Kwanini Baadhi Ya Watu Wakishafika Dar Wanakuwa Na Roho Mbaya

debbug

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2018
Posts
562
Reaction score
855
Lady and Gentleman habali za asubui .Natumain mu buheri wa afya bila kupoteza muda niende straight to the point lakin mtanisamehe Sana sababu ya huu uandishi wangu kwakweli hata mm napata tabu kuusoma sababu si uandishi mzuri.

Nilikuwa na mdogo wangu(just friend) niliekuwa naishi nae huku mkoan alikuwa fundi garage .lakin kutokan na kutafuta maisha akapata location moja ivi uko dar ya ufundi uo uo wa magari( garage) .Baada ya mda gari yangu aina ya passo ikapata matizo yaan nilikuwa nikienda umbali mrefu mfano wilaya up to mkoan inawasha taa ya oil .Mafundi wakanishauli ninunue oil pump mpya ili tubadili sasa kwa vile nilikuwa na uyo dogo uko dar nikamwambia aninunulie iyo oil pump nikamtumia Tsh 180000 ivi .Kwakweli yule dogo akaanza kunipiga chenga mala baadae,mala natuma kesho ,mala nimeenda kununua kumbe sio yenyewe mwisho akawa apokei simu wala ajibi sms zangu mwisho akatupa laini ya simu basi nikaamua kupotezea .

Wa pili ni jamaa yangu nimesoma nae tangu vidudu,chekechea,primary, secondary lakin A level tulisoma tofauti .lakin kwa sasa yeye ni msanii mkubwa tu apa bonge kwa upande wa kutegeneza bit na kuimba na kashawatengenezea wasanii kibao tu kama diamond, mavoco,rayvan,weusi ashaimba nao yaan kiufupi ni mkubwa tu kiusanii sasa uyu msanii kuna siku akanipigia simu akanambia oya vp naomba uniazime laki tatu(300000) kesho nakuludishia nikamwambia apa sina adi niende (November maik Bravo) yaan NMB tena ilikuwa usiku akanambia ninashida plz naomba nisaidie mwanangu kweli nikawasha gari yangu mpaka benki apo nikamuamishia iyo laki tatu kutoka kwenye account yang kwenda simu yake ya mkononi alafu ndio ilikuwa pesa ya emergency kama Tsh350000 nikijua huyu ni msanii mkubwa hawezi kosa laki tatu nikiitaka mda wowote .Jaman kumbe jamaa sio akaanza kupiga chenga nikimpigia simu anakata anaandika call you soon sasa apo mimi nilikua nina shida sana afu nilikuwa naumwa naitaji matunda ,nyama choma,majuic, maji kwa wingi afu sina pesa nipo geto tu nimelala namtegemea uyo msanii .kwakweli nilikoma akawa apokei simu na ajibu sms mpaka nikaamua kumpigia simu mama ili anisaidie ndio akanitumia Tsh 50000 lakin namshukuru mungu now nimepona ila uyo msanii ataki kunitumia pesa yangu sasa najiuliza kwanini? mtu ukimfanyia wema yeye anakujib kwa ubaya au kwann? mtu akifika dar anakuwa na roho mbaya ya kutokujali maisha ya mwenzake .

Naombeni ushauli jinsi yakuwakamata awa matapeli wangu kwakweli Tsh 480000 kwa usawa huu inauma San sijui nifanyeje ili wanilipe hii pesa yangu sababu inaniumiza San kichwa.

Ushauri
Enyi wanaume na wanawake wa dar maisha yakiwashida ludin tu uku mikoani usipende kuishi kiujanja ujanja haipendezi mbinguni na duniani .Yaan mmenifanya nimchukie kila mtu anaeishi dar naona kama wote wanaishi kiujanja ujanja tu .
Nawasilisha.
 
HAHAHA MKUU BANA MI NIKAJUA WANA ROHO MBAYA LABDA WACHOYO AU MAKATIRI.
Hiyo sio roho mbaya ni utapeli mkuu.Dar vyuma vimekaza sana mkuu afu huku kila kitu pesa.So nyie kina ngosha wa mikoani kueni makini mnapofanya miamara na watu wa dar.Hata kama unamuamini vipi huwezi jua amekwama vipi kwa wakati huo
 
Wengi wao njaa Kali
Wameendekeza starehe sana
Wanapenda kupendeza sana
kweli kwasababu uyu msanii nilikuja kupata za chini chini eti kumbe siku ile kulikuwa na happy birthday ya jux ndio maana sasa kwanini asiniludishie pesa yangu au atoe mtejesho ataludisha siku furan?
 
pole sana mkuu.... ila hapo naona siyo ishu ya watu wakihamia dar bali inaonekana marafiki zako wengi ni matapeli

kama huniamin embu mkopeshe rafiki yako uliyenaye huko mkoani alafu leta mrejesho ninaamini hatokulipa pia[emoji23]
apana kwakweli bora mtu nilie karibu nae kuliko mbali maana haoni tabu kuvunja lain yake tu
 
Pole sana mkuu,ila kwasasa nadhani utakua umeshajifunza na ndio kitu muhimu zaidi kwako,Mungu awe nawe na akulipe zaidi ya ulizopoteza.
 
sasa uyo nilijua ni msanii mkubwa afu ni lafiki yangu awezi nitapeli lakin ndio kawa msafara wa mbele wa kunitapeli pesa yangu kubwa sijui kwasababu sijawai fika uko dar anajua siwez kuja?
 
mkuu hiyo sio roho mbaya, hayo maziko, roho mbaya ingekuwa hawana shida ya hela hiyo wakakuchukulia ili wakukomoe. Ila nakubaliana na wewe huko mjini shida hiyo ipo.
 
njoo uamie dar!
 
walala hoi wa dar ukiona pics zao mitandaon utadhan wana utajir kama wa mmiliki wa amazon.
 
pole sana mkuu.... ila hapo naona siyo ishu ya watu wakihamia dar bali inaonekana marafiki zako wengi ni matapeli

kama huniamin embu mkopeshe rafiki yako uliyenaye huko mkoani alafu leta mrejesho ninaamini hatokulipa pia😂
Hahaa amkopeshe mtu mwingine tena" naona una hamu ya kumuua mwenzio wewe
 
Sawa( NOVEMBER MICK BRAVO) NMB ...tumekusikia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…