Kwanini baadhi ya watu wanaichukia pombe wakati hawaitumii!?

Kwanini baadhi ya watu wanaichukia pombe wakati hawaitumii!?

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,623
Reaction score
8,442
Kama swali linavyouliza hapo juu

Nashangaa mtu hanywi pombe Lakini anadiriki kuichukia na kumsema vibaya mnywaji

Hapa duniani kila mtu ana starehe yake ,kuna wapenda mademu,kuna wapenda bangi,kuna wapenda unga na kadhalika ili mradi tu upate ile kitu roho inapenda

Sasa kuna mijitu inaona wale wanaokunywa pombe ni waovu,hawafai katika jamaii, na kuwaona kama watu wasio na akili ya maisha

Wanaona ukinywa pombe basi utakua maskini hutopata maendeleo ,kumbe kila MTU na malengo yake na unywaji wake anajua nini anafanya

Watu tuache unafiki kuhukumiana,mwenye mamlaka ya kumuhukumu MTU mnywaji ni mungu pekee

Acha watu tunywe tuburudike,hiyo starehe unayoipata wewe pale unapokunywa soda basi ndo hiyo hiyo ninayoipata Mimi pale ninapokunywa Balimi zangu za bariiiidi kabisa

Tusipangiane Maisha na usihukumu kabla hujahukumiwa

Cheers[emoji481][emoji481][emoji481]
 
Mimi nimeanza kugonga mitungi way back kitambo bado chalii sana na Moshe zangu zinasonga kama kawa sijawahi zingua mzee.

Ila nashangaaga sana unakutana na mtu ndezi tu afu anakuona wewe unaepiga mitungi unazingua wakati ukishalewa unanyooka mpaka geto hujawahi kumsumbua sababu umelewa na wala hujawahi muomba hela ya mitungi.

Tuvumiliane tu jamani hatuwezi fanana
 
Afadhali umejijibu, kumbe umeelewa kuwa kuna baadhi husumbua baada ya kulewa.

Hapo ni sawa na kusema wachaga bahili sana, sio wote ila kuna baadhi etc
 
Inategemea na mnywaji husika, binafsi sipendi kukaa karbu ya au na mtu mlevi mropokaji, bora awe mlevi mkaa kimya apo tutaendana
 
Matumizi ya pombe kupita kiasi siyo nzuri kwa afya yako...

Tatizo binadamu ni wabishi sana...

Cc: mahondaw
 
Cha P [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji125][emoji125]
 
Madhara ya pombe hayaji kwa anaye kunywa bali asiye kunywa, hivi umesha wahi kuishi na mlevi wa pombe, alafu akakutapikia umelala usiku, au ushawahi ishi na mlevi mfano mtu mwenye majukumu ya familia alafu anadhamini pombe wakati familia haina hata chakula, utaipenda pombe unadhani ?
 
Kama swali linavyouliza hapo juu

Nashangaa mtu hanywi pombe Lakini anadiriki kuichukia na kumsema vibaya mnywaji

Hapa duniani kila mtu ana starehe yake ,kuna wapenda mademu,kuna wapenda bangi,kuna wapenda unga na kadhalika ili mradi tu upate ile kitu roho inapenda

Sasa kuna mijitu inaona wale wanaokunywa pombe ni waovu,hawafai katika jamaii, na kuwaona kama watu wasio na akili ya maisha

Wanaona ukinywa pombe basi utakua maskini hutopata maendeleo ,kumbe kila MTU na malengo yake na unywaji wake anajua nini anafanya

Watu tuache unafiki kuhukumiana,mwenye mamlaka ya kumuhukumu MTU mnywaji ni mungu pekee

Acha watu tunywe tuburudike,hiyo starehe unayoipata wewe pale unapokunywa soda basi ndo hiyo hiyo ninayoipata Mimi pale ninapokunywa Balimi zangu za bariiiidi kabisa

Tusipangiane Maisha na usihukumu kabla hujahukumiwa

Cheers[emoji481][emoji481][emoji481]
Inawezekana pombe ukanywa wewe halafu harufu mbaya wakanusa wengine, sasa hapo napo utashangaa wanavyoichukia hiyopombe tu?

Mimi sichukii pombe (pombe ni dawa ya mafua na inaua bacteria ikitumiwakwa dozi sahihi, ndiyo maana dawa nyingi za vidonda zina alcohol). In fact nakunywa kwa kipimo changu (double double highland single malt Scotch Whisky), lakini nakueleza tu kwamba si lazima mtu aitumie ili aichukie.

Inawezekana anaichukia ndiyo maana haitumii.
 
uharamu wa pombe ni matendo yenu,,,,mpo wengine mkilewa Mnalia bila sababu,,wengine mnacheza na kuimba kwa sauti ya juu tena 8BILA KUWA NA MUZIKI usiku wa manane ,,,wengine mnaanguka mtaroni huku kichwa kipo mtaroni na mwili upo barabarani MSAMBWANDA wote upo juu,,,,mbaya zaidi asubuhi mkiingia chooni HARUFU BALAA,,,wengine hamuoni mmelewa hadi MTUKANE WATU,,,AU MPIGWE NGUMI ZA USO,,,,
 
Back
Top Bottom