Kwanini asisifiwe Mwananchi anayelipa kodi inayotekeleza miradi ya kitaifa?

Duh
 
Shida hapa ni elimu ya kodi,kodi ni ya serikali .Utapogezwa kwa lipi wakati kitu sio chako,neno kodi mmiliki ni serikali ndio maana inapongezwa kwa kutumia pesa zake vizuri.Wewe ukitumia pesa zako vizuri tutakupongeza ,chanzo chako cha mapato ni mjadala mwingine ,ukijenga nyumba sifa ni kwa taasisi iliyokulipa au tunakusifia wewe?Hakuna mwananchi mmiliki wa kodi .Mwananchi ni chanzo kimoja kati ya vingi vya kodi ,serikali ianze kupongeza vyanzo vyote vya kodi zikiwemo taasisi zake maana zinalipa kodi ndio mnataka tuende kwa mfumo huu.Yaani wewe ukilipa ada ya watoto wako tunaipongeza biashara yako au kazi yako iliyokuletea kipato.Elimu ya kodi bado sana nchi hii.
 
Binafsi naunga Mkono kuwa fedha hizo ni Kodi za wananchi lakini kumpongeza kiongozi kwa kusimamia fedha hizo na kufanikisha miradi yenye ubora tarajiwa ni jambo zuri pia ilimradi haligharimu sana, ikumbukwe viongozi hao wanauwezo wa kutotekeleza kwa ufasaha kazi zao na kusababisha huduma mbovu kwa wananchi. Hivyo kiwapongeza kunawaongezea moyo wa kuona wanaotutumikia tunathamini kazi zao ikumbukwe wao pia wanalipa Kodi na ni wananchi pia.
 
Hilo la kusifia Rais ni issue nyingine ambayo tungeifikia mwisho wake bila shida na kilichokuwa kinatafutwa ni point ya kumhalalishia sifa hizo.

Shida iliyopo katika hoja yangu kwako ni ile tabia yako ya kutumia naneno ovu katika mjadala.

Hauwezi mwambia mtu usiyemfahamu kuwa ni 'mjinga', 'mwivu' sijui 'mpumbafu' katikati ya mjadala, wakati ukielewa wazi kuwa maneno hayo ni matusi.

Kwani tunayojadili humu tunalipwa ama kulazimishwa na mtu?

Mi nadhani ni kwa ajili ya kutupatia furaha na kupatuana mawazo!
Sasa yote hayo utayapata kati kati ya matusi!
 
Ulienda shule wewe kweli? Ili mtu awe mjinga inahitaji kumfahamu au tunaangalia unachoandika ndio tuna draw conclusion? Ujinga ni kutokuwa na ufahamu wa jambo
 
Inapendeza ikiwa ... jengo hili ni kwa Hisani ya Kodi za Wananchi wa JMT
 
Mkuu mi nimefurahishwa sana na andiko lako.

Sisi tangu Magufuli tuliipenda kasi ya ufanyaji wa Serikali hasa kwa nyanja za kimaendeleo.

Ila hapa kuna hoja ya msingi hasa linapokuja suala la upindishaji wa lugha sahihi inayopotoshwa kwa makusudi.
Hivi kusema 'mheshimiwa Rais katoa pesa', tena kwa kutaja jina lake halisi, yaani majina yake yote kana kwamba kuna raia asiyemfahamu, unaiona ni sahihi kweli?

Embu tumalizane na hili kwanza nikitumaini uliyoyaongea mengine yapo sahihi.
 
Kuna miradi ipo na imepitishwa kwenye budget lakini pesa ya kutekeleza haipo ,sasa Rais anaweza kutumia mamlaka yake kulazimisha utekelezaji wa mradi huo,pesa zinatoka wapi watendaji mtaumiza vichwa .Huu ni mfano mmoja ambapo Rais anapongezwa .Mfano wa pili chadema walikataa kupokea ruzuku miaka 3 ,kila mwaka bilioni 1 ,sasa kwa mwaka wa kwanza hiyo pesa ilipangiwa matumizi mengine serikali haiwezi kuangalia pesa tu mambo ni mengi ,mwaka wa pili hivyohivyo ,mwaka wa tatu maridhiano yanafanyika chadema wanaweka masharti kulipwa ruzuku miaka mitatu,mlipaji wa serikali anasema hiyo pesa haipo ,Rais anasema walipwe mtajua itatoka wapi ,japo ni haki yako kulipwa mazingira ya kulipwa yanafanya umpogeze Rais kwa kutaja jina la babu yake.Vinginevyo ingekuwa madai ya miaka nenda rudi.
 
Hii imekuwa kawaida sana katika nchi yetu lakini lengo na madhumuni ya kumsifia kiongozi hata kama anafanya mabaya ni yeye aonekane anafanya vizuri kwa wananchi na pia watoa sifa pia wao wanaangalia promotion ya vyeo kwa nchi yetu hii imekuwa ni kama propaganda ya watu flani ili kufanikisha jambo lao.
 
Kimsingi kwa katiba mbovu ukishalipa kodi hiyo Hela siyako Bali ya rais nayeye anaamua afanyie Nini!!!
 
Kumsifia mtu ambaye hatoi hata 💯 kutoka mfukoni mwake kufanikisha hiyo miradi; nadhani ni uwendawazimu wa kiwango cha juu sana.
 
Umesema kweli mkuu hawa machawa wanafikiri kwa kutumia matumbo badala ya vichwa
 
Kiongozi anapewa sifa kutokana na jukumu alilonalo kikatiba la usimamizi wa Kodi zetu. Na inapotokea mambo yameenda vibaya wa kwanza kulaumiwa huwa ni kiongozi na huwa tunamlaumu kwa sababu ya kushindwa majukumu yake ya usimamizi wa Kodi zetu.
 
Vile anavyopewa sifa mbaya kutokana na matendo ya Wananchi wake na ndivyo anavyopewa sifa mzuri pale anaposimamia vyema fedha za Wananchi wake.
Mfano ukitokea ukame Wananchi wakashindwa kuzalisha chakula na wengi wakafa basi atalaumiwa kwa kutochukua hatua Ili kuokoa wananchi wake. Ataitwa mzembe!


Anyway mnapata shida kubadilisha asili ya uongozi na kike kinachoitwa mafanikio au utendaji kazi wa kiongozi.
 
MIMI NAKATWA 1.1 MIILLION PER MONTH SIJAWAHI SIFIWA HATA SIKU MOJA .DAAAAH
 
Kiongozi anapewa sifa kutokana na jukumu alilonalo kikatiba la usimamizi wa Kodi zetu. Na inapotokea mambo yameenda vibaya wa kwanza kulaumiwa huwa ni kiongozi na huwa tunamlaumu kwa sababu ya kushindwa majukumu yake ya usimamizi wa Kodi zetu.
Kodi zenyewe wanaiba tu.hivi hatuwezi kuwa tunawafanyia APPRAISAL viongozi wetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…