HOJA Kwanini Azam Energy hawaoneshi kiwango cha caffeine kilichopo kwenye vinywaji hivyo?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika
A

Anonymous

Guest
Ningependa kuibua hoja kuhusu vinywaji vya Azam Energy Drink, ambavyo havionyeshi wazi kiwango cha caffeine kilichomo katika kila chupa.

Ninaomba mamlaka husika pamoja na wazalishaji wa bidhaa hii kushughulikia suala hili kwa kuweka taarifa sahihi na wazi kwenye vifungashio. Watumiaji wana haki ya kujua kiwango cha caffeine wanachotumia ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na matumizi yao ya kila siku.

Uwekaji wa taarifa hizi utasaidia kuongeza uwazi, kulinda afya za watumiaji, na kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango vinavyotakiwa vya utoaji wa taarifa kwa umma.
 
Vinywaji kwa watu maalum, ila ni hatari sana kwa usalama.
 
Uwekaji wa taarifa hizi utasaidia kuongeza uwazi, kulinda afya za watumiaji, na kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango vinavyotakiwa vya utoaji wa taarifa kwa umma.
Hii nimeshuhudia mpaka watoto na wamama wajawazito wanakunywa tena siku hizi hawaziiti energy kuna majina ya mtaa ndio wanaziita sijui majina gani ila ni code name nilimsikia mmoja anamuagiza mwenye duka baadae ndio nikajua kumbe ameagiza energy na ukimuangalia ni mjamzito ukiuliza anakunywa nani unaambiwa anakunywa yeye na mtoto alie tumboni km hujui huwezi kuelewa
 
Hatari sana.
 
Mkuu, guarana ni central nervous system stimulant ina caffeine pia ambayo inasanabisha uraibu ukitumia kwa muda mrefu unakuwa tegemezi.
Shida ni uraibu au shida ni madhira by the way guarana ni weak kuliko pure caffeine kwa sababu caffeine yake inakua release taratibu sana kuliko pure caffeine hivyo ni salama kiasi
 
Hii Hoja Yako Kuna Mdau Aliileta Mwanzoni Wakati Kiwanda Kimeanza Uzalishaji
Thread Ilijaa Hoja Nzito Sana Hapa JF Na Members
Walilalama Mpaka Mmoja Kutishia Kwenda Mahakamani
Sijajua Thread Bado Ipo Ama Vp
 
Hayo makitu sio salama kabisa. Kama una kitu unataka kupata mwilini then tumia vyakula vya asili. Unataka kuchangamsha mwili baada ya kupumzika tumia kahawa.
 
.
 
Attachments

  • Screenshot_20260706-081124.jpg
    Screenshot_20260706-081124.jpg
    43.2 KB · Views: 18
Shirika la viwango linapaswa kuwawajibisha.Hata hivyo kampuni nyingi sampuli wananzozipeleka TBS kwa ajilinya vibali,siyo hizi ambazo zinaingizwa sokoni.
 
ukichanganya ENERGY DRINKS +POMBE==KUUA FIGO

pia moyo ,pia figo,pia ubongo,pia nguvu za kiume ,pia kila kitu,ni carcinogens hayo mapombe

Jukumu la kulinda afya yako kipo mikononi mwako.
Sumu nyingi kwenye vyakula na mboga mboga na matunda kama haya ma APPLE haya kutoka SA

mboga za majani mboga mboga nyanya zunapulizwa dawa sana halafu zinaletwa shambani

NA MAPOMBE FEKI..

Miaka michache ijayo tutakuwa na WAGONJWA WENGI SANA WA SARATANI KANSA,FIGO NA WAGONJWA WA MOYO. na nguvu za kiume na n.k
 
Shida ni uraibu au shida ni madhira by the way guarana ni weak kuliko pure caffeine kwa sababu caffeine yake inakua release taratibu sana kuliko pure caffeine hivyo ni salama kiasi
Caffeine ni CNS stimulant kwa hiyo inasababisha uraibu kama ikiwa abused. Substances of active ingredient kuwa released taratibu haina maana ni salama.

Aidha ni pure au vinginevyo ni kwamba caffeine ina madhara kwa afya kuliko faida.
 
Kwanza kuendelea kutumia hizo ED pamoja na yote yanayohusishwa nayo ni wazimu.
 
Ningependa kuibua hoja kuhusu vinywaji vya Azam Energy Drink, ambavyo havionyeshi wazi kiwango cha caffeine kilichomo katika kila chupa.

Ninaomba mamlaka husika pamoja na wazalishaji wa bidhaa hii kushughulikia suala hili kwa kuweka taarifa sahihi na wazi kwenye vifungashio. Watumiaji wana haki ya kujua kiwango cha caffeine wanachotumia ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na matumizi yao ya kila siku.

Uwekaji wa taarifa hizi utasaidia kuongeza uwazi, kulinda afya za watumiaji, na kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango vinavyotakiwa vya utoaji wa taarifa kwa umma.
waweke au wasiweke, kitendo tu cha kuamua kunywa hayo matakataka ni upuuzi wa hali ya juuu.
 
Hivyo vinywaji mnanyweshwa nyie,wenyeww hata hawazigusi
Vinywaji pendwa wa bodaboda mixer visungura

Ova
kuna vitu vinawafaa watu au haviwadhuru watu kama inavyotazamiwa kutokana na mifumo yao ya maisha.

ukichunguza magonjwa mengi ya moyo yanachapa watu wa magari zaidi na sio hawa pangu pakavu wanaochomwa sana na jua.

hawa viumbe shida yao kubwa hawalali wanatumia hizi bidhaa kukata usingizi,matokeo yake sio kwenda kwa prof janabi ila kwenda uvunguni mwa malori.
 
Caffeine ni CNS stimulant kwa hiyo inasababisha uraibu kama ikiwa abused. Substances of active ingredient kuwa released taratibu haina maana ni salama.

Aidha ni pure au vinginevyo ni kwamba caffeine ina madhara kwa afya kuliko faida.
Binafsi tangu waanze kutumia guarana uraibu wangu kinywaji hicho umepotea hivyo kwa kiasi fulani ni hatua nzuri kwao
 
Ningependa kuibua hoja kuhusu vinywaji vya Azam Energy Drink, ambavyo havionyeshi wazi kiwango cha caffeine kilichomo katika kila chupa.

Ninaomba mamlaka husika pamoja na wazalishaji wa bidhaa hii kushughulikia suala hili kwa kuweka taarifa sahihi na wazi kwenye vifungashio. Watumiaji wana haki ya kujua kiwango cha caffeine wanachotumia ili waweze kufanya maamuzi sahihi kuhusu afya na matumizi yao ya kila siku.

Uwekaji wa taarifa hizi utasaidia kuongeza uwazi, kulinda afya za watumiaji, na kuhakikisha bidhaa zinakidhi viwango vinavyotakiwa vya utoaji wa taarifa kwa umma.
Hata wakiweka wazi Hiko kiwango Cha caffeine nani anayejali kusoma maelezo watu wanazinywa sana kwasababu ya uraibu
 
Back
Top Bottom