Kwanini 90% ya Mabao ya Mbwana Samatta ni Tap-Ins.?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Nimekuwa nikijiuliza kwanini Mbwana Samatta ameganda pale pale Genk KRC pasi na kusonga mbele.?

Wamekuja wakina Bailey wamesepa..

Wamekuwa wakina Ndidi wamesepa...

Kwani uwezo wake unatia shaka wazungu?

Nilichogundua ni kwamba uwezo wa Samatta ni wa Ligi ndogo ndogo sana barani Ulaya.

Ukizingatia matakwa makubwa sana ya Mshambulizi kwenye soka ni kuwa na uwezo wa ziada na si kufunga mabao tu.. Mbwana amekosa mambo kadhaa ya kiufundi ambayo anatakiwa awe nayo mshambuliaji ili aweze kukidhi kumudu nafasi za juu kwenye klabu zitokazo kwenye ligi kubwa barani Ulaya.

Samatta kama Mshambuliaji amepewa vitu 2 na Mwenyezi Mungu.

1. Insticts (Inayozaa Anticipation)
2. Finishing.

Vitu ambavyo havitoshi kabisa kuhimili mikiki mikiki ya Wakubwa wa Bara la Ulaya.

Nimefualia karibia 90% ya mabao afungayo akiwa Genk ni Tap - Ins.
Kwa wasio elewa maana ya Tap-ins ni ile mipira inayokufikia miguuni au kichwani na kuikwamisha nyavuni mara mona pasi na kuipooza.

Ni nadra sana kuona Mbwana akifunga bao baada ya kupunguza walizi waliwi au watatu.

Kitu ambacho mshambuliaji aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa namna hiyo pia.

Kama akikutana na defence mechanism ambayo inafanya Man to Man marking jamaa anakuwaga anatoa jasho tu kama bomba wa maji ya Dawasco lililo toboka.

Nknachokiona ni kwamba Mbwana Samatta ataishia kucheza soka Genk pekee na mwisho wa siku kustaafu soka akiwa pale pale.

Samatta wetu ni wakawaida sana.
IMG_20180911_165535.jpg
 
Mtanzania katika ubora wake, anyway uzuri tunajijua tulivyo. Mungu anisaidie nisiwe na mawazo kama haya uliyo yaandika. Kwenye mpira what count ni Goli sio mark-up. Mbwana ni striker, kazi yake ni kufunga tu mkuu, ili mradi anafunga basi hakuna shida.
 
Yapo magoli ambayo samatta anafunga akiwa amepunguza beki au ana drible umbali mrefu....je unawajua mastriker wanaoitwa fox in the box ambao wanatafutwa ulaya sahivi kwani toka wastaafu wakina Philip inzaghi na Rud van, siku hizi hawapo hao.
 
Nimekuwa nikijiuliza kwanini Mbwana Samatta ameganda pale pale Genk KRC pasi na kusonga mbele.?

Wamekuja wakina Bailey wamesepa..

Wamekuwa wakina Ndidi wamesepa...

Kwani uwezo wake unatia shaka wazungu?

Nilichogundua ni kwamba uwezo wa Samatta ni wa Ligi ndogo ndogo sana barani Ulaya.

Ukizingatia matakwa makubwa sana ya Mshambulizi kwenye soka ni kuwa na uwezo wa ziada na si kufunga mabao tu.. Mbwana amekosa mambo kadhaa ya kiufundi ambayo anatakiwa awe nayo mshambuliaji ili aweze kukidhi kumudu nafasi za juu kwenye klabu zitokazo kwenye ligi kubwa barani Ulaya.

Samatta kama Mshambuliaji amepewa vitu 2 na Mwenyezi Mungu.

1. Insticts (Inayozaa Anticipation)
2. Finishing.

Vitu ambavyo havitoshi kabisa kuhimili mikiki mikiki ya Wakubwa wa Bara la Ulaya.

Nimefualia karibia 90% ya mabao afungayo akiwa Genk ni Tap - Ins.
Kwa wasio elewa maana ya Tap-ins ni ile mipira inayokufikia miguuni au kichwani na kuikwamisha nyavuni mara mona pasi na kuipooza.

Ni nadra sana kuona Mbwana akifunga bao baada ya kupunguza walizi waliwi au watatu.

Kitu ambacho mshambuliaji aliye kamilika anatakiwa awe na uwezo wa namna hiyo pia.

Kama akikutana na defence mechanism ambayo inafanya Man to Man marking jamaa anakuwaga anatoa jasho tu kama bomba wa maji ya Dawasco lililo toboka.

Nknachokiona ni kwamba Mbwana Samatta ataishia kucheza soka Genk pekee na mwisho wa siku kustaafu soka akiwa pale pale.

Samatta wetu ni wakawaida sana.View attachment 881959
Mkuu Ruud Van Nistelrooy alikua mshambuaji wa aina gani?Chicharito?John Dahl Thomason? Ukipata majibu ya haya jiulize na wao ni wazee wa tap in goals or what??
 
Mbona hata wengine ndivyo walivyo?
1. Giroud anafunga mara nyingi kwa vichwa tu?
2. Diego Costa mbona hajui hata chenga lakini anafunga sana?

Nafikiri ni suala la muda tu, hata akina S. Mane walianza polepole.
Naye ipo siku yake, maana kwa asili soka letu Tz; hata hapo alipofikia WaTz tunamuona kama Pele wa Tz.

Mtoa mada umeongea ukweli kabisa; lakini utaambiwa una roho mbaya na fitina.

Ova
 
Mkuu Ruud Van Nistelrooy alikua mshambuaji wa aina gani?Chicharito?John Dahl Thomason? Ukipata majibu ya haya jiulize na wao ni wazee wa tap in goals or what??
Yaani nilikua nisome comments zote kisha nimtaje huyu Rud Van ,Mkuu umenisaidia

Halafu Bailey na Ndindi hawa wote ni walikua wanatokea pembeni,pale KRC ,Samata anasimama na Trosad
 
Jamaa nahisi kaandika kwa hisia tu Ila hajaconsider kua duniani Kuna mastriker dizain ya Samatta wameshawahi kutamba Sana tena kwenye club kubwa tu
 
Mtanzania katika ubora wake, anyway uzuri tunajijua tulivyo. Mungu anisaidie nisiwe na mawazo kama haya uliyo yaandika. Kwenye mpira what count ni Goli sio mark-up. Mbwana ni striker, kazi yake ni kufunga tu mkuu, ili mradi anafunga basi hakuna shida.
Huyu jamaa sijui anamskia Oliver Giroud au kipindi kile cha Philipo Inzaghi,chizi kabisa na roho yake mbaya
 
Back
Top Bottom