Kwanini baadhi ya taasisi na mashirika ya umma ajira zao hazipitii Sekretariet ya Utumishi?

Kwanini baadhi ya taasisi na mashirika ya umma ajira zao hazipitii Sekretariet ya Utumishi?

Sijui hili mmeliona na moja ya legacy alioiacha Hayati Ruge ni kudepend on vyeti na gpa.

Psrp electronic system yao ikoje katika watu wanaojua kazi lakini vyeti so Sana nitie mfano labda kazi ya Customs halafu anaomba my wa clearing huyu atakuwa very competent kwenye kazi sababu Customs procedure code s zote anazijua lakini Hana bachelor labda.

Happy ndipo Tanzania wengi wanafeli unawatu wanna makaratasi makubwa na rangi nzuri lakini kazi hawajui wakingia kazini wanajifunza rushwa na upigaji tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nadhani uko nje ya ulingo, Ruge alijiajiri yeye alipambana kuona kile alichokianzisha kinasimama. Ukija kwenye ajira rasmi Kuna taratibu zake na mojawapo lazma uwe na vyeti stahiki
 
Sijui hili mmeliona na moja ya legacy alioiacha Hayati Ruge ni kudepend on vyeti na gpa.

Psrp electronic system yao ikoje katika watu wanaojua kazi lakini vyeti so Sana nitie mfano labda kazi ya Customs halafu anaomba my wa clearing huyu atakuwa very competent kwenye kazi sababu Customs procedure code s zote anazijua lakini Hana bachelor labda.

Happy ndipo Tanzania wengi wanafeli unawatu wanna makaratasi makubwa na rangi nzuri lakini kazi hawajui wakingia kazini wanajifunza rushwa na upigaji tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
Mchujo wa UTUMISHI sio masihala,kama mtu wa kubahatisha hupiti.Watu wa IT wanapiga interviews 3,written,practical ilyoshiba na Oral,sasa mtu apite chujio kama hilo alafu awe shallow mimi nakataa.Mimi mwanangu mmoja kapiga written fresh ,practical kakuta na mziki wa Linux ,kaishia kuandika namba yake ya mtihani nakuondoka.
 
Utumishi mimi nawaamini kwani jamaa zangu wengi sana wamepata ajira.Ila hizi ajira za Ngorongoro (NCCA) zilizotoka mwenyewe nina wasiwasi nazo ,najiuliza sijui niapplya au niuchune manake naweza nikachoma nauli yangu ,nikasimamisha shughuli zangu mwisho wa siku wakati nyie masubiria mpite mlango wa mbele kibarazani,kumbe kuna wenzenu wamesha ingizwa uwani zamani.
We Kwanza omba masuala ya kuchoma nauli na kusimamisha shughuli zako utajua hapo baadaye baada ya kuwa shortlisted

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchujo wa UTUMISHI sio masihala,kama mtu wa kubahatisha hupiti.Watu wa IT wanapiga interviews 3,written,practical ilyoshiba na Oral,sasa mtu apite chujio kama hilo alafu awe shallow mimi nakataa.Mimi mwanangu mmoja kapiga written fresh ,practical kakuta na mziki wa Linux ,kaishia kuandika namba yake ya mtihani nakuondoka.
Yes wako vizuri hata mm nilipata ajira yangu ya kwanza kupitia wao
 
Suluhisho ni kizifanya taasisisi zote na mashirika yote na kazi zote ziwe na ujira mzur na unaolingana kwa level flan ya elimu. Haya mambo ktk hiz taasisi ynaweza kupungua. Unakuta jamaa mmesota wote dawat moja na kakupga sna chabo, ushamuonesha sna solving zako. Mnamaliza chuo Alafu wewe unaenda kufanya kaz halmashaur mwenzio anaend BOT. Baada ya mwez tu amekupga gepu mbaya sna kimaisha. Kisa tu mmeajiriwa taasisi tofauti wakt mnalingana elimu hadi chuo mlichosoma.
Hii kwangu me naiona haijakaa sawa kabisa.

Hii kitu ni sahihi lakini kwa mfumo wa tz haitakaa itokee kamwe.
 
Hata hiyo sekretarieti ya ajira ina loop holes nyingi pia. Hakuna mfumo rasmi unaonyesha ulinganisho wa waomba ajira.

Nikupe mfano TRA wametangaza kazi huko. Mara ya pili mfululizo lakini shortlisting inasuasua wakisubiri maelekezo Toka TRA. Kumbe happy tatizo lile la wachaga kubebana Bado halijaondoka.

Sent using Jamii Forums mobile app
Nakubaliana na wewe, TPA interview zilikwishafanyika tangu wiki ya kwanza ya January lakini hicho kigugumizi cha kutangaza walioshinda usaili huo sasa ni hatari - wanasubiri "MAELEKEZO" kutoka Bandari
 
Kwa tz hii ni heri ukose vyeti ila uwe na connection.nakumbuka tulienda oale maktaba house kwa ajili ya interview moja hivi OSHA. Kumbe mtu wao wanamjua na ikishapangwa kitambo.Watu tunasubiri majibu tulikuja sikia mtu alishaanza kazi kitambo na mpka leo hii utumishi hawakutangaza matokea ya ile interview.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchujo wa UTUMISHI sio masihala,kama mtu wa kubahatisha hupiti.Watu wa IT wanapiga interviews 3,written,practical ilyoshiba na Oral,sasa mtu apite chujio kama hilo alafu awe shallow mimi nakataa.Mimi mwanangu mmoja kapiga written fresh ,practical kakuta na mziki wa Linux ,kaishia kuandika namba yake ya mtihani nakuondoka.
Kiongozi hapo kwenye IT nakubaliana nawew kabisa! Tulivyomaliza chuo tulienda interview moja tulikuwa na mwalimu wetu wa chuo nae aliitwa kwenye usahili yan ile interview ya kwanza tulipita japo kwa mbinde ila ilivokuja practical aisee ilikuwa balaa mwalimu alirud chuo kuendelea kufundisha!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchujo wa UTUMISHI sio masihala,kama mtu wa kubahatisha hupiti.Watu wa IT wanapiga interviews 3,written,practical ilyoshiba na Oral,sasa mtu apite chujio kama hilo alafu awe shallow mimi nakataa.Mimi mwanangu mmoja kapiga written fresh ,practical kakuta na mziki wa Linux ,kaishia kuandika namba yake ya mtihani nakuondoka.
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila kwa upande wa PSRP sidhani kama tatizo lao n kubwa sana.

Mimi naona chakuboresha ni namna ya kufanya Mtihani usivuje tu.

Sent from my GT-N7000 using Tapatalk
PSRP ndo taasisi gani hiyo?
 
Utumishi mimi nawaamini kwani jamaa zangu wengi sana wamepata ajira.Ila hizi ajira za Ngorongoro (NCCA) zilizotoka mwenyewe nina wasiwasi nazo ,najiuliza sijui niapplya au niuchune manake naweza nikachoma nauli yangu ,nikasimamisha shughuli zangu mwisho wa siku wakati nyie masubiria mpite mlango wa mbele kibarazani,kumbe kuna wenzenu wamesha ingizwa uwani zamani.
Imagine wanakwambia uwe na experience ya 8 or 13 years, hii si maana yake kuna mtu wamempanga tayari kabisa?😅😅
 
Habari zenu wanajamvi,
Naungana nanyi wote mlioko Tanzania kwa msiba wa kijana mwenzetu Ruge..! Hakika kazi yake ya hapa duniani ameimaliza na mungu ailaze roho yake mahali pema peponi,

Pia naona kwenye mitandao ya kijamii habari za kurudi nyumbani kwa mzee EL poleni pia mlioguswa kwa namna yeyote na huu uamuzi wake(Kama taarifa zitakuwa ni sahihi).

Niliahidi wiki ijayo siku ya alhamisi nitaleta humu uzi wa kuelezea fursa mbalimbali zilizoko nje ya nchi kwa wale watafutaji wanaoingia kihalali hili mpaka mda huu uzi ushakamilika unasubiri siku tu urushwe humu.

Leo naomba kuzungumzia ubovu uliopo kwenye michakato ya ajira unaowapa ugumu watoto wa maskini katika baadhi ya taasisi na mashirika ya umma na jinsi wakuu Hawa ambao michakato ya ajira ya taasisi zao haipitii utumishi wanavyopeana ajira kwa kujuana, ninayozungumza nina uhakika nayo kwa asilimia zaidi ya 100 maana nimefanya kazi serikalini kabla ya kuacha na kwenda nje ya nchi na nilipata kujenga connection na taasisi nyingi za serikali kwa nature ya kazi niliyokuwa nafanya hivyo Siri nyingi nilizijua.

Tangu psrs ( Sekretariati ya ajira) ianze kuratibu michakato ya ajira kwa taasisi na mashirika ya umma,. Urasimu na udanganyifu umepungua kwa kiasi kikubwa ( sio kwamba psrs haupo urasimu upo, huu urasimu nitauzungumzia siku moja), Leo nazungumzia hizi taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi.

Kuna mashirika na taasisi ambazo ajira zake hazipitii utumishi Kama TANROAD, TANAPA, HIFADHI YA NGORONGORO, TANESCO, TPDC,WCF, NSSF, na hayo mashirika yaliyounganishwa kuunda (PSSSF) pia Kuna BOT, EWURA, TAKUKURU ziko nyingi Mimi nazungumzia hizi nilizo na uzoefu nazo.

Hawa BOT Kama hauna connection pale ya kukufanya ujulikane Basi hata wakikushortlist utaenda kukamilisha ratiba tu, nafasi zikitoka pale wanaanza kuulizana wao Kama Kuna mtu ana ndgu anakidhi vigezo then wanakuscreen kwa vimemo kwa watu wote wanaohusika na huo usaili ushahidi ninao sihitaji kuuweka wazi kwa watu walioingia hapo BOT kwa mlango huu, inaweza fanya wakanijua mapema maana wengi ni watu wangu wa karibu.

Kuna Hawa TANROAD ( Hawa ni warasimu kwelikweli kwenye masuala ya ajira) kwa nature za ofisi zao hasa mikoani kote isipokuwa makao makuu Hawa ofisi zao zinakuwa jengo moja na ofisi za Temesa, TBA, TAPE na pia huwa zinapakana na GPSA na kwenye hayo magodauni ya GPSA utazikuta ofisi za MSD wamepanga humo kwa ukanda wa ofisi hizi wafanyakazi wa TANROAD na MSD ndo huonekana matawi ya juu kwa sababu wanalipwa vizuri, Safari nyingi wanapata ikiwa wafanyakazi wa ofisi zingine Kama TAPE,TBA TEMESA, na GPSA wako hoi bin taaban ( labda kwa mfanyakazi wa GPSA kituo Cha mafuta huyu Yuko njema), hivyo hii inawafanya wawe wababe kwenye ukanda wa ofisi hizi, Hawa huwachukua ndgu zao au watoto wa kike wazuri waliohitimu vyuo wanawafanya vimada wao then wanawaweka kwenye ofisi wakiwa kama wafanyakazi wanaojitolea then nafasi za kazi zikitoka TANROAD mkoa wowote ule wanaanza kuwafanyia connection Kama mkoa husika uliotangaza hakuna mtu aliye ndani anafiti vigezo, kasheshe linakuja Kama huna mtu wa kukushika mkono hata nafasi ya kujitolea hupati labda uwe msichana mrembo then wakwere wakuone ukikubali masharti Yao Basi hapo utaula, MSD na TRA zamani nao walikuwa na tabia hii baada ya michakato ya ajira yao kuhamishiwa Psrs urasimu kwenye taasisi hizi umepungua.
Ushahidi wa taasisi hizi ninao na kwa kifupi fuatilieni ajira zilizotoka mwaka Jana mikoa ya tanga, njombe na Kilimanjaro, kigoma na ruvuma na kwingineko
Hawa ni watu ninaowajua na jinsi walivyopata kazi najua kwa hiyo najua ninachokiongea kwa zaidi ya asilimia 100

TANESCO Hawa ndo walewale ukiona umepata nafasi ya kazi hapa basi ujue wamemtafta wa kumuweka wamekosa, Tena Hawa wameenda mbali mpka nafasi zao za kazi Mara nyingi huwa wanatoa Kama "INTERNAL ADVERTISEMENT" tabia hii walikuwa nayo pia TPA kabla ya michakato Yao kuhamishiwa psrs, ili kuwapa nafasi watu wao waliowaweka kujitolea, Yaani hapa utakuta baba meneja, mtoto dereva, mwipwa afisa ugavi, binamu mhasibu hawaachani na TANAPA, Hifadhi ya ngorongoro na WCF ( kwa Sasa Hawa ndo wanaolipa vizuri + malupulupu kwa taasisi za serikali) Wala NSSF.

Hizi tabia zinachangia kuwafilisi watoto wa maskini just Imagine haya mashirika yanatoa nafasi labda Kilimanjaro, mtu Yuko ruvuma Hana nauli anauza mifugo au anakopa kwenda usaili ambao wenye michakato ya ajira wanajua nani mshindi wa kazi husika.

Pia hivi vibali wanavyopewa mameneja wa taasisi kuajiri watumishi wa mikataba nashauri hapa kuwe na utaratibu mzuri. Nakumbuka ilishawahi kufanyika ofisini kwetu kulikuwa Kuna upungufu wa madereva, phone operator, mhasibu,mgavi na mhudumu wa ofisi kwa uhitaji wa watumishi Hawa tulipewa kibali tuajiri ajira za mikataba, mimi nilianda tangazo then likasambazwa kubandikwa kwenye ofisi za serikali ili watu waone waweze kuomba ilikuwa mwaka Jana na kweli watu waliomba wengi, tukaita wote usaili ukafanyika na meneja alikuwa sauti ya mwisho kwenye hizi ajira Cha kushangaza watu walioitwa kuanza kazi wote ni ule mkoa anaotoka boss, siku zilivyoenda tukaja kugundua kumbe ni jamaa zake, na hii iko karibia ofisi zote za umma kwenye hizi ajira za vibali maalumu wanawekana kwa undugu na ujamaa na hapa ndo MAUMIVU yanapokuja kwa mtoto wa mkulima na maskini ambaye kwenye familia anakuwa hana mtu wa kumuongoza.

Nini kifanyike:

Ajira zote za serikali na mashirika yake zipitie Sekretariati ya ajira katika utumishi wa umma watu washindanie huko, haina maana ya kuundwa chombo hiki halafu taasisi zingine ziendelee kuajiri zenyewe wakati zinatumia pesa za umma, maana kwa Sasa zile taasisi zinazolipa vizuri zinaajiri zenyewe na ambazo Zina Hali mbaya kimaslahi ndo ajira zake zinapitia utumishi that's why Hawa watoto wa kimaskini wakishapata ajira huko mawazo yao yanakuwa ni kuhama taasisi kwenda taasisi zinazolipa vizuri na sio kufanya kazi kwa ufanisi.

Mungu ibariki Tanzania

Maisha ya sasa ukiajiriwa bila kua na connection yoyote ni mtihani kwelikweli utasumbuka sana nadhani hii moja ya sababu ya vijana wengi hawana ajira

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mchujo wa UTUMISHI sio masihala,kama mtu wa kubahatisha hupiti.Watu wa IT wanapiga interviews 3,written,practical ilyoshiba na Oral,sasa mtu apite chujio kama hilo alafu awe shallow mimi nakataa.Mimi mwanangu mmoja kapiga written fresh ,practical kakuta na mziki wa Linux ,kaishia kuandika namba yake ya mtihani nakuondoka.
Ni kweli alinisimulia jamaa wa IT alienda kufanya usaili hapo Maktaba anasema interview nyingi halafu zile zenyewe kama kilaza hupiti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom