Dada Bite,
Beatrice Kamugisha , kwanza naomba nikusahihishe, hakuna popote rais Samia amesema katiba mpya isuburi baada ya 2025. Alichosema ni kwa sasa tumpe muda ajenge kwanza nchi.
Pili mimi ni mwana CCM na tuko wana CCM kibao tunaounga katiba mpya.
Kitu tusichokubali ni kumshinikiza Mama Samia kuwa katiba mpya lazima sasa!.
Kama hoja ya Katiba mpya ilikuwepo kwenye ilani ya uchaguzi ya Magufuli, na akasema katiba sii kipaumbele chake, akaitosa na hakushinikizwa, kwa sasa katiba mpya haipo kwenye ilani ya Samia, kumshinikiza Mama Samia kuwa katiba mpya lazima sasa ni kumuonea!.
Tusimuonee Mama yetu!.
P