Kwanini alaumiwe tip tip kwa kununuwa watumwa lakini wasilaumiwe machifu kwa kuwauza watu wao

Bin Faza

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2013
Posts
502
Reaction score
191
Waungwana katika JF

Kila siku kila sehemu katika lalamiko kubwa tunazozisikia ni biashara ya utumwa

lawama kem kem zinamuangukia Bwa Mohammed Murjib au kwa umaarufu wake Tip Tip kama ndie aliendesha biashara ya utumwa huko tanganyika.

Biashara maana yake ni kununuwa na kuuza.

Lawama zote zinamuangukia Tip Tip kwa kununuwa watumwa lakini sijawahi kusikia hata mtanganyika mmoja akiwalaumu MACHIFU wa kabila zao kwa kuwauza raia au watu wao kwa TIP TIP na WaZUNGU.

naomba pasiletwe hoja kwamba tip tip alikwenda na bunduki na akawazunguka watanganyika elfu na kuwachukuwa akawatia michororo ya miguu na mikono na kuwawekea magogo mabegani na kuwapelekwa znz kuwauza.....hii haiwezi ku add up kwasabau na wao walikuwa nayo mikuki na mishale siku hizo

Lazima itakuwa kulikuwa na ushirikiano baina ya tip tip na machifu, mashirikiano ya kibiashara

Nguruvi3 na washabiki wenzako sisemi hivi kuthibitisha kwamba ninafurahiya biashara hiyo, no. mimi ninaulaani kwa level ya juu kabisa

lakini nakusudia kusema kwanini sisi katika generation hii, watu tulisoma na kutembea lakini wenye matatizo mengi kiasai ambacho tukimbebesha tembo anaweza kuanguka........tuwache kushuhulishwa na matatizo yetu na tukerwe na matukio ya 1800s

Ahsanteni
 
tukishakerwa na kukemea kifuatacho kitakua ni nini?

Pamoja na kuwa matukio yaliyopita yanamfanya binadamu mwenye upeo mzuri kutengeneza na kuipanga kesho, bado binadamu huyo haishi kwa matukio yaliyopita.....
 
mkuu wewe naona hiyo biashara ya utumwa either umesimuliwa kipindi uko oman or umeangalia documentary flani. ninachokuomba hebu tafuta vile vitabu vya history vya zaman co hivi vya .com nyangwine..... ukisoma uelewe vizuri njoo andika upya huu uzi maana hapo ulichokiandika hukielewi.
 
Tip Tip au Mohamef Murjib hastahili lawama kwa biashara ya watumwa aliyofanya kwa sababu dini aliyokuwa akiiamini inaruhusu utumwa.
 
Waungwana katika JF

Kila siku kila sehemu katika lalamiko kubwa tunazozisikia ni biashara ya utumwa

lawama kem kem zinamuangukia Bwa Mohammed Murjib au kwa umaarufu wake Tip Tip kama ndie aliendesha biashara ya utumwa huko tanganyika.

Biashara maana yake ni kununuwa na kuuza.

Lawama zote zinamuangukia Tip Tip kwa kununuwa watumwa lakini sijawahi kusikia hata mtanganyika mmoja akiwalaumu MACHIFU wa kabila zao kwa kuwauza raia au watu wao kwa TIP TIP na WaZUNGU.

naomba pasiletwe hoja kwamba tip tip alikwenda na bunduki na akawazunguka watanganyika elfu na kuwachukuwa akawatia michororo ya miguu na mikono na kuwawekea magogo mabegani na kuwapelekwa znz kuwauza.....hii haiwezi ku add up kwasabau na wao walikuwa nayo mikuki na mishale siku hizo

Lazima itakuwa kulikuwa na ushirikiano baina ya tip tip na machifu, mashirikiano ya kibiashara

Nguruvi3 na washabiki wenzako sisemi hivi kuthibitisha kwamba ninafurahiya biashara hiyo, no. mimi ninaulaani kwa level ya juu kabisa

lakini nakusudia kusema kwanini sisi katika generation hii, watu tulisoma na kutembea lakini wenye matatizo mengi kiasai ambacho tukimbebesha tembo anaweza kuanguka........tuwache kushuhulishwa na matatizo yetu na tukerwe na matukio ya 1800s

Ahsanteni

a) Kwanini anafungwa miaka 30 baba aliefanya mapenzi na mtoto wakike wa miaka kumi na mbili badala ya kufungwa mtoto huyu aliyefanya kwa hiari yake?

b) Mkuu una asiri ya kiarabu nini mbona hoja yako ipo kiutetezi kwa mkosaji?

Unafahamu wengi waliouzwa walikuwa mateka wa kivita? na kwamba ilikuwa kudhoofisha kwa kukosa elimu na ufahamu?
 
Huyu jamaa sasa ndio nimeanza kuamini ule uzi alioleta mdau mmoja hapa akionyesha wasiwasi na uraia wake.we ni mwarabu mkuu na hapa unajaribu kujustfy unyama waliokuwa wakiufanya.sorry am not among wale wachovu wachache uliowakamata.
 
Remote

Unachotaka kuleta hapa Uislamu

Usisahau na mimi neno UISLAMU ninalijua na nadhani unajuwa wazi kwamba siogopi kulitumia ikipaswa kufanya hivo

nilolisema ni hilo hilo ambalo limekuwa likikaririwa day in day out hata muhu jukwaani
 
chicco

Huyu jamaa sasa ndio nimeanza kuamini ule uzi alioleta mdau mmoja hapa akionyesha wasiwasi na uraia wake.we ni mwarabu mkuu na hapa unajaribu kujustfy unyama waliokuwa wakiufanya.sorry am not among wale wachovu wachache uliowakamata.

sikushangai kwa hilo kwasababu nyinyi huko tanganyika munayo tabia ya kutuita sisi wazanzbari...waraabu
 
Ehud

Tip Tip au Mohamef Murjib hastahili lawama kwa biashara ya watumwa aliyofanya kwa sababu dini aliyokuwa akiiamini inaruhusu utumwa.

ikiwa unasema ukweli lete uthibitisho wako
 
option

mkuu wewe naona hiyo biashara ya utumwa either umesimuliwa kipindi uko oman or umeangalia documentary flani. ninachokuomba hebu tafuta vile vitabu vya history vya zaman co hivi vya .com nyangwine..... ukisoma uelewe vizuri njoo andika upya huu uzi maana hapo ulichokiandika hukielewi.

kosa lipo wapi katika yaho niloandika.

hsitory inaonesha kwamba machifu ndio walokuwa wakiwauza watu wao kwa wazungu na hata kwa waarbu au tuseme kwa wafanyabiashara ya utumwa.......hili soi east africa tu hata huko nwest afrika ilikuwa same deal
 
Bin Faza nakubariana na approach yako ya kuangalia namna hii biashara ilivyoenenda.lakini naomba maelezo yako ya ziada katika maeneo yafuatayo.

Biashara
Kwamba katika biashara lazima awepo muuzaji na mnunuzi,hivyo ni lazima tip tip aliuziwa hao watumwa.

Lakini vipi juu ya uwezekano kwamba,ushenzi huu uliitwa ni biashara kwa sababu tip tip ndio alienda kuwauza binaadamu wenzake huko alikowapeleka na sio lazima kwamba hata yeye aliuziwa huku kwetu?

Mishale na bunduki.
Hivi ni sahihi kulinganisha silaha hizi mbili? Alafu inaonekana ni kama vile unachukulia tip tip alikuja yeye mwenyewe na bunduki yake,ni sawa? Tip tip hakuja na jeshi la kukamata watu? Ama sivyo hata hao machief waliwakamata vipi au watu wakati wao walitumia mishale tu na tunaambiwa watu waliokamatwa walikuwa mipande ya watu achilia mbali wazoofu wa sasa wazanzibar wanaoshindia urojo.
 
Waungwana katika JF

Kila siku kila sehemu katika lalamiko kubwa tunazozisikia ni biashara ya utumwa

lawama kem kem zinamuangukia Bwa Mohammed Murjib au kwa umaarufu wake Tip Tip kama ndie aliendesha biashara ya utumwa huko tanganyika.

Biashara maana yake ni kununuwa na kuuza.

Lawama zote zinamuangukia Tip Tip kwa kununuwa watumwa lakini sijawahi kusikia hata mtanganyika mmoja akiwalaumu MACHIFU wa kabila zao kwa kuwauza raia au watu wao kwa TIP TIP na WaZUNGU.

naomba pasiletwe hoja kwamba tip tip alikwenda na bunduki na akawazunguka watanganyika elfu na kuwachukuwa akawatia michororo ya miguu na mikono na kuwawekea magogo mabegani na kuwapelekwa znz kuwauza.....hii haiwezi ku add up kwasabau na wao walikuwa nayo mikuki na mishale siku hizo

Lazima itakuwa kulikuwa na ushirikiano baina ya tip tip na machifu, mashirikiano ya kibiashara

Nguruvi3 na washabiki wenzako sisemi hivi kuthibitisha kwamba ninafurahiya biashara hiyo, no. mimi ninaulaani kwa level ya juu kabisa

lakini nakusudia kusema kwanini sisi katika generation hii, watu tulisoma na kutembea lakini wenye matatizo mengi kiasai ambacho tukimbebesha tembo anaweza kuanguka........tuwache kushuhulishwa na matatizo yetu na tukerwe na matukio ya 1800s

Ahsanteni

Kwa mfano nikikutana na wewe usiku wa manane mimi nina SMG full magazine wakati wewe hauna silaha yeyote, halafu nikakupigia magoti nikakwambia bin faza nipo chini ya miguu yako naomba niuzie viatu vyako(labda vya laki) kwa shilingi kumi, na wewe kweli ukavivua na kuniuzia. Je mimi nitajisifia kuwa sina makosa kwa sababu umekubali nilikuomba uniuzie viatu vyako ukakubali kwa hiari yako?
 
option

kosa lipo wapi katika yaho niloandika.

hsitory inaonesha kwamba machifu ndio walokuwa wakiwauza watu wao kwa wazungu na hata kwa waarbu au tuseme kwa wafanyabiashara ya utumwa.......hili soi east africa tu hata huko nwest afrika ilikuwa same deal

Bin Faza
Ni wakati muafaka wa kutafakari yale tunayoambiwa kuhusu historia yetu,kwa namna unavyoelezea hili swala ni kama vile kama machief wangekataa kuwauza watu wao kwa waarabu na wazungu basi hao jamaa wangeona biashara imekuwa ngumu na kuondoka zao.

Kwa namna yoyote ile hakuna chief aliuza watu wake katika misingi ya biashara ya maridhiano popote pale duniani.

Style hii ya kuielezea historia ni lazima ipingane na sababu zozote zile za mapigano kati ya machief na waarabu ama wazungu.

Hata ukisema kwamba machief waliopigana na waarabu au wazungu walifanya hivyo baada ya kuona himaya zao zinataka kuangushwa,walitumia majeshi yepi kupigana wakati waliuza watu wao,au ni nani angekubali kupigana kwa niaba ya chief mpumb.avu ambaye anauza watu wake.
 
Katika vita vijijini, anayeshindwa Lazima atoe watu wake watumike Kama watumwa au wake wa wanavijiji walioshonda vita. Ukisoma "Things Fall Apart" na Chinua Achebe utaelewa zaidi. Pili, wazungu na warabi walichukua advantage hii na kufanya biashara na machifu wenye Nguvu. Divide and rule! Ukumbuke simu Gozo Hamna Mpaka, ila ukabila tu. afrika iligawanyiwa pale Berlin 1880 ili wazungu wazidi kuwatenga wanavijiji wenye asili Moja .
 
Wazungu na Waarabu pia walitumia Nguvu kuwateka na kuwauza Waafrika katika masoko ya utimwa Mpaka uingereza ilipoingilia Kati na kusema kuwa katika makoloni Yake haitaruhusu utumwa tena kwa kutumia unabe wa jeshi lake la Baharini. Pia, tukumbuke kuwa Enzi hizo Hamna UN, ndugu wa damu wanauana ili kupata kiti cha inflame au ardhi zaidi. Kumbuka wag slime wote wa ulaya Mpaka Leo ni damu Moja kwa mfano czar wa urusi Alikuwa binamu wa kaiser wa ujerumani pamoja na ndugu Yao wa Karibu Mfalme wa uingereza, king George IV.
 
Ehud

njoo jukwaa la dini nikufunde mwali

Mkuu, kuna msemo unasema pezwa hujipalilia makaa mwenyewe.

wewe ikiwa huna la kunijibu hapa kwenye jukwaa la siasa unataka kutafuta janga kubwa zaidi kwenye dini

kwa taarifa yako tu, ninalijuwa bibilia juu chini, na wewe labda uwe padri ulobobea ndio uweze kuhimili hoja zangu za kidini otherwise save urself from BP mkuu
 
Tokyo40

Katika vita vijijini, anayeshindwa Lazima atoe watu wake watumike Kama watumwa au wake wa wanavijiji walioshonda vita. Ukisoma "Things Fall Apart" na Chinua Achebe utaelewa zaidi. Pili, wazungu na warabi walichukua advantage hii na kufanya biashara na machifu wenye Nguvu. Divide and rule! Ukumbuke simu Gozo Hamna Mpaka, ila ukabila tu. afrika iligawanyiwa pale Berlin 1880 ili wazungu wazidi kuwatenga wanavijiji wenye asili Moja .

haya yote ulosema ni kwlei na ninayasapoti

lakini nina suala moja tu kwako

hivo vita vya makabil ahuko tangayika vichukuwa muda gani na biashara ya utumwa ilichukuwa muda gani?
 
Bin Faza, elimu yangu ni Ndogo kuhusu utumwa tanganyika na biashara ya utumwa. Ila Najua Kwamba Waafrika Kabla ya Wakoloni kuwagawanya walikuwa wanapigana vita ili wapate ardhi zaidi, Mali na watumwa wa kuwafanyia kazi zao. Hii imeelezwa katika kile kitabu cha Achebe. Na Sio tu afrika ila dumiani kote mnyonge Alikuwa anapokonywa ardhi na Ngugu zao kuwa watumwa Kabla utumwa haujapigwa vita. Kwa mfano, marekani walichukua ardhi kubwa ya Mexico kwa kuwa kijeshi Mexico walishindwa katika vita . Sasa California, New Mexico, Nevada, Texas, Arizona n.k ni Mali ya USA. Zote zilikuwa Mikoa ya Mexico.
 
Back
Top Bottom