Kwani Wakulima waliikosea nini Serikali ya CCM?

Mkuu kwanza heshima kwako umenijibu kwa hekima sana unafaa kuwa kiongozi shukrani kwa busara uliyoinyesha kwa jibu lako
 
CCM OYEEEEEE ... !!! Nchi zote zinazo jitambua kilimo cha umwagiliaji hupata ruzuku ili kuukomaza uti wa mgongo wa taifa hili

Lakini wenzetu wanataka viwanda basi haya toeni ruzuku ya viwanda au ndio tutashia kwenye viwanda vya kushona viatu ... yani CCM ni chama cha kizamani sana ase!
 
Waziri wa pesa ni mwigulu unategemea nini hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Hii wizara ilitakiwa apewe mtaalam aliyebobea kwenye masuala ya uchumi kama ilivyokuwa kwa Philipo Mpango! Ila siyo Mwigulu Nchemba mzee wa TOZO!

Huyu angepelekwa Wizara ya Muungano na mazingira akapige porojo na mwenzake Jaffo.
 
Hivi jpm ni nani nchi ifuate aliyokuwa anataka yeye jpm alifanya yake mwacheni mama afanye jpm jpm mnatuchosha na jpm wenu huyo si mmufuate huko aliko.
Huu ndo upumbavu kuleta ushabiki hata kwenye Mambo yenye maslahi kwa taifa kwaio Kama budget imembana mkulima watu wasiseme wamwache wakati wanaumia angekua nchi ni Mali yake angeachwa afanye anavyotaka.hata uyo jpm alikua anaambiwa hapa JF akienda sivyo.
 
Huyo jpm wako alikuwa na muda kukusikiliza acha upumbavu na jpm wako
 
Budget hii ya Waziri Wa Fedha imeweka dhahiri kwamba:

1) Dk Mwigulu haiwezi hio Wizara, na anageuka kuwa mzigo kwenye serikali ya SSH.

2) Waziri Wa Kilimo na Naibu Waziri wake sasa ni maadui wakubwa wa wakulima nchini.

Moja, huwezi kuruhusu upumbavu huu kufanyika kwenye wizara yako ya kilimo wakati wakulima bado hawajajiweza wala hawajaingia kwenye kilimo cha kisasa.

Pili, wakulima hawana mtaji na hawana masoko ya mazao yao wanayolima.

Tatu, swala la kilimo cha umwagiliaji kwanza lingepewa kipaumbele ili wakulima wengi waingie kwenye sekta hio ya kilimo cha umwagiliaji.

Nne, ahadi za CCM za uchaguzi mkuu 2015 zilikua kuongeza idadi za hekta katika kilimo cha umwagiliaji (Jambo ambalo hawakuweza kufanya, hawakuongeza hata ekari 1 ya kilimo cha umwagiliaji, kwasababu walikua bussy kununua ndege na treni).

Tano, nchi haijaweza kujikwamua kwenye kilimo na haijaweza kuzalisha chakula cha kutosha na chakula cha ziada (Yaani kufikia mahitaji ya chakula kinacho hitajika).

Sita, viongozi wanaangalia matumbo yao, na kukalia upuuzi uliopitiliza kwenye kuliongoza taifa katika sekta ya kilimo.

#WAZIRI WA FEDHA, WAZIRI WA KILIMO & NAIBU WAZIRI WA KILIMO - WAENDE WAO WAKASHIKE MAJEMBE NA WAKALIME HALAFU WALIPE HIZO KODI, NDIO WAJE KUTUPA MREJESHO KAMA KUNA FAIDA WATAPATA HUKO.
 
Kwa hili la umwagiliaji mama amekwenda kinyume na dhamira ya jpm ya kuinua kilimo cha umwagiliaji
Rais anaongoza kwa dhamira yake mwenyewe haongozi wala kushawishika kuongoza kwa dhamira ya marehemu.

Acheni ujinga wenu
 
CCM ilipotwaliwa na matajiri jumla kutoka kwa wakulima kupitia mabadiliko ya katiba.
Vijana nendeni mkazurure mjini mkichuuza 'made in China', kilimo kimeonekana kama kazi ya laana.
Hata viongozi wakiwa majukwaani hujitapata kuwatetea bodaboda, machinga na mama ntilie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…