Kwanini Ali Kiba hataki bifu lake na Diamond liishe?

Yeye mwenyewe kachoka tu nyimbi zake hazina kiki kama zamani. Hata skendo za wema tu zinampoteza na mziki wake. So.lazima atafute nyota ya mtu atembelee ndio maana anampigia magoti kiba. Ingawa akina salah ndio walikuwa busy kwa matusi mitandaoni
Huyo 'salah' ndo nani mkuu?!
 
UShabiki mwingine ni shida domo si ndio alianza bifu sasa anataka liishe ili iweje .kilichomfanya babu tale azime mic kule mombasa nini .ungekuwa wewe ungelimaliza hilo bifu? Hapo kuna jambo la hatari litakuja kiba usikubali ng'oooo
Duh yaani we ndio hujui kitu kabisa hasa hyo habari ya kusema ban tale ndo alizima mic... Umekurupuka sana aisee
 
Mbona hajataja jina au wewe umejuaje anaeongelewa ni chibu dangote?wewe ndio mchochezi,shenzi
 
Yani kuna vitu vingine haviitaji akili kuwaza mtu anakutusi kila mstari wa nyimbo zake,kwa interview ukiulizwa ukiona kiba unaona nini unajibu VITA! Leo hii umefungua kiplatform chako cha kuuza mziki unataka kutubuni watu ili waingie mkenge upige pesa kupitia yeye! Diamond mdomo umkuponza Kiba sio boya kama unavyo mfikiria ! Usiforce ushost
 
Hakuna balaa kama siku bubu akipata nafasi ya kuongea [emoji23][emoji23][emoji23]
Siamiani kama mashabiki wa Diamond leo wamepata hasira baada ya Kiba ku-post maneno yanaonyesha kamlenga Diamond ambae kiuhalisia ndio nguli wa kutupa vijembe kwa Kiba na ni tabia yake ya muda mrefu nafikiri mashabiki wa Diamond wameumia zaidi kwa kua Kiba amejibu wakati ambao Diamond kama alikua anarudi kwenye mstari ivi kitu ambacho kwa tafsiri nyepesi utadhani alikua anamaliza msuguano wao hata mashabiki wake wehu hawakupenda Diamond aonyeshe kufungua mikono kwa Kiba wanatamani aendelee kutoa vijembe bahati mbaya siku ambayo kapoa kwenye media ndio siku ambayo Kiba kajilipua kuliko siku zote naamini Kiba aliisubiri kwa muda wakati kama huu ufike ili roho yake nae isuuzike baada ya kupigwa sana vijembe,niliwahi kusema Diamond alipofikia hana sababu ya kupenda kejeli na dharau hasa kwa kauli zake tata maana siku zinakimbia ukimsema mtu hawezi kumiliki buku hakika siku akipata buku 10 lazima uteswe na kauli zako kwa mfano hakukua na sababu kwenye video ya Kokoro kuweka vijembe vya Kiba kulala kuhusu kuzimiwa Mic ila kwa kupende vijembe akapitisha kijembe kiwemo kuna kauili nyingi kama "Ana post show wao wana post tembo" au "Waambie dada zao wa k'koo waje Ulaya" ukiangalia leo aliyomnanga Kiba yote hayana maana kwa kua Kiba anafanya show toka mwaka umeanza na kama Ulaya nadhani imekua sio ishu tena na awards za nje kabeba.
Hawa watoto ipo siku wenyewe waatachana na huu msuguano bila kuambiwa maana music cycle ni baba wa kila kitu ipo siku tutawasikiliza kama wasanii wa kawaida tu bila kushtuka hapo ndipo wanatakua kitu kimoja nani alijua Nature na Inspector leo wangekaa maskani moja wanawaza bangi nzuri watapata wapi ila muda umewakutanisha,hakuna TMK wala ECT tena,Prof J leo anazunguka na Sugu,hakuna Sister P wala Zay B ni suala la muda tu na kwa kua malumbano yao yanawapa pesa na wanakua motivated kufanya kazi bora tuwaache wamalize ujana wao ni heri hawapigani zaidi ya maneno tu.
 
Ni kwasababu yeye ndiyo aliyekosewa, hivyo basi mkosaji anatakiwa amuombe msamaha.
 
Mei 2016:Mie siwezi kusainishwa itakuwa haina maana hao SONY walinifuata(baada ya Ally kusaini Sony)
Disemba;-Mziki wao unaishia Chalinze, watoke nje wafanye show wajaze watu. Mayote wanaongea kifaransa tuu ila wanaimba nami.
-Sina pete ya kijani mie.
-Ni msanii pekee mwenye nyumba Afrika kusini.
-Nimesaini Univesal nyimbo za WCB zitauzwa huko

Januari: Ukisikia jina Alikiba kitu gani chakujia kichwani?.... Vita

Machi: Kiba namheshimu hatuna tatizo tunajaribu kuongea na uongozi wake wauze nyimbo kwetu...


Daima wakati rafiki mwema[\b]

Jizuie kuropoka wote wanaoneana wivu bila sababu Naseeb kamzidi Ally pakubwa lakini chuki na dharau zake dhidi ya Ally zinaonekana kama vile Ally alivyo na chuki dhidi ya Naseeb.

Nashangaa kuna wanaomwona mmoja mtakatifu kisa mafanikio yake wengine kisa upole wake.
 
nilimuelewa sana diamond jana kwenye kipindi cha Clouds 360. bifu tuna lizidisha mashabiki sisi, sisi mashabiki tuki kaa kimya hakuna kitakacho tokea.

Jana Diamond alisema wakikutana huwa wanaongea mara ya mwisho kuongea ilikuwa ni Kenya. na ndiyo mana diamond ana taka nyimbo za kiba ili ziuzwe kwenye tovuti ya wasafi. ana subiri jibu.

KWA MIMI NINAVYO ONA HII BIFU IPO KIBIASHARA YANI KIMZIKI ZAIDI...SASA SISI MASHABIKI TUNA IPELEKA KWENYE MAISHA YAO BINAFSI
 
Kwa story ya ndani akina ruge ni mmoja wa washauri na wasimamizi wa dimond,,na siku moja Ruge wakat yupo XXL akihojiwa kuhusu Lady Jay D alichomekewa swali kuhusu bifu la dimond na kiba,,na akaambiwa kwamba yy ni mtu anaeweza kuwakalisha chini na kuwapatanisha,,lakin alijib jibu ambalo nimeelewa ni kwa nn bif hili halipo katibu kuisha,,,

Nanukuu.....

Matatizo ya dimond na kiba sio makubwa kama wengi wanavyodhan,,ni suala la kibiashara tu ndio maana hakuna kati yao aliesema ana ugomvi na mwenzie,,hii bif inakaliwa sana na mashabiki wao,,mashabiki wa kiba huwaambii chochote wakakuelewa kuhusu dimond na mashabiki wa dimond hawaelewi cchote kutoka kwa kiba,,so mm binafsi sipend bifu liishe sababu ni biashara kubwa,,likiisha kuna biashara nying hazitafanyika.. Mwsho wa kunukuuu...

Kwa hyo hii ni biashara za watu ambao tupo mbali tunaweza ona kuna bonge la ugomvi lakin walaaaaaa
 
Wote wanafiki hakuna cha mashabiki wala nani Almas mnafiki tuu kama alivyo Ally
 
Mbona hajataja jina au wewe umejuaje anaeongelewa ni chibu dangote?wewe ndio mchochezi,shenzi
Yani hadi Leo hujajua jinsi yakufikili
Naenda fb ndio saiz yako uku waachie wakubwa
 
unataka kutwambia kiba huwa harushi vijembe kwa mond....au unajitoa ufaham mbona mond mnapendaga kumuona ndo mrusha vijembe sana kwa mwenzake lakini vijembe vya alikiba huwa hamvioni.....kumtuhumu mwenzio ananunua tunzo mara view zako ni real cyo za kutumia robot, mara mziki mzuri no janja janja.....kuingilia show ya mwenzio as a sapraiz artist (mombasa) hivo vyote huwa hamvioni

ingia sporah show kipindi kiba ndo yupo kwenye harakati za kurudi uone vijembe ambavyo kiba alivitupa kwa mond cyo vya nchi mfano, kizuri kikikosekna hata kile kibaya huonekana kizur.....mlishangilia sna hizi kauli lakini mond akijibu moja tu mnaandamana......nashauri kitu kimoja kama mond unapitaga kwenye hii jamii forum pliz usije ukamzungumzia kiba tena even kwa uzuri even kwa ubaya maana ww umeonyesha kutaka yaishe mwenzio kachukua advantage ya kama ww umesarenda.....wenye akili tumeng'amua kuwa ni yupi ana beef na mwenzie pliz mond usije kujibu swali lolote linalomuhusu huyo wa mchangani....jana umeniuzi na kunikera kuzidi siku yyt tangu nianze kuwa shabiki yako.....umeonyesha weakness ya hari ya juu sana.
 
Itakua hili bifu ndo linampa kiki zaidi ko hataki kupoteza hiyo.
Ata hivyo amefika adi alipofika bila msaada wa mondi, why ajisalimishe saivi? Ana kiburi cha kiume kiume "Ego".
Kama mondi aliweza pambana mpaka akachomoka, kwanini yeye ashindwe mpaka ashikiliwe mkono na mond?
 
Vipi kuhusu kajiandae na aje remix au kwa kuwa ww ni team kiba hulioni hilo.....ukweli unajulikana kuwa bila beef kiba mziki unamuishia maana wanaomsapoti ni wale anti diamond damu damu
Ndio.
Kiba hana fans bali ana antfans wa mondi. Ndo maana upepo ukimjia msanii flani wote wanahamia huko kama darasa na harmorapa. Kwenye page zao zimejaa post za mondi kuliko za kibakuli. It's obvious sio fan wa kiba bali antfans wa mondi [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…