joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Mkuu mimi Ni shahidi kwa hili kama kuna udanganyifu Basi ujue umesukwa kweli kweli niliwahi hudhuria interview pale utumishi jamaa akazamia aseh jamaa walimfurusha ilibaki kidogo akabiziwe kwa ma pot kwa kweli wamezibiti sana yani sasa hivi sio rahisi kabisa labda wale wa kanzidata pia napo sio rahisi kiivyo, ila siwezi kukubishia yawezekana upo jikoni unajua kinachoendelea..Wanafanyakazi kazi kwa kweli na wamepunguza urasimu kwa asilimia kubwa, tofauti na taasisi zikiachwa ziajiri zenyewe
But udanganyifu upo, nitaleta thread humu siku moja.
Hujataja baadhi ya VYUO VIKUU,utaitwa kwenye USAILI lakini hutaitwa KAZINI.Yaani wanatangaza nafasi kwa ajili ya kukidhi masharti na matakwa kisheria kumbe kuna WATU WAO wameshawapanga kupata ajira.Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,
Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake(Kama taarifa zitakuwa ni sahihi).
Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.
Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.
Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.
Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.
Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.
Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TAPE,TBA TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100
TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.
Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.
Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.
Nini kifanyike:
Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.
Mungu ibariki Tanzania
Achana na hiyo mkuu ipo nitakuonesha siku nikileta uzi, halafu kinachofanyika pale zinaangaliwa taasisi zenye maslahi makubwa sio hizi ambazo ukiwekwa mshahara hautoboi mwisho wa mwezi.. na mipango yao sio ya kuzamiaMkuu mimi Ni shahidi kwa hili kama kuna udanganyifu Basi ujue umesukwa kweli kweli niliwahi hudhuria interview pale utumishi jamaa akazamia aseh jamaa walimfurusha ilibaki kidogo akabiziwe kwa ma pot kwa kweli wamezibiti sana yani sasa hivi sio rahisi kabisa labda wale wa kanzidata pia napo sio rahisi kiivyo, ila siwezi kukubishia yawezekana upo jikoni unajua kinachoendelea..
Mimi hapa kwenye nafasi za TPA kwakweli wamekuwa kimya sana alafu tunasubiri Aya majibu ili tuweze kufanya maamuzi sahihi mambo yangu watoe tu hata kesho roho yangu iridhike
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes mkuu hili linawaumiza Sana watoto wa maskini, yaani linazidi kuwatia umaskiniHujataja baadhi ya VYUO VIKUU,utaitwa kwenye USAILI lakini hutaitwa KAZINI.Yaani wanatangaza nafasi kwa ajili ya kukidhi masharti na matakwa kisheria kumbe kuna WATU WAO wameshawapanga kupata ajira.
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa iyo hii inawezekana kuwa sababu TPA wamechelewesha kutoa majina ya selected candidates?Achana na hiyo mkuu ipo nitakuonesha siku nikileta uzi, halafu kinachofanyika pale zinaangaliwa taasisi zenye maslahi makubwa sio hizi ambazo ukiwekwa mshahara hautoboi mwisho wa mwezi.. na mipango yao sio ya kuzamia
Basi ngoja nione hii ya TPA ntatupia macho vizuri uzuri Nina majina ya walioitwa interview walionde oral pia hivo tutafanya upembuzi yakinifu apoAchana na hiyo mkuu ipo nitakuonesha siku nikileta uzi, halafu kinachofanyika pale zinaangaliwa taasisi zenye maslahi makubwa sio hizi ambazo ukiwekwa mshahara hautoboi mwisho wa mwezi.. na mipango yao sio ya kuzamia
Pale utumishi wanafanya kazi Sana kwa kweli lazma tuwapongeze japo Kuna kasoroUtumishi mimi nawaamini kwani jamaa zangu wengi sana wamepata ajira.Ila hizi ajira za Ngorongoro (NCCA) zilizotoka mwenyewe nina wasiwasi nazo ,najiuliza sijui niapplya au niuchune manake naweza nikachoma nauli yangu ,nikasimamisha shughuli zangu mwisho wa siku wakati nyie masubiria mpite mlango wa mbele kibarazani,kumbe kuna wenzenu wamesha ingizwa uwani zamani.
Hawatoki nje ya mliofanya nao oral, Hawa wanapitia process zoteBasi ngoja nione hii ya TPA ntatupia macho vizuri uzuri Nina majina ya walioitwa interview walionde oral pia hivo tutafanya upembuzi yakinifu apo
Sent using Jamii Forums mobile app
Au TPA nao mishahara Ni ile ile ya walala hoi?Hawatoki nje ya mliofanya nao oral, Hawa wanapitia process zote
Mm najua ilishawahi kutangazwa nafasi za kazi NSSF watu wakaitwa usaili mwisho wa siku waziri mmoja akamnyanyulia waya meneja wa zone husika akawekwa jamaa yake bila hata usaili mpaka Leo yupo, na hii hata pale TANROAD tanga Kuna mtoto wa kigogo kachomekwa pale bila hata usaili japo ni marafiki zangu but is not fairNikupongeze kwa kuliona hilo ni kweli kuna tatizo mahala na ukiangalia Taasisi ambazo hazipelek ajira utumishi ndo zinalipa vzur na kuna watoto wa wakubwa wengi sana na viongoz wa kisiasa wanatumia loop iyo kupitisha watu wao kama Wazir flan flan anavyoweka watu wake kwenye sekta flan....!!uzi wako huu ni wa muhimu na kufuatliwa
Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja tuone mkuu, lakini wamechelewesha sana yani mpaka keroTPA wako njema Sana mkuu
Ngoja tuone mkuu, lakini wamechelewesha sana yani mpaka keroTPA wako njema Sana mkuu
Ndiyo nani huyo?haya mambo ya urasimu ndiyo yanasababisha Tanzania tuendelee pole pole...
hivi TBC watake mtangazaji.. au mtu creative.. Mirald Ayo aombe .. mumzungushe kwa taratibu ndefuuu..
Hizi ni zama za kanda ya ziwa...wengine tusubiri baada ya 2025hata trump kampa vyeo mwanae, shemeji yake,....
hata toyota.. imejaa watu wanaitwa toyota surname kibao...
yule mama chief financial officer wa huawei aliekamatwa canada sijui marekani.. baba yake ndiye mwenye huawei...
museven kawapa vyeo ndugu zake kibao
hata rais wa wanyonge nae amewakumbuka ndugu zake na wapwa na marafiki zake...
hiyo ipo kila sehemu..
ndio maana wale wanaojijua wakali huwa hawalalamiki lalamiki.. wanakomaa wenyewe kwa kujiajiri au kwa kulazimisha mpaka wanapenya wanapopataka
Tatizo taasisi zote za maana hazipitii tume ya ajiraKwenye udanganyifu kuhusu Secretariat ya ajira sidhan mana utaratibu wao uko wazi sana kama upo mdogo mno kwa hili nawapongeza Hawa jamaa kwa kweli wanatenda haki sana wasiojua tu ndo wanaweza sema kuna udanganyifu ila magufuli apa ameweka mambo sawa kabisa tumpongeze amewazuia wale walanguzi
Sent using Jamii Forums mobile app
Acha kuota...kwenye tume uhuni upo kama kawaida......halafu hao TPA wanaangalia watu wa karibu kwanzaMkuu mimi Ni shahidi kwa hili kama kuna udanganyifu Basi ujue umesukwa kweli kweli niliwahi hudhuria interview pale utumishi jamaa akazamia aseh jamaa walimfurusha ilibaki kidogo akabiziwe kwa ma pot kwa kweli wamezibiti sana yani sasa hivi sio rahisi kabisa labda wale wa kanzidata pia napo sio rahisi kiivyo, ila siwezi kukubishia yawezekana upo jikoni unajua kinachoendelea..
Mimi hapa kwenye nafasi za TPA kwakweli wamekuwa kimya sana alafu tunasubiri Aya majibu ili tuweze kufanya maamuzi sahihi mambo yangu watoe tu hata kesho roho yangu iridhike
Sent using Jamii Forums mobile app