Kwanini adhabu ya kifo(capital punishment) haitakiwi kufutwa

Kwanini adhabu ya kifo(capital punishment) haitakiwi kufutwa

Kassim Rashid

Member
Joined
Mar 19, 2016
Posts
50
Reaction score
29
Ni mda mrefu kidogo tangu hoja mbalimbali zilianza kutolewa na watu hususani wanaharakati wa haki za binaadam(human and peoples rights activists) na wanasheria mbalimbali(lawyers social group) kuwa adhabu ya kifo dhidi ya mtuhumiwa aliefanya kosa la kuuwa mtu mwingine kwa makusudi(murder) chini ya kifungu cha Sheria ya Kanuni za Adhabu sura ya 16 kifungu cha 196 inatakiwa kufutwa(being repealed) kwa kuwa inakinzana na misingi ya haki za binadam hususan misingi ya ibara ya 14 ya Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977(kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara) kuwa kila mtu anahaki ya kuishi na haki ya kupata ulinzi wa maisha yake kwa jamii, vile vile hoja hizi zimeegemea(base on) katika ibara ya 13(6)(e) ya katiba hii hii kuwa ni marufuku kwa mtu yoyote kumtesa mtu au kumtenza utu wake,na kwa mara ya kwanza kwa Tanzania katika kesi ya Jamhuri dhidi Mbushuu Dominic Mnyaroje(1983) mahakama iliamua katika rufaa ya kesi hiyo kuwa adhabu ya kifo ni kinyume na katiba hii ya 1977.Na utakaposoma Tanzania Human Rights Report(2013) utaona hoja kubwa iliyojengwa kuwa adhabu ya kifo haina manufaa kwa kuwa watu bado wanatenda kosa hilo la kuuww kwa makusudi licha ya kuwepo kwa adhabu ya kifo. Hivyo kasoro ya kwanza wanasheria wengi na wanaharakati wa haki za binaadam wanafanya ni kuwa wanatafsiri ibara ya 14 kwa kumlinda upande wa mtuhumiwa wa kosa la kuuwa yaani kumpa adhabu ya kifo ni kinyime na katiba na ni sawa na kutenza na kumtesa mtu na utu wake,lakini hawatafsiri kuwa mtu alieuwawa naye utu wake umetenzwa na ameteswa(he suffer the pains which cannot be measured by any standard), vile vile hawakumbuki wala kutoa hoja kuwa maisha ya marehem yaliyochukuliwa yatalipwa kwa kiwango kipi kiasi ambacho sheria itakuwa imempa adhabu stahiki kwa kosa la kuuwa(retaliation).Hivyo hoja yangu kubwa hapa ni kuwa kila mtu anatafsiri ibara ya 14 na 13(6)(d)(e) kwa ulewa wake na je misingi ipi inatumika kutafsira katiba?.Hoja nyingine ni kuwa watafiti wa haki za binaadam Tanzania na maanisha Kituo cha Sheria navHaki za Binaadam(Human and Legal Right Center) katika kitabu chao cha Tanzania Human Rights Repott(2013) wanadai kuwa adhabu ya kifo haina manufaa kwa kuwa tu watu bado wanatenda kosa hilo licha ya kuwa na sheria inayokataza vikali kosa hilo hivyo haitishii wala kuzuia(it is neithert hreat nor preventive) sasa hii ni hoja isiyo na msingi kwa sababu kutokuogopeka wala kutotishia watu kufanya kosa hilo kusipelekee kufutwa kwa adhabu hiyo kwani kawaida ya watu ni kufanya makosa haijalishi utaweka adhabu ya namna gani,hivyo adhabu hiyo lazima iwepo haijalishi watu hawaogopi atakaekutwa na hatia ya kuuwa kwa makusudi lazima anyongwe tu kwa kumtenza mtu mwingine na kumpa maumivu makali ambayo huwezi ukayapima kwa kiwango cha aina yoyote( you cannot measure by any standard), vile vile serikali inatakiwa kuboresha idara ya upelelezi wa makosa ya jinai hususani ya kuuwa.
 
Back
Top Bottom