Kwanini Arsene hafukuzwi kazi Arsenal?

Kwanini Arsene hafukuzwi kazi Arsenal?

Kama wanataka kumbakisha, wampe kazi kwenye uongozi, ukocha awaachie wengine.
Asee Hata Mi Ndo ningependa iwe hvo., ni ngumu kwa Arsenal kuja kuchukua ubingwa chini ya Arsene Wenger...
 
Wenger siku akiamua mwenyewe kutimka, bila hivyo sidhani.
 
UKIFIKA katika eneo la mazoezi la Arsenal katika eneo la Colney, takribani kilomita 41 kutoka katika ya Jiji la London, hakika utasema kuwa Arsenal ni klabu kubwa na ina mipango madhubuti.

Eneo hilo kwa nje linaonekana utafikiri ni la kawaida, lakini kuna ulinzi mkali. Unapoingia ndani mambo ni tofauti kwa kuwa eneo ni kubwa sana. Viwanja kumi vya soka, pia kuna uwanja mmoja wa ndani, gym kubwa na sehemu maalum kwa ajili ya masuala ya afya.

Thamani ya eneo hilo ni zaidi ya pauni milioni 10 (zaidi ya shilingi bilioni 28) na imekuwa ikizidi kuongezeka thamani kadiri siku zinavyosonga mbele na sasa kuna sehemu bora ya mazoezi kwa ajili ya timu za watoto na vijana.

Arsenal ina hadhi ya Real Madrid au FC Barcelona hasa unapozungumzia sehemu ya mazoezi au uwanja kama ulivyo ule wao wa Emirates.

Kabla ya hapo, Arsenal ilikuwa inafanya mazoezi kwenye uwanja wa chuo ambao pia unatumiwa na timu ya Watford ambao unapakana na eneo la sasa la Arsenal ambalo ni mali yake.

Mtu wa kwanza kutia msisitizo kutaka Arsenal iwe na eneo lake na baadaye akatoa wazo la kusaidia kupatikana kwa uwanja ambao unamilikiwa na Arsenal ni Kocha Arsene Wenger, ambaye mwisho alisaidia kwa wazo la kumuuza Nicholas Anelka kwenda Real Madrid na baadaye fedha kuwa chanzo cha ununuzi wa mashamba ambayo sasa ndiyo eneo la mazoezi la Arsenal.

Wenger raia wa Ufaransa, ndiye alikuwa sehemu ya chanzo cha uamuzi wa Arsenal kuona wakati mwafaka wa kujenga uwanja mpya umewadia na mipango ya Emirates ikachagizwa na mwisho, leo Arsenal ni kati ya timu 10 za Ulaya zinazomiliki uwanja wa kisasa zaidi.

Arsenal imeendelea kuwa ndani ya 10 bora na mara nyingi 5 bora ya timu za Ulaya ambazo ni tajiri kifedha. Hii inaonekana ni mipango mizuri iliyoanzishwa na Wenger na inaonekana wazi, klabu imekuwa ikimtumia kama kocha, wakati mwingine kama mtaalamu wa masuala ya kiuchumi.

Kila klabu yenye viongozi wenye “akili timamu” za kibiashara duniani, lazima itaangalia suala la faida kwanza na mengine yatafuatia.

Klabu ipo kwa ajili ya kufanya biashara na biashara ni faida na si kutoa sadaka. Kama klabu inaingiza faida, hakika inakuwa inapanga kuingiza faida zaidi. Na kama kuna mtu anaisaidia kufikia inachokitaka, hakika lazima impe thamani kubwa.
Kuna mtazamo tofauti kati ya mashabiki wengi wa Arsenal na uongozi wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa kuendelea kumbakiza Wenger ambaye anaonekana ni kero kwa mashabiki wengi wa Arsenal wakiwemo wale kutoka Tanzania.

Tokeo Wenger ametua Arsenal mwaka 1996 akitokea Grampus Eight ya nchini Japan, amefanikiwa kubeba makombe matatu ya Ligi Kuu England, mataji saba ya Kombe la FA na Ngao za Jamii saba pia.

Kama ni makombe, ukiachana na ngao maana yake anayo kumi. Huyu si mtu ambaye unaweza kusema amefeli na huenda kizazi cha Arsenal kuanzia miaka mitano au sita kimekuwa na hamu kubwa ya kuona kombe la Ligi Kuu England linakwenda Emirates.

Kizazi hicho kinataka kuona kombe hilo, maana kama ni kombe, Wenger amebeba makombe ya FA matatu tokea mwaka 2013 hadi 2017 na kuifanya kuwa klabu ya England iliyobeba makombe mengi ya FA kwa kipindi hicho.

Hamu ya kuliona Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu England, imekuwa ni msukumo wa vijana au mashabiki wengi kutaka Wenger aondoke.
Mambo ni tofauti kabisa kwa uongozi wa Arsenal au wale Arsenal wenye uwezo wa upigaji wa mahesabu hasa kama wanaamini soka ni biashara kubwa na watu kama Wenger wanahitajika kuisaidia klabu kupata mafanikio makubwa kama kocha huyo Mfaransa alivyofanya.

Ukiachana na yale ya kikosi, Arsenal wanaonekana kuwa na manufaa makubwa na Wenger na huenda itakuwa kuna ugumu wa kumuondoa kama ambavyo mashabiki wengi wanataka.

Wenger anaendelea kuwa kiungo muhimu sana katika kikosi cha Arsenal na Klabu ya Arsenal. Viongozi na wamiliki wanamchukulia kama shujaa na ndiyo maana unaona wakati wengi wakipiga kelele aondoke, lakini uongozi wa klabu hiyo ulimuongezea miaka miwili ya kazi.

Hii inaonyesha, huenda wale wanaotamani au wanaotaka kumuona Wenger anaondoka, watasubiri kwa muda mrefu na wasio wavumilivu, wanaweza kuondoka Arsenal na kumuacha Wenger akiendelea “kudundadunda” ndani ya klabu huyo kutoka Kaskazini mwa jiji kubwa zaidi Uingereza la London.
Akifukuzwa ww utafaidika na nn acha roho mbaya
 
Hivi mkataba wake unaisha lini?
Mods nadhani muda umefika kwa kutoa msemo wa "be the first to reply" na kuweka "be Joseverest" maana daah..! Sio kwa kuwahi huku kureply..! [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Naona Pro-Arsene Wenger umejitahidi sana, nakubaliana nawe kwa sababu za stability na continuity, ila game imebadilika sana mkuu, babu anajaribu kukimbizana nayo ila am sorry to say his tenure at Game Theory has reached its life-cycle.
Kafanya mazuri mengi kwa fans na zaidi hasa kwa wawekezaji, ila tukubali kila kizuri kina mwanzo na mwisho, tatizo nafikiri walilonalo Board of Directors ni nani wa kumpa hicho kiti na aendeleze legacy.
Katika kuendeleza thread yako tumeona kuna power struggle Game Theory
Stan Kroenke makes £525m offer to buy Alisher Usmanov’s Arsenal shares Stan Kroenke makes £525m offer to buy Alisher Usmanov’s Arsenal shares
Twachoombea amalize hiyo miaka 2 vizuri aende, aje mwingine tuone tutaendelea kivipi...
 
Arsena WENGA hafukuzi arsenal hadi wabadilishe JINA LA TIMU...huoni majina yanavyofanana?
 
Naona Pro-Arsene Wenger umejitahidi sana, nakubaliana nawe kwa sababu za stability na continuity, ila game imebadilika sana mkuu, babu anajaribu kukimbizana nayo ila am sorry to say his tenure at Game Theory has reached its life-cycle.
Kafanya mazuri mengi kwa fans na zaidi hasa kwa wawekezaji, ila tukubali kila kizuri kina mwanzo na mwisho, tatizo nafikiri walilonalo Board of Directors ni nani wa kumpa hicho kiti na aendeleze legacy.
Katika kuendeleza thread yako tumeona kuna power struggle Game Theory
Stan Kroenke makes £525m offer to buy Alisher Usmanov’s Arsenal shares Stan Kroenke makes £525m offer to buy Alisher Usmanov’s Arsenal shares
Twachoombea amalize hiyo miaka 2 vizuri aende, aje mwingine tuone tutaendelea kivipi...
aje mwingine nani?!..wachezaji wa arsenal wangekua wanacheza kama walivocheza game ya Chelsea juzi..ndani ya miaka 10 ilyopita wangechukua ubingwa walau Mara 3..tatizo hawakazani,na sidhani MTU mzima kama Ramsey anatakiwa kuimbiwa mapambio ya kukazana na wenger
 
Naona mkuu unapigilia msumari wa moto kwa mashabiki wa Arsenal
 
2019 katikati
Huyu mzee tukitaka aondoke labda Mungu amchukue siombei lakini ila ndo ukweli ulivyo.......

Huyu mzee anataka aondoke kwa heshima kwa kuwapa watu kombe la Epl
 
Xhaksminist: 23805604 said:
Mkuu,sikatai Wenger ni kocha mzuri., bt show ya epl imebadilika pakubwa mno...
Kimebadilika nini zaidi ya man city kuwa timu yenye hela?
 
Arsenal watakuwa vizuri sana msimu ujao wameajiri jamaa wawili mmoja kutoka dortimund huyu yupo vizuri sana kwenye kurecriut wachezaji wazuri
eb24b5e8061902a6fc19309b62df54f3.jpg
Alafu wamemchukua mkurugenzi wa maswala ya soka wa barcelona huyu sasa ni mzee wa figisu yupo vizuri kwenye mambo ya mikataba ya wachezaji na mambo ya usajili kwa ujumla
ce78f3b3eeb9ab7a5327a5cb431a5205.jpg
 
aje mwingine nani?!..wachezaji wa arsenal wangekua wanacheza kama walivocheza game ya Chelsea juzi..ndani ya miaka 10 ilyopita wangechukua ubingwa walau Mara 3..tatizo hawakazani,na sidhani MTU mzima kama Ramsey anatakiwa kuimbiwa mapambio ya kukazana na wenger
Timu kama wake zetu?! Yaani hujuwi mkiamka kuna kucheka au kununiwa!
Shidaaa...
 
UKIFIKA katika eneo la mazoezi la Arsenal katika eneo la Colney, takribani kilomita 41 kutoka katika ya Jiji la London, hakika utasema kuwa Arsenal ni klabu kubwa na ina mipango madhubuti.

Eneo hilo kwa nje linaonekana utafikiri ni la kawaida, lakini kuna ulinzi mkali. Unapoingia ndani mambo ni tofauti kwa kuwa eneo ni kubwa sana. Viwanja kumi vya soka, pia kuna uwanja mmoja wa ndani, gym kubwa na sehemu maalum kwa ajili ya masuala ya afya.

Thamani ya eneo hilo ni zaidi ya pauni milioni 10 (zaidi ya shilingi bilioni 28) na imekuwa ikizidi kuongezeka thamani kadiri siku zinavyosonga mbele na sasa kuna sehemu bora ya mazoezi kwa ajili ya timu za watoto na vijana.

Arsenal ina hadhi ya Real Madrid au FC Barcelona hasa unapozungumzia sehemu ya mazoezi au uwanja kama ulivyo ule wao wa Emirates.

Kabla ya hapo, Arsenal ilikuwa inafanya mazoezi kwenye uwanja wa chuo ambao pia unatumiwa na timu ya Watford ambao unapakana na eneo la sasa la Arsenal ambalo ni mali yake.

Mtu wa kwanza kutia msisitizo kutaka Arsenal iwe na eneo lake na baadaye akatoa wazo la kusaidia kupatikana kwa uwanja ambao unamilikiwa na Arsenal ni Kocha Arsene Wenger, ambaye mwisho alisaidia kwa wazo la kumuuza Nicholas Anelka kwenda Real Madrid na baadaye fedha kuwa chanzo cha ununuzi wa mashamba ambayo sasa ndiyo eneo la mazoezi la Arsenal.

Wenger raia wa Ufaransa, ndiye alikuwa sehemu ya chanzo cha uamuzi wa Arsenal kuona wakati mwafaka wa kujenga uwanja mpya umewadia na mipango ya Emirates ikachagizwa na mwisho, leo Arsenal ni kati ya timu 10 za Ulaya zinazomiliki uwanja wa kisasa zaidi.

Arsenal imeendelea kuwa ndani ya 10 bora na mara nyingi 5 bora ya timu za Ulaya ambazo ni tajiri kifedha. Hii inaonekana ni mipango mizuri iliyoanzishwa na Wenger na inaonekana wazi, klabu imekuwa ikimtumia kama kocha, wakati mwingine kama mtaalamu wa masuala ya kiuchumi.

Kila klabu yenye viongozi wenye “akili timamu” za kibiashara duniani, lazima itaangalia suala la faida kwanza na mengine yatafuatia.

Klabu ipo kwa ajili ya kufanya biashara na biashara ni faida na si kutoa sadaka. Kama klabu inaingiza faida, hakika inakuwa inapanga kuingiza faida zaidi. Na kama kuna mtu anaisaidia kufikia inachokitaka, hakika lazima impe thamani kubwa.
Kuna mtazamo tofauti kati ya mashabiki wengi wa Arsenal na uongozi wa klabu hiyo ambayo imekuwa ikilaumiwa kwa kuendelea kumbakiza Wenger ambaye anaonekana ni kero kwa mashabiki wengi wa Arsenal wakiwemo wale kutoka Tanzania.

Tokeo Wenger ametua Arsenal mwaka 1996 akitokea Grampus Eight ya nchini Japan, amefanikiwa kubeba makombe matatu ya Ligi Kuu England, mataji saba ya Kombe la FA na Ngao za Jamii saba pia.

Kama ni makombe, ukiachana na ngao maana yake anayo kumi. Huyu si mtu ambaye unaweza kusema amefeli na huenda kizazi cha Arsenal kuanzia miaka mitano au sita kimekuwa na hamu kubwa ya kuona kombe la Ligi Kuu England linakwenda Emirates.

Kizazi hicho kinataka kuona kombe hilo, maana kama ni kombe, Wenger amebeba makombe ya FA matatu tokea mwaka 2013 hadi 2017 na kuifanya kuwa klabu ya England iliyobeba makombe mengi ya FA kwa kipindi hicho.

Hamu ya kuliona Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu England, imekuwa ni msukumo wa vijana au mashabiki wengi kutaka Wenger aondoke.
Mambo ni tofauti kabisa kwa uongozi wa Arsenal au wale Arsenal wenye uwezo wa upigaji wa mahesabu hasa kama wanaamini soka ni biashara kubwa na watu kama Wenger wanahitajika kuisaidia klabu kupata mafanikio makubwa kama kocha huyo Mfaransa alivyofanya.

Ukiachana na yale ya kikosi, Arsenal wanaonekana kuwa na manufaa makubwa na Wenger na huenda itakuwa kuna ugumu wa kumuondoa kama ambavyo mashabiki wengi wanataka.

Wenger anaendelea kuwa kiungo muhimu sana katika kikosi cha Arsenal na Klabu ya Arsenal. Viongozi na wamiliki wanamchukulia kama shujaa na ndiyo maana unaona wakati wengi wakipiga kelele aondoke, lakini uongozi wa klabu hiyo ulimuongezea miaka miwili ya kazi.

Hii inaonyesha, huenda wale wanaotamani au wanaotaka kumuona Wenger anaondoka, watasubiri kwa muda mrefu na wasio wavumilivu, wanaweza kuondoka Arsenal na kumuacha Wenger akiendelea “kudundadunda” ndani ya klabu huyo kutoka Kaskazini mwa jiji kubwa zaidi Uingereza la London.
Watamtoa kama Mugabe
 
Back
Top Bottom