Kwanini abiria wenzangu wa daladala hamsogei nyuma mnapopanda?

Kwanini abiria wenzangu wa daladala hamsogei nyuma mnapopanda?

Ww ni konda nini? 😜 mda mwengine hatupendi kusogea nyuma especially km unashuka kituo cha karibu coz ukichelewa kufika mlangon unashtukia dereva kashaondoa gari..... Baadhi ya Konda na Dereva hawana subra wanahisi km unawachelewesha kupakia abiria wengine.
 
Nyuma raha yake iwe safari ndefu. Sio unapanda Morocco kwenye Ile migari mirefu ya mbagala ukashukie Manyanya wallah utajuta kukaa nyuma

Sent using Jamii Forums mobile app


Na sio daladala tu, hata mwendokasi pia km unashuka njiani na upo mbali na mlango utajuta kupanda 😂😂 ndomana watu wanaganda mlangoni lol
 
Wengine huwa tunapenda kukaa nyuma kabsaa maana kuna
mimtu inapenda kuchungulia simu za
wenzao wakati wanachati.

Ila Wanaokaa dilishani wanakela sana yaani
wanafunga vioo wakati gari limejaa..umwambie
sasa afungue kiooo aiseee kitachokukuta.
 
Nayapenda magari ya mbagala
Dereva anajua kuchekecha na breki za ghafla mtasogea tu nyuma

Wakiingia kundi la akina Chau wanasukuma mpaka mnakaa vizuri
 
Back
Top Bottom