Kwanini bado unatumia Vocha za kukwangua, na baada ya kuitumia huwa unaifanya nini?

Kwanini bado unatumia Vocha za kukwangua, na baada ya kuitumia huwa unaifanya nini?

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
378
Reaction score
766
1738563787444.png

Kwa namna ambavyo teknolojia inavyokuwa Watu wengi siku hizi hawatumii tena vocha za kukwangua lakini kuna wachache ambao bado watumia vocha hizo ili kuweza kuongeza salio na kununua vifurushi kwenye simu zao.

Je, ni kwanini bado unatumia vocha za kukwangua kwa kipindi hiki ambacho dunia inaelekea kwenye uchumi wa pesa za Kidijitali (cashless economy)?

Kwa wanaotumia vocha za kukwangua unajua madhara yake ikiwa utatumia na kutupa vocha hizo bila ya kuichana na kuiharibu kabisa?

Ukimaliza kutumia vocha ya kukwangua usiitupe hovyo kwani mtu anaweza kutrace na kupata taarifa binafsi za mhusika aliyetumia vocha hiyo. Taarifa kama vile kama vile anwani ya barua pepe, namba ya simu na jina lako vinaweza kupatikana . Hapa ni baadhi ya njia ambavyo hili linaweza kutokea:
  1. Ikiwa vocha imetolewa mtandaoni na unahitajika kuunda akaunti, taarifa zako binafsi (jina, barua pepe, nk) zinaweza kuunganishwa na vocha hiyo. Ikiwa mtu atapata akaunti yako, anaweza kufuatilia au kupata vocha ulizotumia.​
  2. Baadhi ya vocha zina namba maalum "tracking codes" ambazo zinaweza kufuatiliw kwa mtu aliyetumia vocha hiyo​
  3. Ikiwa vocha imetumwa kupitia barua pepe, njia za ufuatiliaji zinaweza kutumika kuona nani alifungua barua pepe hiyo, aliye bonyeza kiungo cha vocha, au aliyeitumia vocha.​
  4. Ikiwa vocha imetumika wakati wa muamala, muuzaji au mtoaji wa huduma anaweza kuwa na taarifa kama vile njia ya malipo ya mnunuzi, eneo, na historia ya agizo, hivyo kuunganisha ununuzi na mtu fulani​
Ili kulinda taarifa zako binafsi, epuka kutupa vocha hovyo.

Huwa unatupa vipi vocha baada ya kumaliza matumizi nayo?​
 
Eeh bado mnakwangua vocha miaka hii? mna,shida gani watu? huvi kwa nini mnapenda kujitesa hivo? sjui hata nina miaka mingapi sijawahi hata ishika hiyo ya karatasi.
 
Tunaoishi maisha ya kizamani bado tunatumia vocha na hatuchani tukiishaingiza namba tunatupa hovyo, ila kwa sasa itabidi tuwe tunazichana
 
Mh! wenyewe wachunguze tu si wamekosa kazi yakufanya!
 
Hakuna haja ya kutumia vocha ya kukangua kwa siku za leo
 
Back
Top Bottom