Infinite_Kiumeni
JF-Expert Member
- Jan 23, 2023
- 382
- 687
Umemshawishi ukachukua namba ya mwanamke mzuri umtakaye.
Akilini mwako ushapanga kumtoa out. Jinsi utakavyomfikisha kileleni na ufundi wako wa kitandani. Kadri siku zinavyozidi kwenda ndo unazidi kumuwaza na kuona unachelewa.
Ukikutana nae katika mizunguko ya kila siku mnaongea vizuri tu.
Pengine unamtongoza kila ukikutana nae. Unamnunulia vitu vizuri na kumshawishi. Au unamtembelea anapoishi mara kwa mara lakini haoneshi kusogea mbele kwa kile unachokitaka.
Kila ukimtumia sms hajibu, unabaki kujiuliza unakosea wapi?
Kwanza ujue wanawake wana sms nyingi za kujibu hivyo uwe na subira lakini muhimu ujue haya ili upo wapi na ujue cha kufanya.
Umeharibu mwenyewe.
Ukipenda kupitiliza unakua na tamaa.
Unahisi mambo yanaenda taratibu sana na utampoteza usipofanya jambo. Inawezekana mwanamke mwenyewe alishakukubali lakini akishaona amekua na tamaa kwake anakua hana mpango na wewe. Unaonesha udhaifu.
Aitha umekua ukimshawishi sana kukupenda kiasi kwamba unaomba penzi. Au unamtumia sms nyingi mno au muda wote upo kwa ajili yake. Au unamtongoza kila mara, ukiamini ndo utaharakisha mambo.
Kwa mwanamke ataona unamkosesha uhuru, unalazimisha penzi.
Atakuona unataka kumtumia tu kisha umuache. Atapotezea sms zako ili upunguze kasi na usimbane sana.
Kama ulikua unafanya hivyo, au vitu kama hivyo basi punguza kasi.
Hajavutiwa na hana mpango na wewe kimapenzi.
Shida huanza pale unapopenda usipopendwa.
Wanawake wengi hawawezi kukuambia hujanivutia, watatumia njia za kukukataa kimtindo ili ujiongeze na umuache. Mtu hachagui kuvutiwa na mwingine, hutokea tu. Ndo maana unaona hata umshawishi vipi huyo mwanamke hawezi kuwa na wewe, labda kama ni mchunaji atakukubali ili kukutumia tu.
Anakuchangamkia ili usijisikie vibaya, lakini anakupotezea muda tu.
Hivyo, angalia jinsi ya kumpotezea usije ukautesa moyo wako.
Hajui unachokitaka.
Pengine hujafanya kosa la hapo juu.
Mwanamke naye amevutiwa na wewe.
Anasubiri umuongoze vile unavyotaka.
Lakini kila ukimtumia ujumbe, hauna mwelekeo wowote. Mnachati tu, mnachati kuhusu kila kitu lakini humwambii vizuri unataka mtoke. Pengine unamwambia nitakupeleka sehemu fulani, au ntakufanyia hivi na vile. Unamuuliza umpeleke wapi au kama anataka kutoka na wewe.
Vyote hivyo vitamfanya mwanamke aone hujui unachofanya na huna ujasiri. Atakupotezea ataona unampotezea muda tu.
Mwanzoni mwanamke hawezi kukuongoza (labda kama amekupenda sana) kupanga vitu.
Cha kufanya, chati naye sms mbili tatu kisha muulize siku ambayo yupo na nafasi, kisha mwambie hiyo siku utamtoa out, saa fulani na mkutane sehemu fulani, basi.
Umejiweka kirafiki mno.
“Acha tuwe marafiki kwanza alafu baadaye atanipenda”.
Ukiona unajiambia ivo ujue utapata hilo penzi endapo mwanamke atakosa mwanaume. Kitu ambacho ni nadra sana.
Hutaki kumkwaza kivyovyote. Sms zako zitakua hazimshawishi au kumsisimua kihisia sababu unatuma kirafiki mno. Kabla hujatuma sms isome wewe kwanza alafu jiulize je hii sms ina ushawishi wowote?
Ushawishi wako kwa mwanamke ndio utamfanya ajibu sms zako, pia ukikutana naye hakikisha unashawishi hisia zake kiasi kwamba awe anakuwaza. Kumshawishi nii jambo endelevu, la sivyo atakuchunia na atajibu sms za wanaomshawishi.