Prim K
Member
- Jul 19, 2016
- 14
- 8
Jitihada za kupunguza matatizo na vifo kwa mama wajawazito ni kipaumbele dunianii kote, jitihada hizi zinatiliwa mkazo Zaidi kwenye nchi zinzoendelea kama Tanzania. Mwaka 2015 shirika la afya duniani WHO limeripoti vifo vya wamama wajawazito 830 kila siku kwa sababu ya matatizo wakati wa ujauzito,
Jitiada nyingi zmefanyika kupunguza kadhaha hii, moja kati ya hizo ni ushiriki wa wanaume kwa kuwapeleka wenza wajawazito kliniki,kwani imeonekana inachangia kwa kiasi kikubwa afya ya mama wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua, baada ya kujifungua na hata kwenye malezi ya watoto.
Kwenye jamii nyingi za kaifrika wanaume ndio watoa maamuzi kwenye mambo mengi ndani ya familia, ila wamekua nyuma sana kujihusisha kwenye afya ya wenza wao hasa wakati wa ujauzito, na wamekua wakipinga sana kuwapeleka kliniki kwani wanaona inapingana na tamaduni zao, hii ni sababu ya kivivu, kukwepa majukumu na sababu isiyo na mashiko. Barani ulaya, ushiriki wa wanaume kwenye afya ya mama mjazito na kumpeleka kliniki upo juu sana na unachangia kwa kaisi kikubwa kwenye afya ya mjamzito na kupunguza vifo vya kina mama.
Tafiti mbali mbali zimefanyika kuangalia umihimu wa wanaume kuwapeleka wanawake wajawazito kliniki,tafiti zimefanyika sehemu mbalimbali dunia na zote zinaleta majibu sawa, imeonekana ushiriki wa wanaume una faida nyingi kama zifwatazo;
Idadi ya kliniki, ushiriki wa wanaume unaongeza namba za kwenda kliniki kwa wajawazito, takribani mara 4 zaidi ya wale ambao hawasindikizwi kliniki(chuo cha Cambridge 2020). Clinic za wajawazito hua kunatolewa elimu na umuhimu wa kuhudhuria kliniki mara kwa mara, na wanapewa tarehe za kaurudi, hivyo baba hua kama sehemu ya hamasa na kumkumbusha mama kwenda kliniki. Mara nyingine wanaume huchangia usafiri na chakula wakati wa kwenda na kurud kliniki.
Huimarisha afya ya mama mjamzito na kumwepusha na magonjwa mbalimbali wakati wa ujauzito. Mwanaume nae anapata na kushiriki elimu ya afya ya mama mjamzito akienda kliniki, mfano elimu ya lishe bora kwa mjamzito, vitu vya kuepuka akiwa mjamzito kama pombe, sigara na baadhi ya dawa. Pia huweza kuelewa dalili hatari kwa mama mjamzito na muda gani wa kwenda hospitali ata bila ya tarehe ya kliniki kufika.
Husaidia mjamzito kujifungua hospitalini. Kuna umuhimu mkubwa kwa wajawazito kujifungua hosipitalini, wanaume hua ni msaada kwa kuwapeleka hospitlini pale wanapopata uchungu, na wanaume wanaelimishwa umuhimu ya kujifungulia hospitalini. Mwanaume pia anashiriki kwenya maandalizi ya kujifungua kwa mjamzito, na kumpa mama sapoti ya kiakili pale wanapokumbwa na woga wa kujifungua.
Matunzo baada ya kujifungua, mwanaume huweza kujifunza mambo muhimu ya kufanya kwa mama na mtoto mara baada ya kujifungua, kama sapoti ya kiakili, kuepusha sonona baada ya kujifungua, na magomjwa yanayoweza kutokea baada ya kujifungua, chakula muhimu kwa mjamzito ili mama atoe maziwa ya kutosha kwa mtoto, na kuhakikisha mtoto anapata chanjo zote.
Furaha kwa mama mjamzito, raha ya mama mjamzito aone upendo usio na kifani kutoka kwa mwenza wake, ile kumjali, kumpatia anacho omba, kumpeleka kliniki na kumsaidia majukumu ndani ya nyumba hua ni Amani tosha kwake. Furaha, Amani na afya ya akili huchangia pia afya ya mtoto na kumwepusha mama na maudhi madogo madogo ya mimba. Msongo wa mawazo wakati wa ujauzito huweza kupelekea mimba kutoka.
Upendo wa baba na mtoto, mara nyingi upendo hua mkubwa kwa vitu ambavo tumevipigania na kugaramia, hivyo mtoto ambae umempigania na kumhudumia tangu yupo tumboni, akizaliwa utaendelea kumpenda na kumjali.
Hitimisho, mwanume kushiriki kwenye afya ya mama mjamzito (mwenza) huchangia sana kwenye afya na kuepusha magonjwa na vifo kwa mama wajawazito. Mwanaume ukishajua kuwa umempa mwanamke mimba, bila kujali unampango nae au huna, bila kujali umempaje mimba ni jukumu lako kuijali na kihudumia mimba mpaka mtoto azaliwe na uendelee kumlea. Wazungu wasema 'a man must take responsibilities for his actions'.
Asanteni.

Upvote
2