Kwanini Afrika Kusini inataka Marekani iwekewe vikwazo?

Kwanini Afrika Kusini inataka Marekani iwekewe vikwazo?

Stunnaman008

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2022
Posts
238
Reaction score
272
Rais wa Marekani ambaye hivi karibuni alikutana na Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel, anajaribu kuchukua hatua za kuilinda Israel na kuzilazimisha nchi zingine zifuate sera za Washington na hivyo kuwa pamoja na Israel.

Ni kwa kuzingatia ukweli huo ndio maana ametumia sera za Afrika Kusini kama kisingizio cha kuweka mashinikizo kwa nchi hiyo na kuitishia nchi hiyo kuikatia misaada ili iachane na siasa zilizo dhidi ya Israel.

Ukweli wa mambo ni kuwa, Trump anajaribu kuilazimisha Afrika Kusini, ambayo ni miongoni mwa wanachama muhimu wa kundi la BRICS na Mwenyekiti wa Zamu wa kundi la 20, kutii sera zake inazotaka katika uga wa kisiasa, hususan kukomesha uadui dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Lakini msimamo thabiti wa viongozi wa Afrika Kusini kuhusu hatua ya uhasama ya Trump ya kukata misaada ya kifedha ya kupambana na UKIMWI, ambayo si ya kibinadamu unaonyesha kwamba, Pretoria imeazimia kwa moyo imara kupinga ubabe na sera za kibeberu za Washington
 
Back
Top Bottom