kasimba123
JF-Expert Member
- Apr 18, 2010
- 1,753
- 816
Sasa ndicho simba itakifanya kwa Banda kumboresha kwahiyo ondoa wasiwasi atakuwa tu kama miqkavulata said:
hakuwa mzuri kama sasa hivi, simba ilimboresha
Nyie huko Morocco mtarudi na mimba tu Mwarabu kawalipia kila kitu siyo mchezoLuis ni mwanaume hiki kibwabwa akiwezi ile mikwanja aliyokua anapigwa luis,ligi yetu ina mabeki wakatili sana,kiukweli mikia msubiri maumivu tu,konde mmepoteza mtu pale
View attachment 1891404
Mbona Utopolo ndiyo mnalakamikia kuondoka kwao inawahusu nini?Miquissone na Chama kuondoka kwa wakati mmoja sio jambo dogo. Zaidi ya robo tatu kama sio theluthi mbili ya magoli ya Simba yamechangiwa na hawa wanaume 2
lazima ziuzwe ziletwe nyingineMpira ni biashara, na wachezaji ndo bidhaa zenyewe
Kocha aliyeko Al Ahly leo Pitso Mosimane ndiyo huyo huyo alikuwa Kocha wa Mamelodi Sundowns ambayo Luis Miquissone alitokea hivyo ni Mtu ambaye anamjua na kaona ameimarika zaidi na Kumuhitaji aliko sasa Al Ahly tofauti na Peter Banda ambaye hakumfahamu vyema au labda anamfahamu ila kwa Ushindani wa Al Ahly hatoweza lakini pengine kwa Kiwango cha Simba SC atafanikiwa.Kwa vyovyote vile kuondoka kwa Moquissone na Chama kumeiumiza Simba, no doubt.
Miquissone alikuwepo na Banda alikuwepo lakini mmoja kaenda Al-Ahly na mwingine kaja Simba. Tusidanganyane, Banda sio Miquissone hata kwa robo. Tukaze buti
Mbona Man U wanamkatalia Pogba kuhama, spurs wanamkatalia Harry kuondoka? SEMA TU Mwamed wenu anataka kupiga helaSimba haina historia ya kumzuia mchezaji atakiwapo na timu nyingine.
Yanga msitake kutupa tabia yenu ya roho mbaya ya kuzuia mafanikio ya mchezaji maana ninyi ndio wenye historia hiyo
Anaweza kuboreka hapa au asiboreke kumfikia Miquissone. Miquissone kaja na ubora wake kwakuwa alishafika Mamelod tayari. Huyu Banda hata Mamelod ajafika huwezi kumfanisha na miquissone. Banda ni kama Waziri junior wa Malawi. Waziri kaja Yanga na rekodi ya ufungaji bora lakini hakuborekaKwani kipindi Simba haijamchukua Luiz Al Ahly walikuwa wapi?
Sasa ndicho simba itakifanya kwa Banda kumboresha kwahiyo ondoa wasiwasi atakuwa tu kama miq
-Thread imefungwa hapa!
Hata wanasimba wanafahamu kuwa kuwapoteza miquissone na Chama kwa wakati mmoja ni pigo, wanajifaragua TU.Ni muda tu ulifika wa Chama na Konde Boy kuondoka kwani viwango vyao vilikuwa juu sana na walipata ofa kubwa sana kuzidi uwezo wa Simba kifedha. Na sikuona namna ambavyo Simba wangeweza kuzia wasiondoke. Na Konde Boy na Chama ni wachezaji wa kimataifa na mawakala wao nao ni wa kimataifa kwa vyovyote vile mikataba yao japo sijaiona lakini naamini lazima ilikuwa na kipengele cha kuondoka mara tu wapatapo ofa kubwa. Tuwe wakweli tu mtu mzima yoyote yule anapoamua kuondoka mahali iwe ni kwenye ndoa, kazini, mchezaji, mlinzi, hata "house girl" huwezi kumzuia na ikitokea umemzuia kwa nguvu abaki kila mtu anajua madhara yake. Japo Simba walikuwa na uwezo wa kuwalazimisha wamalizie mikataba yao lakini mwishoni wangeondoka bure kabisa. Pia wangeweza kucheza chini ya kiwango na kuigharimu timu na mbaya zaidi wachezaji wenye vipaji vikubwa na malengo ya baadaye wasigekubali kusajiliwa Simba wakijuwa kuwa watabaniwa wakipata ofa kubwa.
Watu wanoujua mpira kwa undani wanajua kabisa kuna Konde Boy mmoja tu na kuna Chama mmoja tu kwahiyo nashangaa sana watu wanapoanza kuwalinganisha na wakina Banda. Hiyo katu haiwezekani kwani mburudishaji kama Chama anatokea baada ya miaka kadhaa. Ile "work rate" ya Konde Boy sijui unaipatia wapi kwa siku za karibuni. Ni raha sana kuwatazama hao wachezaji wawili jinsi wanavyouamrisha mpira ufanye watakavyo lakini sasa watakosekana hiyo lazima kila mpenda mpira alikubali. Kwangu mimi binafsi kidogo naweza kumlinganisha Chama kiuchezaji na watu wawili mafundi Hamisi Gaga "Gagarino" na Said Mwamba "Kizota" japo uchezaji wao bado haulingani kwa asilimia 100%.
Kwa hiyo hao wakina Banda waachwe waje waonyeshe vipaji vyao ikiwezekana na wao waweke alama zao kivyao kwani Mungu amemjalia kila mmoja kipaji cha aina yake. Lakini kitendo cha kuwalinganisha ni "big no". Inaweza kutokea japo si rahisi kati ya hawa wachezaji wapya wakawa sawa na Chama au Konde Boy au hata kuwa zaidi yao lakini hiyo ni bahati nasibu na nadra sana kuwa hivyo kwa siku za karibuni. Na duniani kote ipo hivyo kwa mfano mchezaji gani leo tunaweza sema ni sawa na Ronaldino Gaucho, au Messi au Ronaldo. Lakini wakina Mbappe, si wanakuja na staili zao na tunaanza kunawakubali kivyao vyao.