Kwanini adhabu kwa vyombo vya habari iwe kufungiwa badala ya kulipa faini?

Kwanini adhabu kwa vyombo vya habari iwe kufungiwa badala ya kulipa faini?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kuna usummbufu mkubwa na hasara kubwa sana kwa vyombo vya habari na hata kwa Kodi ya serikali Kama chombo Cha habari (redio, tv, gazeti) kitafungiwa japo kwa wiki moja tu.

Kwanini makosa yanayosababisha kituo kufungiwa kwa wiki moja isiwe kulipa hela badala ya kukifungia?.

Kufungia chombo kunasababisha usumbufu kwa watu wasiohusika Kama vile matangazo ya biashara, wasikilizaji na wafanyakazi wanaoishi kwa kutafuta habari kila siku.

Kodi ya serikali pia inapotea kutoka kwenye Makato ya Mapato mbalimbali yakiyositishwa kutokana na kusimamishwa kwa chombo Cha habari.
 
Tatizo la kuweka kwenye position watu wasiojua husstle ni nini, mijitu imekaa tu ofisin haijui maisha ya ujasiliamali yakoje. Tutashuhudia maumiv sana sekta binafsi awamu hii
 
Back
Top Bottom