kwanini Abiria wengi huzuiliwa kubeba Power Bank kwenye Ndege!

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833
Unajua kwanini Abiria wengi huzuiliwa kubeba Power Bank kwenye Ndege!!!

Power bank.png

Mnakumbuka ajali ya Ndege ya Airbus A321 iliyotokea nchini Korea kusini chanzo chake kimebainika sababu kubwa ni Power bank.

Ndege hiyo. ya abiria ya Air Busan ilishika moto katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Gimhae nchini Korea Kusini Januari 28, 2025. Watu watatu walijeruhiwa kidogo.

Wizara ya Uchukuzi ya Korea Kusini ilisema mnamo Machi 14 ilisema kwamba sababu kubwa ilibaini kuwa power bank iliharibika na kusababisha ndege hiyo kushika moto.

Power bank ilikuwa kwenye eneo la kuhifadhia juu ya kiti cha abiria, ambapo moto huo ulizuka kwa mara ya kwanza. Lakini Tika Mwaka 2016 Power bank zilizuiliwa kubebwa kwenye Ndege.

Mashirika ya ndege duniani kote yamepiga marufuku power bank kubebwa kwenye mizigo inayoingia (vitu unavyokabidhi kabla ya kupanda ndege) kwa miaka mingi kwa sababu za kiusalama.

Kwani power bank zina Betri za lithium ioni ambazo zinaongoza kulipuka kutokana na kuzalisha joto kubwa na zinaweza kusababisha mshtuko wa umeme ikiwa kuna kasoro yoyote ndani yake.

Kulingana na ushauri uliotolewa na Shirika la Kimataifa la Usafiri wa Anga, tangu 2016, abiria wamepigwa marufuku kubeba betri zozote za lithiamu-ion kwenye mizigo iliyokaguliwa kwenye ndege.
 
Unajua kwanini Abiria wengi huzuiliwa kubeba Power Bank kwenye Ndege!!!

View attachment 3283092

Ikikaa kwenye checked in bags sio ishu?
 
Back
Top Bottom