Kwanini 90% ya Mabao ya Mbwana Samatta ni Tap-Ins.?

Hizo Tap Ins zingekuwa rahisi hivyo mbona Sanchez angefunga nyingi tu kwa jinsi wanavyomnanga.
 
Kuna mtu anaitwa Javier Hernandez chicharito.... From Mexico to Man United.. Angalia magoli ya chicharito, chunguza ya vanestariooy then mwangalie pippo inzaghi... Hata Yule Gabriel Jesus japo kwasasa hayupo kweny kiwango bora... Then utamwelewa samatta....
 

Umeshasema mwenyewe kuwa Mbwana samata ana vitu viwili ambaqvyo ni instincts na finishing...sasa hivyo ndivyo vinavyomsaidia awe nyota...ana uwezo wa kutambua kuwa muda na wakati fulani akae mahali fulani...anausoma mpira unavyokwenda na wachezaji walivyokaa uwanjani na kumfanya akae mahali sahihi na wakatisahihi wa kufunga bao...ni wachezaji wachache duniani wenye vipaji hivi...mchezaji mwingine anayefanana na Mbwana Samata ni Romario aliyekuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Brazil na pia Barcelona miaka ya mwanzoni mwa 1990...Romario alikuwa hana chenga yeye kazi yake ilikuwa ni kufunga tu..alikuwa anakaa mahali sahihi na wakatisahihi na kufanya tapping za mipira kuwa magoli...Hata Bebeto pia wa Brazil alikuwa wakati mwingine ni bingwa wa tapping na finishing..
 
Hebu mfuatilie Sammata wakati akiwa mazembe, mbona alikua ana dribble na kupunguza mabeki kwa sana, inawezekana Genk anafata maelekezo ya kocha wake na style ya kiuchezaji ya Timu.
 
Mkuu Ruud Van Nistelrooy alikua mshambuaji wa aina gani?Chicharito?John Dahl Thomason? Ukipata majibu ya haya jiulize na wao ni wazee wa tap in goals or what??

Usiwafananishe ma legend na chokochoko. Samatta siku zake za ulaya zinahesabika.
 
Kwani Nelsteroy alikiwaje
 
Mbwana ayafoka tu tisiwe na haraka ni mtu makini sana sina waswas nae
 
Mkuu Hizo tap in ndio muhimu kwenye mpira time ipate magoli na points, www tap in hapa JF Samatta ata-tap in atapoenda sajiliwa. Mpongeze bana hata kidogo
 
Quote of The Day:

"Nknachokiona ni kwamba Mbwana Samatta
ataishia kucheza soka Genk pekee na mwisho
wa siku kustaafu soka akiwa pale pale."

by Demigod.
 
Kwanza ningetamani kujua asili ya Uraia wako,

Pili natamani kujua umri wako,

Tatu jitahidi uwe na uwezo wa kuchambu mchezo wa soka bila kufungwa na mapenzi binfsi au chuki binafsi,

ASANTE
 
Hivi L.Suarez huwa anapunguza mabeki kweli?
Mkuu huyo mtu hakunaga kabisa asee kwa kupiga vyenga vya ajabu na matobo.

Enzi akiwa Ajax na Liverpool kutokana na mifumo kuwa tofauti na Barca huyo jamaa alikuwa noma kwa kuchukua mabeki na chenga zake zisizoeleweka unaweza kudhani anaanguka kumbe ashapita mtu.

Suarez wa Liverpool alikua complete striker asee. Vyenga, anakaba ana nguvu na magoli ya aina zote unayoyataka.

 
Wee huijui kesho yake Samata, na pia Samata atabakia kuwa mtanzania pekee aliyefanikiwa kwenye soko kwa sasa
 
Dah, kuna mengi ya kuchambua hapa, katika hoja yako ya kum-crash Samatta na uwezo wake katika ufungaji.

A striker's role is to score goals, that's why he's called a striker. Philipo Inzagi alikuwa "poacher", hakuwa tofauti sana na Mbwana, lakini he was one of the best strikers on the world during his time.

Hata hivyo, kocha anatoa maelekezo ni jinsi gani anataka watu wake wacheze, kuna Giroud, Lukaku type of strikers, wao wanachojua ni ku-hold up play, kuruhusu wingbacks kuja mbele, ila hawajui hata kupiga chenga, and they're fine atrikers.

Wapo pure finishers, just finishers kama enzi za kina Van Nesterloy, wale ni wamaliziaji tu, hawakuwa na mbwembwe, lakini kuna wale type ya Bergkamp, Hazard, Aguero, they have talents, they can dribble, dink, shoot, head etc.

Kocha anamtumia strikerkutokana na uwezo wake, aina ya mchezo wanaocheza na opponent anayekutana nae.

Simple, Samatta is a good striker.
 
Duh! Muwe mnakuja kwenye Nyuzi zenu basi angalau Kukanusha kuwa mlinukuliwa vibaya!
Kijana anazidi kuwaumbua...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…