Kwanini Abiria wengi wa Mabasi ya Mikoani wakifika maeneo ya Mto Wami na Milima ya Kitonga Nyuso zao huwa ni za Huruma sana?

Tena ukiwa kwenye majinja unabana mpaka.......[emoji43][emoji43][emoji43]
 
Wami kuna lori lilipiga mbizi pale juzi mamba wakafanya yao.

Pale kwa dereva mzoefu wa njia hakuna changamoto sana. Kikubwa ni ku-control speed. Na miguu ya gari iwe vizuri.

Kuna Dereva Mmoja wa Malori ya Congo DR, Malawi na Zambia anasema ukitaka uyapite vyema bila Hofu hayo Maeneo lazima Ulanduke vilivyo.
 
Kimeshanuka wami huko

Inasemekana Siku ya Jana hapo Darajani kulikuwa na FIESTA Maalum ya Mamba Wakazi wa hilo eneo la Mto na Daraja na Walishiba na Kusaza.
 
Title tu nimecheka😀. Adui yetu mkubwa zaidi ni kifo.
 
Maeneo hayo hata simu kama inaingia watu wanazikaushia kama hawazioni utadhani na wao wamekuwa madereva,kila mtu anataka kuangalia mbele,corridor ya katikati huwezi kuona mbele kila mtu katoa kichwa ili aone mbele...
 
Sir nimekuja kuwatia hasira mtafute hela muache kupanda mabasi.

Nina uhakika kama Jamvini Members tungekuwa tuna uwezo wa Kujuana unaweza kukuta wale Wanaojiona Matajiri kumbe ndiyo Masikini sana tu.
 
Wami kwa uzoefu wa macho yangu nimeshuhudia sereka sereka za kila aina.

Nshatembezwa kwa mguu kuanzia darajani mpaka geti la kambi ya jeshi tena usiku usiku.

Ile sehemu jamani ni Mungu tu Ngoja hilo daraja jipya la JPM liishe maisha yaendelee tu na mengine yabaki historia.
 
Nimecheka sana, siai wasafiri kweli tukifika hayo maeneo hata sala zitaombwa, kumkumbuka muumba wako wakati wa hatari tu ni hatari zaidi, unakua kama unaleta matani kwa muumba wako, Jengeni tamaduni za kumuomba Mungu nyakati zote.
 
Kuna maeneo yakuhofia sio Wami.
Kuna mlima Nyang'oro njia ya Iringa-Dodoma, mlima Ndororo njia ya kwenda Mahenge.

Milima na kona za Lukumburu njia ya Songea na njia ya kwenda Mgeta ukitoka Mlali kuna Mlima mkali umewekwa zege.
We kweli msafiri
 
Juzi kuna Lori limezama hapo na inavyosemekana ( sijathibitisha ) ni kwamba Miili ya Dereva na Utingo imeshaishia ndani ya Midomo ya Mamba.
Hivi mamba pale wami wanafanta nini au nikivutio, watolewe pale haraka
 
Kuna Dereva Mmoja wa Malori ya Congo DR, Malawi na Zambia anasema ukitaka uyapite vyema bila Hofu hayo Maeneo lazima Ulanduke vilivyo.
Ulanduke ni kuongeza speed ama kuchizika? Na wewe umeamini, mwambie akawadanganye nursery
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…