha chakula cha kutosha na chakula cha ziada (Yaani kufikia mahitaji ya chakula kinacho hitajika).
Sita, viongozi wanaangalia matumbo yao, na kukalia upuuzi uliopitiliza kwenye kuliongoza taifa katika sekta ya kilimo.
#WAZIRI WA FEDHA, WAZIRI WA KILIMO & NAIBU WAZIRI WA KILIMO - WAENDE WAO WAKASHIKE MAJEMBE NA WAKALIME HALAFU WALIPE HIZO KODI, NDIO WAJE KUTUPA MREJESHO KAMA KUNA FAIDA WATAPATA HUKO.